Vipele Sehemu Ya Siri,Vipele Ukeni, Vipele Kwenye Uume Afyaclass Bongo Social •

VIPELE SEHEMU YA SIRI,VIPELE UKENI, VIPELE KWENYE UUME 

Vipele kwenye Uume:

Vipele Kwenye Uume: Chanzo, Dalili na Matibabu

Tatizo la vipele kwenye uume ni hali inayowapata wanaume wengi duniani kote. Hali hii inaweza kuathiri sana afya ya mwili na akili ya mtu.

Kwa bahati mbaya, wanaume wengi hawajui kuhusu hali hii na wanashindwa kutafuta matibabu sahihi,

Makala hii inalenga la kutoa elimu kuhusu Tatizo la vipele kwenye uume, ikiwa ni pamoja na sababu za hali hii, dalili zake na matibabu.

Sababu za Tatizo la vipele kwenye uume:

Tatizo la vipele kwenye uume Linaweza kusababishwa na sababu mbalimbali. Sababu hizo ni pamoja na:

- Tatizo la Balanitis,kuvimba kwa kichwa cha Uume,

Hii hutokea sana kwa wanaume ambao hawajatahiriwa, kama hujafanyiwa tohara ni ngumu sana kusafisha vizuri ngozi ya chini kabsa kwenye uume,

Bacteria, jasho pamoja na seli za ngozi zilizokufa hujikusanya na kufunika eneo hili, hii huweza kupelekea miwasho,vipele,ngozi kuwa nyekundu pamoja na uchafu kutoka chini ya ngozi ya mbele ya Uume(foreskin).

- Tatizo la ngozi linalojulikana kama Contact Dermatitis, ngozi huwa nyekundu,kuwasha au kuwa na vipele

- Kuwa na Mzio au allergic reaction juu ya vitu mbali mbali ikiwemo dawa, vitu vyenye kemikali kama sabuni za kuogea,mafuta n.k

- Kuwa na tatizo la Genital Psoriasis,

- Kuwa na tatizo la Scabies

- Magonjwa ya Zinaa-Sexually Transmitted Diseases (STDs) ikiwemo;

  • Ugonjwa wa kaswende(Syphilis),
  • Genital herpes n.k

- Mashambulizi ya Fangasi sehemu za Siri(Yeast Infection), pia huweza kusababisha miwasho pamoja na vipele.

- Maambukizi ya Bakteria au Virusi: Maambukizi ya bakteria au virusi kwenye sehemu za siri kama vile uume, yanaweza kusababisha vipele kwenye uume. Bakteria na virusi hao hupata nafasi ya kuzaliana kwenye uume na kusababisha vipele zaidi.

- Kuwa na Ngozi Kavu: Ngozi kavu kwenye uume inaweza kusababisha vipele. Hii ni kwa sababu ngozi kavu hupasuka na kuacha nafasi ya bakteria na virusi kuzaliana kwa urahisi zaidi.

- Kutumia Dawa: Baadhi ya dawa zinaweza kusababisha vipele kwenye uume. Dawa hizo ni pamoja na dawa za kulevyia,  baadhi ya antibiotics, na dawa zingine zinazotumika kutibu magonjwa mbalimbali.

Dalili za Tatizo la vipele kwenye uume:

Dalili za Tatizo la vipele kwenye uume hutofautiana kulingana na sababu ya hali hii. Hata hivyo, dalili za kawaida za Tatizo hili ni pamoja na:

• Kuvimba kwa uume: Hii ni dalili ya kawaida ya Tatizo la vipele kwenye uume. Uume unakuwa mkubwa kuliko kawaida na unaweza kuuma.

• Kuwasha: Tatizo la vipele kwenye uume linaweza kusababisha kuwasha kwenye ngozi ya uume.

• Kuvimba kwa korodani:Tatizo la vipele kwenye uume linaweza kuambatana na kuvimba kwa korodani.n.k

Matibabu ya Tatizo la vipele kwenye uume:

Matibabu ya Tatizo la vipele kwenye uume hutofautiana kulingana na sababu ya hali hii. Hata hivyo, matibabu ya kawaida ni pamoja na:

Kutumia Dawa: Kwa tatizo la vipele kwenye uume linalosababishwa na maambukizi ya bakteria au virusi, daktari anaweza kuagiza dawa za kupambana na maambukizi hayo.

