Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa Wa Homa ya Nyani,chanzo,dalili Na Tiba yake




Ugonjwa Wa Homa ya Nyani,chanzo,dalili Na Tiba yake

Ugonjwa wa homa ya nyani au Mpox ni ugonjwa ambalo unasababishwa na virusi, Ugonjwa huu unasababishwa na virusi ambao hujulikana kwa jina la Mpox ambapo hapo awali vilijulikana kama MonkeyPox. Mpox Virus wapo kwenye kundi la Orthopoxvirus genus ndani ya familia ya Poxviridae.

Ugonjwa wa homa ya nyani kwa binadamu(Human Mpox),Mara ya kwanza kabsa uliripotiwa Mwaka 1970 nchini DRC(Democratic Republic of the Congo) kwa kijana mmoja wa Miaka 9 aliyekuwepo kwenye eneo ambalo ugonjwa wa Smallpox ulishaondolewa tangu mwaka 1968. Ndipo visa vingine vikaanza kuripotiwa na maeneo mengine, (Disease history Source:WHO)

Dalili za Ugonjwa wa Homa ya Nyani

DALILI ZA UGONJWA HUU WA Homa ya Nyani NI PAMOJA NA;

– Mtu kuwa na homa pamoja na mwili kutetemeka

– Kupata maumivu makali ya kichwa

– Mwili kuchoka kupita kawaida

– Mwili kukosa nguvu na kuwa dhaifu sana

– Lymph nodes kuanza kuvimba ambapo kwa lugha nyingine hujulikana kama lymphadenopathy

– Kupata maumivu ya viungo,joints pamoja na misuli ya mwili

– Kupata maumivu ya mgongo(back ache)

– Kutokewa na UPELE kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wako kama vile; Usoni, kwenye mikono pamoja na viganja vya mikono,
miguuni,machoni,,mdomoni,sehemu za siri n.k

Upele huu unaweza kuwasha sana, na hata baadae huweza kutumbuka kabsa,

Mwili huweza kubaki na makovu au alama alama.

UGONJWA HUU WA HOMA YA NYANI(MPOX) husambaa kutokana na ukaribu(Close contact) kwa mtu,wanyama au vitu ambavyo tayari vina virusi hawa wa Mpox.

Unaweza kuupata kwa njia ya ya mgusano sehemu zenye majeraha, kupitia body fluids zote kama vile damu,mate,jasho n.k, kutoka kwa Mtu au wanyama wenye Virusi hawa(Mpox virus).

Virusi vya MPox vinaweza kuingia mwilini kupitia kwenye ngozi iliyo na jeraha au michubuko yoyote, au kwa njia nyingine kama vile njia ya upumuaji au kupitia macho, pua pamoja na mdomo.

Pia Uenezwaji wake unaweza kuwa  kwa kugusana na wanyama walioambukizwa kama vile nyani, panya na kindi ,kupitia vitu kama vile matandiko au nguo za mgonjwa mwenye virusi hawa.

- Ugonjwa wa Homa ya Nyani unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine kwa njia zifuatazo; kupitia maji maji ya mwili ikiwemo mate, matapishi, jasho, mkojo, matone ya mfumo wa njia ya hewa na ngozi kupitia kugusana na kujamiana na mtu mwenye maambukizi ama kutumia vifaa, matandiko au kugusa sehemu zilizo na vimelea vya ugonjwa huu. Aidha, ugonjwa huu unaweza pia kuenezwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

- Dalili kuu ya Homa ya Nyani ni upele, malengelenge au vidonda kwenye mwili hasa, mikono na miguu, kifuani, usoni na wakati mwingine sehemu za siri. Dalili nyingine ni homa, uchovu, maumivu ya kichwa, misuli, mgongo, uchovu na kuvimba mitoki.

- Ugonjwa huu wa homa ya nyani haujaingia nchini, hivyo, ni vyema tukashirikiana kuhakikisha nchi yetu inabaki kuwa salama. Wizara inatoa tahadhari kwa Wananchi wote kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa wa huu kwa kutekeleza yafuatayo;-

i. Kutoa taarifa kupitia namba 199 bila malipo endapo utamuona mtu mwenye dalili za Homa ya Nyani(Mpox).

ii. Kuepuka kugusa majimaji ya mwili au ngozi ya mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Homa ya nyani(Mpox).

iii. Kuepuka kusalimiana kwa kupeana mikono, kukumbatiana na kubusiana mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa homa ya nyani(Mpox).

iv. Kuepuka kugusana na mtu yeyote mwenye dalili za ugonjwa wa Homa ya Nyani(Mpox).

v. Kunawa mikono kila mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono.

vi. Epuka kula au kugusa mizoga au wanyama mfano nyani au swala wa msituni.

vii. Safisha na kutakasa vyombo vilivyotumika na mhisiwa au mgonjwa pamoja na maeneo yote yanayoguswa mara kwa mara.

viii. Kuvaa barakoa iwapo itabidi kukaa na kuongea kwa karibu na mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Homa ya Nyani(Mpox).

ix. Kuwahi katika vituo vya huduma za afya unapoona dalili za ugonjwa wa Homa ya Nyani(Mpox).

x. Watoa huduma za afya kuzingatia miongozo ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi (IPC) wakati wote wanapowahudumia wagonjwa.

MATIBABU YA UGONJWA WA HOMA YA NYANI

Ugonjwa huu wa Homa ya Nyani hauna tiba(no cure),bali watalaam wa afya hudhibiti dalili zinazotokana na ugonjwa huu wa homa ya nyani.

