WHO yaripoti visa 30,000 vinavyoshukiwa kuwa vya MPOX barani Afrika, haswa nchini DRC
Takriban watu 30,000 wanaoshukiwa kuwa na virusi vya MPOX wameripotiwa barani Afrika kufikia sasa mwaka huu, wengi wao wakiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC),Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO) lilisema Jumatatu.
Zaidi ya watu 800 walikufa kwa kushukiwa kuwa na Mpox katika bara la Afrika, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilisema katika ripoti yake.
Nchi jirani wa Kongo kama vile Burundi pia imekumbwa na mlipuko unaokua kwa Kasi, Ripoti ya WHO iliongeza.
Mpox inaweza kuenea kupitia mawasiliano ya karibu(Close contact). Inaweza kuonyesha dalili za Kawaida, lakini ni hatari na inaweza kusababisha Vifo katika hali za nadra. Kwa kawaida husababisha dalili zinazofanana na mafua na vidonda vilivyojaa usaha mwilini.
#SOMA ZAIDI hapa Kuhusu Ugonjwa wa Mpox na Dalili Zake
Taarifa ya WHO haikutoa takwimu linganishi za miaka iliyopita.
Shirika la afya ya umma la Umoja wa Afrika(The African Union's public health agency) limesema visa 14,957 na vifo 739 viliripotiwa kutoka majimbo saba yaliyoathirika mwaka 2023 - Sawa na ongezeko la asilimia 78.5 la kesi mpya kutoka 2022.
Kulikuwa na kesi 29,342 zinazoshukiwa na vifo 812 kote barani Afrika kuanzia Januari hadi katikati ya Septemba mwaka huu, kulingana na ripoti ya WHO.
Jumla ya kesi 2,082 zilizothibitishwa ziliripotiwa kote ulimwenguni mnamo Agosti pekee, idadi kubwa zaidi tangu Novemba 2022.
Siku ya Jumamosi, mfuko wa Benki ya Dunia wa janga la ugonjwa huu(World Bank's pandemic fund) ulisema utatoa dola milioni 128.89 (euro milioni 115) kwa nchi kumi za Afrika kusaidia kupambana na mlipuko huo.
Reviewed via;
- Shirika la Afya Duniani(WHO)
- Reuters
- Shirika la afya ya umma la Umoja wa Afrika(The African Union's public health agency)
- https://www.rfi.fr/en/africa/20240924-who-reports-30-000-suspected-mpox-cases-in-africa-mainly-in-drc
-https://www.afyaclass.com/2024/09/ugonjwa-wa-homa-ya-nyanichanzodalili-na.html?m=1
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!
Emoji