Dawa hizi zinaweza kuwa za kupaka kwenye uume, au kutumika kwa njia ya mdomo.n.k

Jinsi ya kuzuia Tatizo la Vipele kwenye uume:

Kuzuia Tatizo la vipele kwenye uume ni muhimu kwa afya ya uume na mwili kwa ujumla. Hatua za kuzuia hali hii ni pamoja na:

1. Kuvaa nguo za ndani safi: Kuvaa nguo za ndani safi na kubadilisha mara kwa mara ni njia moja ya kuzuia maambukizi ya bakteria na virusi.

2. Kuepuka kugusa uume bila kuosha mikono: Kuosha mikono kabla ya kugusa uume ni muhimu sana kuzuia kuenea kwa bakteria na virusi.

3. Kuepuka kushiriki ngono bila kinga au Condom: Kujikinga wakati wa kushiriki tendo la ndoa ni njia mojawapo ya kuzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ikiwa ni pamoja na magonjwa yanayosababisha dalili hii ya vipele kwenye uume.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Kuota vipele kwenye mashavu ya uke:

vipele kwenye mashavu ya uke huweza kusababishwa na sababu nyingi mbali mbali ikiwemo matatizo ya ngozi,maambukizi ya magonjwa n.k,

Dalili za vipele kwenye mashavu ya uke

Kwa kawaida dalili za vipele kwenye mashavu ya uke huambatana na muwasho wa mara kwa mara, na hali hii ya muwasho huzidi kuongezeka au kuwa mbaya Zaidi pale unapojikuna eneo husika.

Kwa Ujumla dalili za vipele kwenye mashavu ya uke ni pamoja na;

  • Kupata muwasho au kuhisi kuungua sehemu ya upele kuota
  • Kutokea kwa vipele vinavyoonekana kwa macho
  • Kuwa na malengelenge au vidonda
  • Ngozi kuwa na mabaka mabaka
  • Kuvimba kwa ngozi
  • Wengine hupata homa

vipele kwenye mashavu ya uke huweza kuambatana pia na;

– Uchafu wenye harufu mbaya kutoka ukeni

– Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa n.k

Chanzo cha vipele kwenye mashavu ya uke

Asilimia kubwa tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke ni tatizo ambalo hutibika na husababishwa na sababu za kawaida, Ingawa wakati mwingine huweza kuwa tatizo Sugu na ambalo halitibiki kulingana na chanzo chake.

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu za vipele kwenye mashavu ya uke;

1. Matatizo ya Ngozi kama vile Contact dermatitis,

Tatizo hili la ngozi ni miongoni mwa matatizo yanayosababisha vipele kwenye mashavu ya uke kwa kiasi kikubwa.

Baadhi ya Tafiti za Mwaka 2014 zilionyesha Contact dermatitis huhusika na tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke kwa karibu asilimia 50% ya wanawake wenye shida hii.

2. Tatizo la kuvimba kwa Uke au mashavu ya Uke(Vaginitis au vulvovaginitis),

kwa mujibu wa vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa “the Centers for Disease Control (CDC)”, moja ya chanzo kikubwa cha tatizo hili ni maambukizi ya bacteria au fangasi.

3. Maambukizi ya Fangasi-Yeast infections (Candida),

Watu wengi wenye vipele kwenye mashavu ya uke pia hutokana na maambukizi ya fangasi sehemu za siri hasa fangasi ambao hujulikana kama Candida albicans.

4. Magonjwa ya Zinaa kama vile Trichomoniasis (trich),

Tatizo hili huweza kusababishwa na protozoan parasite na husambazwa kwa njia ya kujamiiana.

Tiba ya Trichomoniasis ni pamoja na matumizi ya antibiotics

5. Tatizo la Psoriasis

Psoriasis ni tatizo kwenye mfumo wa kinga ya mwili(autoimmune condition) ambalo matokeo yake huathiri ngozi ikiwemo ngozi ya Sehemu za Siri.

Tatizo hili huweza kuwa chanzo cha vipele kwenye mashavu ya uke au vidonda(Psoriasis lesions),

Lakini tatizo hili la Psoriasis haliwezi kuathiri sehemu ya ndani ya Uke.

6. Maambukizi ya Virusi- Molluscum contagiosum

Molluscum contagiosum ni maambukizi ya Virusi ambayo kwa asilimia kubwa hushambulia ngozi, maambukizi haya huweza kusambaa kwa njia ya kujamiiana n.k,

Moja ya dalili zake ni kusababisha upele(bumps) wenye ukubwa wa millimeters kati ya 2 mpaka 5 (mm).

7. Ugonjwa wa Scabies

Moja ya dalili kubwa za ugonjwa wa Scabies ni kusababisha vipele kwenye ngozi ambavyo huweza kuambatana na muwasho,

Hivo wanawake wenye ugonjwa wa Scabies huwezs kupata tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke.