Kwa Sasa Shirika la Afya Duniani(WHO) limeidhinisha Chanjo za Kutumika Kuzuia Ugonjwa huu wa Homa ya Nyani. #SOMA Zaidi hapa Kuhusu WHO na Chanjo hii ya Mpox

Hata hivo ugonjwa huu huisha wenyewe kwa kipindi flani baada ya kumpata mtu.

Fahamu pia,Maambukizi haya ya ugonjwa wa homa ya nyani(Mpox) huisha yenyewe na hudumu kati ya siku 14 na 21.


Mpox ni nini? Mpox/Homa ya Nyani

Kumekua na mlipuko barani Africa, nchi za jirani pia zimetangaza kua na wagonjwa wa mpox. Hivi karibuni hata mabara mengine yameanza kutangaza uwepo wa ugonjwa huu kwa kasi, hiii imepelekea WHO kuutangaza ugonjwa wa homa ya nyani kama janga la kimataifa. Hata hivyo nchini Tanzania bado hakujatangazwa kupatikana kesi ya ugonjwa huu.

Homa ya nyani ni ugonjwa unaosababishwa na virusi.virusi hivi ni familia moja na virusi vinavyosababisha smallpox au ndui kwa kiswahili.

Tuone historia ya Homa ya nyani kifupi.

Homa ya nyani sio ugonjwa mpya, umegundulika mwaka 1958 katika nyani waliokua wakifanyiwa tafiti. Kesi ya kwanza ya homa ya nyani kwa binadamu iligundulika mwaka 1970 nchini  DRC.

Tangu wakati huo kumekua na kesi chache barani africa hasa  africa ya kati na afrika ya magharibi. Lakini mwaka 2022 tumeanza kuona ugonjwa huu ukienea kwa kasi maeneo ambayo sio endemic na hata nje ya bara la Africa.

Ugonjwa wa Homa ya Nyani Unaambukizwaje

  1. Mji maji au mate yanatotoka kinywani wakati wa Kuongea, kukohoa au kuoiga chafya. (Droplets)
  2. Aina zote za ngono zinaweza kuambukiza, hii inajuimuisha kumbusu mtu mwenye mpox(All forms of sexual contact including kissing)
  3. Kukutana au kugusana ngozi na mtu mwenye homa ya nyani (Skin to skin contact)
  4. Kuvaa nguo au kutumia mashuka na foronya za mtu mwenye homa ya nyani. (Sharing clothes and/or bedding)
  5. KUgusa au kula wanya walioathirika au mizoga.

Dalili za Ugonjwa wa Homa ya Nyani

  1. Upele (una wezakutokea kwenye ngozi, mdomoni, ukeni, au ndani ya njia ya haja kubwa)
  2. Homa
  3. KUskia maumivu kwenye koo. (Sore throat)
  4. Maumivu Kichwa
  5. Maumivu ya Misuli
  6. Maumivu ya mgongo
  7. Uchovu wa kupitiliza usio elezeka
  8. Kuvimba tezi

Tiba na chanjo ya Ugonjwa wa homa ya Nyani

  1. Homa ya nyani isiokua na dalili kali (severe) hupona yenyewe ndani ya wiki 2-4 ( self limiting)
  2. Nenda kituo cha afya kuhakiki kama ni mpox na sio kitu kingine.
  3. Matibabu ya upele na kutibu dalili zingine kama homa kali na maumivu ya misuli yanaweza kupatikana

Chanjo ya homa nyani ipo lakini bado haipatikani nchi nyingi za Africa.

Watu walio katika hatari Ya kupata Homa ya nyani yenye Dalili Kali (severe).

  1. Watoto chini ya mwaka mmoja
  2. Wajawazito
  3. Watu wenye upungufu wa kinga mwilini.

Watu walio katika hatari ya kupata homa ya nyani

  1. Watoa huduma ya afya
  2. Wanaofanya kazi katika mkusanyiko/msongamano  wa watu wengi
  3. Watu wenye wenza wengi ( multiple sexual partners)
  4. Watu wenye kujihusisha na biashara ya ngono
  5. Wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja pia wametajwa kuwa na hatari ya kupata.

Jinsi ya kujikinga na Ugonjwa wa Homa ya Nyani

  1. Epuka sehemu zenye msongamano  ambazo utagusana na watu
  2. Nawa mikono kabla ya kujigusa, kula, au unapotoka kwenye mizunguko
  3. Tumia kinga wakati wa kujamiiana
  4. Epuka kugusa wanyama wanaumwa au mizoga bila kujua ugonjwa au sababu ya kifo.

Jinsi ya kuwalinda wengine endapo wewe umeathirika na Ugonjwa wa Homa ya Nyani.

  1. Kaa nyumbani au katika chumba chako mwenyewe kama inawezekana.
  2. Osha mikono mara nyingi kwa sabuni na maji au na vitakasa mikono, hasa kabla au baada ya kugusa vidonda.
  3. Vaa barakoa na funika vidonda unapokuwa karibu na watu wengine hadi upele wako upone.
  4. Weka ngozi yako kavu na bila kufunikwa (isipokuwa unapokuwa chumbani na mtu mwingine).
  5. Epuka kugusa vitu katika maeneo ya pamoja na safisha maeneo ya pamoja mara kwa mara.
  6. Fuata maelekezo ya daktari katika kutibu vipele/vidonda.
  7. Tumia dawa za kupunguza maumivu zinazopatikana bila agizo la daktari kama vile paracetamol au ibuprofen.

 Nini cha kuepuka kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Nyani

Kupasua au kukuna vipele/malengelenge. Hii inaweza kuweka vijidudu kwenye vidonda na kusababisha vishambuliwe na bakteria au kuchelewa kupona kwa vidoonda. Au kusambaza zaidi mwilili.

Kwa Taarifa, msaada na ushauri zaidi piga simu namba 199

Credits|Article By;

Dr Ladina Msigwa