8. Kuwa na Chawa Sehemu za Siri(Pubic lice)

Chawa Sehemu za siri(Pubic lice) ni wadudu jamii ya parasite wadogo sana ambao huweza kuathiri nywele za Sehemu za Siri na chakula chao kikubwa ni damu ya binadamu.

Unaweza kuwapata baada ya kujamiiana na mtu mwenye hawa chawa, au kupitia nguo,mashuka,taulo za kuogea n.k kutoka kwa mtu mwenye chawa.

Wadudu hawa huweza kusababisha hali ya muwasho sehemu za Siri na eneo la mashavu ya Uke kwa ujumla.

Chawa Sehemu za Siri(Pubic lice) huweza kutibiwa na dawa kama vile permethrin (Nix).

9. Maambukizi ya Genital herpes

Genital herpes husababishwa na Virusi vinavyojulikana kama herpes simplex virus, hasa hasa aina ya 2 (HSV-2).

Huu ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa yanayoenezwa kwa kiasi kikubwa, na asilimia kubwa dalili zake huchukua siku 4 mpaka 7 kuanza kuonekana toka siku ya kuambukizwa.

Dalili zake ni pamoja na kuwa na vipele, malengelenge au vidonda vyenye maumivu pamoja na kuhisi hali ya kuungua sehemu za Siri, kuzunguka uke, kwenye matako, na sehemu ya haja kubwa.

10. Ugonjwa wa Kaswende(Syphilis)

Kaswende ni ugonjwa wa zinaa ambao husababishwa na bacteria Treponema pallidum. Ugonjwa huu pia huweza kusababisha vipele kwenye mashavu ya uke au vidonda ambazo hujulikana kama chancre.

11. Tatizo la masundosundo(Genital warts)

Tatizo hili ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa ambapo chanzo chake ni maambukizi ya human papillomavirus (HPV).

Pia tatizo hili huweza kusababisha vipele kwenye mashavu ya uke.

Hizo ndyo baadhi ya Sababu za Mwanamke kupata Tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Mvua kubwa kunyesha nchini,Tahadhari yatolewa na TMAAfyaclass Bongo Social •

Mvua kubwa kunyesha nchini,Tahadhari yatolewa na TMA

TMA imedai kuwa maeneo machache yanatarajiwa kupokea mvua nyingi kwanzia kesho. Kulingana na taarifa tulizozipata, mikoa ya ukanda wa ziwa Victoria na Magharibi inatarajiwa kupokea mvua nyingi na ngurumo za radi wikendi.

Utabiri wa hali ya hewa nchini Tanzania kwa saa 24 zijazo: Mikoa ya Katavi, Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyangu, Mara na Simiyu hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo zinatarajiwa katika maeneo machache na vipindi vya jua wakati wa asubuhi hadi wakati wa mchana.

Vile vile visiwa vya Unguja na Pemba, mkoa ya Daresalaam na Tanga, Mikoa ya pwani, kulingana na habari tulizozipata mvua nyepesi wakati wa jioni na usiku zinatarajiwa. Pia vipindi vya jua vinatarajiwa wakati wa mchana. Wakazi wahimizwa kujiandaa ipasavyo.

Kanda ya ziwa Victoria, mikoa ya Kagera, Geita, Shinyangu, Mwanza, Shinyangu. Vipindi vya mvua vitavyoambatana na ngurumo za radi katika baadhi ya maeneo vinatarajiwa kwanzia kesho.

Nyanda za juu Kaskazini-mashariki, Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro inatarajiwa kupokea kupokea vipindi vya jua wakati wa asubuhi hadi wakati wa mchana. Mvua nyepesi nyepesi ngurumo za radi zinatarajiwa kuendelea maeneo mengi ya ukanda huu.

0 Comment

Uganda yaripoti kifo cha kwanza kinachotokana na Virusi vya Homa ya nyani,MpoxAfyaclass Bongo Social •

Uganda yaripoti kifo cha kwanza kinachotokana na Virusi vya Homa ya nyani,Mpox

Takriban miezi mitatu baada ya maambukizi ya hapo awali kuripotiwa nchini. Maelezo kutoka kwa wizara hiyo yanaonyesha kifo hicho kiliripotiwa Masindi kutoka kwa mtu anayeugua na virusi vya ukimwi.

Kulingana na ripoti iliyonukuliwa kutoka kwa Wizara ya Afya na vyombo vya habari nchini Uganda, Wilaya ya Masindi imesajili maambukizi matatu ya ugonjwa wa Mpox, ambao hutambulika kwa kutoka majipu yaliyojaa usaha usoni, sehemu za siri na sehemu zingine za mwili.

Akizungumza na maofisa wa afya na viongozi wa wilaya wakati wa Misheni ya Kudhibiti Mpango wa Pamoja wa Afya wa Mwaka jijini Kampala siku ya Jumatano, Dkt. Jane Ruth Aceng, Waziri wa Afya, alitoa wito wa kuanzishwa upya kwa vikundi maalum vya kupambana na Mpox, kama vile ilivyokuwa wakati wa Covid-19.

Mlipuko wa Mpox, tunaweza kudhani ni suala rahisi lakini hali halisia ni suala gumu. Mlipuko huu ambao umeathiri dunia nzima unahitaji kudhibitiwa na kukomeshwa.

Nchini Uganda, maambukizi haya yalithibitishwa tarehe 24 Julai, 2024,” alisema.

“Mlipuko unaendelea kuenea. Hadi sasa, tuna jumla ya maambukizi 153, kati ya hizo 42 zilikuwa katika wiki moja iliyopita. Katika siku chache zilizopita, idadi ya maambukizi inaongezeka kwa kasi,” aliongeza.

Dkt. Aceng alifichua kuwa wilaya 19 zimeripoti maambukizi. Ilioathirika zaidi ni Kampala yenye maambukizi 55, ikifuatiwa na Nakasongola, jumuiya ya wavuvi, ambayo ina maambukizi 35, na Wakiso yenye maambukizi 23.

0 Comment

Nini hutokea kwenye Ubongo Mtu anapokaribia kufa?Afyaclass Bongo Social •

Nini hutokea kwenye Ubongo Mtu anapokaribia kufa?

Mwaka 2023, watafiti walichapisha utafiti uliochunguza wagonjwa wanne ambao walikuwa katika usingizi mzito (coma) wakiwa katika mashine.

"Walikuwa wakifa kutokana na magonjwa mbalimbali," anasema mwanasayansi wa mishipa ya fahamu (neva), na Profesa wa Chuo Kikuu cha Michigan, Jimo Borjigin.

Madaktari na familia walipofikia makubaliano kwamba hawakuwa na jambo lolote la matibabu ambalo wangeweza kufanya, waliamua kuziondoa mashine. Kwa ruhusa kutoka jamaa zao, mitambo ya upumuaji iliondolewa.

Watafiti waligundua katika wagonjwa wawili, shughuli za ubongo zinazohusishwa na kazi za utambuzi zilionekana. Mawimbi ya gamma, katika ubongo yaligunduliwa, ambayo yanahusika katika uchakataji wa taarifa na kumbukumbu.

Kwa wanadamu, ni sehemu fulani tu za ubongo zinazoamshwa unapokaribia kufa. Haya ni maeneo yanayohusiana na kazi za fahamu za ubongo.

Mojawapo ni sehemu ya nyuma ya ubongo inayowajibika kwa utambuzi wa hisia, pia ndoto na maono ya kuona.

Eneo jingine ambalo waliona limeamshwa ni eneo linaloitwa Wernicke, linalohusishwa na lugha, kuzungumza na kusikiliza. Liko karibu na masikio yetu, sehemu hiyo ni muhimu sana si tu kwa kuhifadhi kumbukumbu, lakini kwa kazi nyingine za utambuzi.

Profesa anasema eneo la upande wa kulia la ubongo huhusika na hisia za huruma.

"Wagonjwa wengi ambao wamenusurika kifo kutokana na mshituko wa moyo ama walikaribia kufa, wanasema walipata hisia kubwa za huruma."

Karibu na kifo

Katika historia, watu wengi ambao wamekaribia kufa wamezungumza juu ya kuweza kukumbuka nyakati muhimu za maisha yao; wengi wameona mwanga mkali; wengine hujihisi wameiacha miili yao, wakiinuka na kuona kile kilichokuwa kikiendelea karibu nao.

Utafiti wa 2023 unabainisha kuwa katika kundi la watu waliopata mshtuko wa moyo, 20% au 25% waliripoti kuona mwanga, ikimaanisha ubongo uliamsha eneo la kuona.

"Baadhi ya wagonjwa walionusurika kifo wameripoti kusikia kilichokuwa kikiendelea wakati wa upasuaji wao au kile ambacho wahudumu wa afya waliowaokoa walichokuwa wakikisema."

Inawezekanaje mtu anaweza kuona mwanga, kusikia sauti, kuhisi mwili umeondoka na kuelea hewani? "Hayo yote ni sehemu ya kazi ya ubongo," anasema Profesa.

"Kwa sababu wataalamu wa matibabu wanafikiri ubongo haufanyi kazi wakati mtu anapokaribia kufa, kuna wale wanaoamini shughuli hizi zote hutokea nje ya mwili, yaani ni kitu kisicho cha kawaida."

"2013 tulipochapisha utafiti wa kwanza wa wanyama, tuliandika, wazo kwamba hali hiyo hutokea nje ya mwili haliwezi kuthibitishwa."

''Tangu awali, naamini matukio hayo hutokea kwenye ubongo, ingawa ni matukio ya kushangaza kwa sababu inadhaniwa kuwa ubongo haufanyi kazi wakati unapopata mshtuko wa moyo."

"Ninaamini kwamba matukio ya karibu kufa huja kutokana na shughuli za ubongo ambazo hutokea kabla ya ubongo kukoma kufanya kazi kabisa," anasema Borjigin.

Uelewa wa zamani

Borjigin anakubali kwamba utafiti wake kwa wanadamu ni mdogo sana na utafiti zaidi unahitajika juu ya kile kinachotokea katika ubongo tunapokufa.

"Ubongo, badala ya kuwa na shughuli kidogo, huwa na shughuli nyingi wakati wa mshtuko wa moyo. Tunahitaji kuboresha uelewa wetu kuhusu kazi ya ubongo wakati wa shida kama hiyo."

Anafikiri ongezeko la shughuli za ubongo ni sehemu ya mbinu ya ubongo kuishi wakati unapokosa oksijeni .

"Wanyama, panya na wanadamu, wana utaratibu wa asili wa kukabiliana na ukosefu wa oksijeni."

"Uelewa wetu wa sasa ni kwamba, moyo unaposimama, ubongo hufa tu, tunaamini ubongo hauwezi kukabiliana na kusimama kwa moyo."

Lakini anasema – hatujui ikiwa hilo ni kweli.

0 Comment

Wagonjwa zaidi ya 23,000 wamepatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Njombe Afyaclass Bongo Social •

Wagonjwa zaidi ya 23,000 wamepatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Njombe 

Wagonjwa zaidi ya 23,000 wamepatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Njombe huku wagonjwa wa dharura na mahututi wakiwa 1,322 katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufani mkoa wa Njombe Dk. Gilbert Kwesi katika uzinduzi wa huduma ya uchunguzi wa magonjwa ya mfumo wa chakula (ENDOSCOPY UNIT) uliofanyika katika hospitali hiyo.

Dk. Kwesi amesema magonjwa hayo ya mfumo wa chakula mchanganyiko yamekuwa yakiongoza kwa kuwa na idadi ya wagonjwa wengi ambapo kwa kipindi cha Januari hadi Septemba wagonjwa 566 wamefanyiwa uchunguzi na kutibiwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua huduma hiyo amewataka watumishi wa hospitali kuendelea kutoa huduma bora sambamba na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

“Fanyeni kazi kwa kuzingatia maadili lakini tembeeni kifua mbele kwa sababu serikali inaendelea kuhakikisha mnafanya kazi katika mazingira rafiki na kuridhisha pamoja na kutatua matatizo yenu ya kimaslahi,” amesema Mtaka.

Katibu Tawala Mkoa wa Njombe,Judica Omary ametoa rai kwa watoa huduma hao kuongeza ufanisi ili maboresho ya vifaa tiba yaweze kuleta tija.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Kissa Kasongwa ametoa wito kwa wakazi wa Njombe kuiamini hospitali ya rufaa ya mkoa huo kutokana na uwapo wa vifaa tiba vya kibingwa vya teknolojia ya kisasa na huduma zake zikiwa ni bora.

Kuzinduliwa kwa huduma ya tiba kwa wenye matatizo katika mfumo wa chakula kunaifanya hospitali ya rufaa Mkoa wa Njombe kuwa na huduma zote muhimu ambazo awali wakazi wa mkoa huo walilazimika kuzifuata katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

0 Comment

Kuchelewa kwa Hatua za Ukuaji kwa Mtoto: Sababu, Dalili, na Namna ya KushughulikiaAfyaclass Bongo Social •

Kuchelewa kwa Hatua za Ukuaji kwa Mtoto: Sababu, Dalili, na Namna ya Kushughulikia

Ukuaji wa mtoto ni mchakato muhimu unaojumuisha hatua mbalimbali za kimwili, kiakili, kijamii, na kihisia. Watoto wengi hufuata hatua hizi za ukuaji kwa muda unaotarajiwa, lakini kwa baadhi yao, kuchelewa kwa hatua za ukuaji kunaweza kutokea. Kuchelewa huku kunahusisha mtoto kutofikia hatua muhimu kama vile kutembea, kuongea, au kujifunza ujuzi fulani kwa wakati unaotarajiwa.


Dalili za Kuchelewa kwa Hatua za Ukuaji

Watoto wanapokosa kufikia hatua fulani kwa umri unaotarajiwa, inaweza kuwa ishara ya kuchelewa kwa hatua za ukuaji. Dalili hizi zinaweza kuonekana katika maeneo mbalimbali ya ukuaji:

1. Ukuaji wa Kifiziolojia: Watoto wanachelewa kukaa, kutambaa, kusimama, au kutembea. Kwa mfano, mtoto ambaye hafanyi majaribio ya kutembea akiwa na miezi 18 anaweza kuhitaji uchunguzi zaidi.

2. Ukuaji wa Lugha na Mawasiliano: Kuchelewa kuanza kuzungumza ni dalili ya kawaida. Mtoto anayeshindwa kusema maneno yoyote akiwa na umri wa miezi 12 au zaidi anaweza kuhitaji msaada wa kitaalamu. Watoto wanaweza pia kuwa na changamoto za kuelewa lugha au kujieleza.

3. Ukuaji wa Kijamii na Kihisia: Watoto wanaweza kushindwa kuonyesha tabia za kawaida za kijamii kama kuonyesha hisia kwa watu, kucheka, au kuonyesha urafiki na watoto wengine kwa umri unaofaa.

4. Ukuaji wa Kiakili: Watoto wengine wanaweza kushindwa kujifunza mambo mapya kwa kasi inayotarajiwa. Hii inaweza kuonekana kwa kuchelewa kujifunza ujuzi wa kimsingi kama vile kufahamu rangi, maumbo, au kuunda sentensi.

Sababu za Kuchelewa kwa Hatua za Ukuaji

Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia kuchelewa kwa hatua za ukuaji kwa mtoto. Sababu hizi zinaweza kuwa za kibaiolojia, kijamii, au kimazingira:

1. Sababu za Kiafya: Magonjwa ya kuzaliwa kama;

  • Cerebral Palsy
  • ulemavu wa akili,
  •  au shida ya kijenetiki kama Down Syndrome yanaweza kusababisha kuchelewa kwa ukuaji wa mtoto.

2. Lishe Duni: Utapiamlo au ukosefu wa virutubisho muhimu unaweza kuathiri ukuaji wa kimwili na kiakili wa mtoto. Watoto wanaokosa virutubisho kama vile vitamini na madini muhimu wanaweza kukabiliwa na changamoto katika ukuaji wao.

3. Matatizo ya Kiafya ya Wakati wa Kuzaliwa: Watoto wanaozaliwa njiti (premature) au waliozaliwa na uzito mdogo wana uwezekano mkubwa wa kupata changamoto za ukuaji baadaye.

4. Sababu za Mazingira: Kukosa malezi ya upendo, kuwa kwenye mazingira yenye msongo wa mawazo, au familia isiyotoa msukumo wa kimaendeleo ya mtoto inaweza pia kuathiri ukuaji wa mtoto.

Namna ya Kushughulikia Kuchelewa kwa Hatua za Ukuaji

Kuchelewa kwa hatua za ukuaji hakumaanishi kuwa mtoto hawezi kufikia malengo yake ya maendeleo. Hatua za mapema za kusaidia mtoto zinaweza kusaidia kuboresha hali hiyo.

1. Tafuta Ushauri wa Kitaalamu: Wazazi wanapaswa kumpeleka mtoto kwa daktari au mtaalamu wa afya ili kufanya tathmini ya kina. Mtaalamu ataangalia historia ya ukuaji wa mtoto, kufanya vipimo vya kimwili, na kuangalia mwenendo wa kijamii na kihisia wa mtoto.

2. Tiba Maalum: Watoto wanaopata matatizo ya ukuaji wa kimwili wanaweza kufaidika na tiba ya viungo (physical therapy), wakati wale wenye changamoto za lugha wanaweza kusaidiwa na mtaalamu wa mawasiliano (speech therapy). Hata hivyo, kila mtoto anahitaji mpango wa matibabu unaolingana na hali yake ya kipekee.

3. Mazingira Yanayosaidia Ukuaji: Wazazi na walezi wanapaswa kuhakikisha kuwa mtoto yuko kwenye mazingira yanayosaidia ukuaji. Kuwapa watoto muda wa kucheza, kuzungumza nao mara kwa mara, na kuwasoma vitabu kunasaidia sana kukuza lugha na uwezo wao wa kufikiri.

4. Lishe Bora: Watoto wanahitaji lishe bora iliyo na vitamini na madini muhimu ili kusaidia ukuaji wa mwili na akili. Ni muhimu kuhakikisha mtoto anapata chakula chenye virutubisho vyote muhimu kwa ukuaji wake.

Hitimisho:

Kuchelewa kwa hatua za ukuaji kwa mtoto si jambo la kutia hofu kubwa mara moja, lakini ni muhimu kuchukua hatua mapema ili kumsaidia mtoto kufikia hatua muhimu za ukuaji. Kwa ufuatiliaji mzuri na msaada wa kitaalamu, watoto wengi wanaweza kushinda changamoto hizi na kuendelea kukuza uwezo wao wa kimwili, kiakili, na kijamii. Wazazi wanahitaji kuwa na umakini, uvumilivu, na msaada wa kitaalamu ili kusaidia ukuaji wa mtoto wao kwa njia bora zaidi.

0 Comment

Wapandikizwa Ini baada ya kula Uyoga wenye sumuAfyaclass Bongo Social •

Wapandikizwa Ini baada ya kula Uyoga wenye sumu

Mwanamume mmoja nchini Ujerumani na watoto wawili wamelazimika kupandikizwa ini katika Hospitali ya Chuo Kikuu katika mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Essen, baada ya kula uyoga wenye sumu.

Mgonjwa wa nne, ambaye ni mvulana mdogo wa miaka mitano, alipata nafuu bila kupandikizwa ini, imesema hospitali hiyo. Wote wanne, mmoja wao akiwa ni baba wa mmoja wa watoto hao, wamekuwa katika uangalizi wa wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo tangu siku ya Jumanne.

"Hali za wagonjwa wote zinaendelea vizuri na wanafuatiliwa kwa karibu na kwa umakini," ilisema taarifa iliyotolewa na hospitali hiyo.

Wagonjwa hao walilazwa hospitalini wakiwa na hali mbaya. Wawili walifanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali na mtoto mmoja alifanyiwa baadaye.

Uyoga huo aina ya Amanita huliwa, lakini pia una vimelea vya sumu.

Katika kisa tofauti huko mjini Münster, mgonjwa mmoja mwanamke ameendelea kupatiwa matibabu ya kina baada ya kula uyoga wenye sumu wiki iliyopita. Inaaminika kuwa mgonjwa huyo alikula uyoga wa aina hiyo ya Amanita.

Msemaji katika hospitali anakotibiwa mgonjwa huyo alisema siku ya Jumatatu kwamba mgonjwa huyo bado ana hali mbaya na anapatiwa huduma ya wagonjwa mahututi. Aidha pia bado wanatafuta mtu anayeweza kuchangia ini ili waweze kumfanyia upandikizaji.

Bado haijafahamika ikiwa wagonjwa hao walichuma uyoga mwituni au walikula ni wapi walipoula uyoga huo.

0 Comment

Tatizo la hormone imbalance,chanzo,Dalili na Tiba Afyaclass Bongo Social •

Tatizo la hormone imbalance,chanzo,Dalili na Tiba 

Tatizo la hormone Imbalance huweza kusababisha dalili nyingi sana kwenye mwili wa Mtu, Bahati nzuri ni kwamba Hali nyingi zinazosababisha Tatizo la hormone Imbalance zinaweza kutibiwa.

Tatizo la hormone Imbalance ni tatizo ambalo huhusisha uwiano usio sawa wa Vichocheo mwilini.

KUMBUKA;Hormones ndiyo Vichocheo;Hivo basi, katika Makala hii utasikia Zaidi haya maneno, kila tunapotumia neno hormones ujue tunamaanisha vichocheo vya mwili na kila tutakapotumia neno vichocheo ujue tunamaanisha hormones.

Hormones ni nini na zinatoka wapi?

Kwa jina lingine Hormones hujulikana kama chemical Messager kemikali hizi zenye nguvu husafiri kuzunguka damu yako, zikitoa taarifa kwa tishu na viungo nini cha kufanya.  

Hormones husaidia kudhibiti michakato mingi Mikuu ya mwili wako, ikiwa ni pamoja na Shughuli Zote za kimetaboliki pamoja na Uzazi yaani metabolism and reproduction.

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba Hormones au Vichocheo vya mwili huzalishwa na tezi zinazojulikana kama endocrine glands, hivo mfumo mzima unaodhibiti vichocheo hivi hujulikana kama Endocrine System.

Tezi zinazounda endocrine system ni pamoja na:

Katika Tezi zote hizi,Vipo vichocheo vya aina mbali mbali ambavyo kila Tezi huzalisha mwilini,

Tatizo la hormone Imbalance hutokea pale ambapo una kiwango kikubwa au kidogo sana cha homoni fulani.  Hata mabadiliko madogo tu yanaweza kuwa na athari mbaya katika mwili wako wote. 

Viwango vingine vya homoni hubadilika katika maisha yako yote na huenda ikawa tu matokeo ya Uzee ambapo ni kawaida kwa binadamu yeyote.  Lakini mabadiliko mengine hutokea wakati tezi zako za endocrine zinapopata kichocheo kibaya.

Dalili Za Tatizo la hormone Imbalance

Homoni zako zina jukumu muhimu katika afya yako kwa ujumla.  Kama matokeo, kuna ishara na dalili ambazo zinaweza kuashiria kuwa hakuna usawa wa homoni mwilini mwako au una tatizo la Hormone Imbalance.  Ishara au dalili zako zitategemea ni homoni zipi hazipo sawa au ni tezi zipi hazifanyi kazi ipasavyo. 

Kwa kiasi kikubwa Hali za homoni zinazoathiri watu wa jinsia zote zinaweza kusababisha mojawapo ya ishara au dalili zifuatazo:

  1. Uzito kuongezeka kwa kasi au wakati mwingine Uzito kupungua kwa ghafla
  2. Mwili kuchoka kupita kiasi
  3. Misuli ya mwili kuwa dhaifu
  4. Misuli kuuma,kukakamaa n.k
  5. Kupata Maumivu ya Joints,kukakamaa au kuvimba
  6. Kuongezeka au kupungua kwa Mapigo ya Moyo(Heart rate)
  7. Kuvuja jasho kupita kiasi
  8. Kuhisi baridi sana au kuhisi joto sana wakati hali ya mazingira ni tofauti
  9. Kukojoa mara kwa mara
  10. Kuongezeka kwa kiu ya Maji
  11. Kuhisi njaa kila wakati
  12. Kuhisi hali ya Hofu,huzuni,woga,Wasiwasi,Kuwa na Msongo wa mawazo n.k
  13. Kuona marue rue
  14. Hamu ya tendo la ndoa kupungua au kuisha kabsa
  15. Kuongezeka sana kwa nywele mwilini au kupungua sana kwa nywele mwilini
  16. Ngozi kukauka sana(dry skin)
  17. Uso kuwa na mafuta Zaidi,Chunusi n.k

KUMBUKA; Dalili hizi huingiliana kwa kiasi kikubwa na matatizo mengine ya kiafya tunasema ni nonspecific symptoms, hivo kuwa na moja ya dalili hizi haimaanishi una tatizo la hormone Imbalance pekee, Inaweza kuwa ni tatizo lingine la kiafya.

Baadhi ya dalili hizi zinaweza pia kuonyesha hali Zingine Sugu(chronic conditions).  Kwa hivyo, ikiwa unapata dalili hizi, kushughulika na mabadiliko yoyote muhimu katika mwili wako au viwango vya hormones ni wazo nzuri kuzungumza na Wataalam wa afya kwanza.


Dalili za Tatizo la Hormone Imbalance kwa Wanawake

Kwa Watu wenye ovari, matokeo ya kawaida ya tatizo la hormone imbalance ni kuwa na hali ambayo hujulikana kama polycystic ovary syndrome (PCOS).

Hata hivo,Mwanamke pia hupokea mabadiliko ya Vichocheo mwilini kwenye Vipindi kama vile;

  • Kipindi cha balehe
  • Kipindi cha Ujauzito
  • Kipindi cha Unyonyeshaji
  • Pamoja na Kipindi cha Ukomo wa hedhi(menopause)

Baadhi ya Dalili za Tatizo la hormone Imbalance kwa Wanawake ni pamoja na:

1. Kuvurugika kwa Mzunguko wa hedhi,hali ambayo hupelekea Mwanamke;

  • Kukosa kabsa siku zake
  • Kukaa muda mrefu bila kuona hedhi au hedhi kuchelewa Zaidi
  • Hedhi kutoka kidogo sana
  • Hedhi kutoka mara kwa mara
  • Kuvuja damu nyingi wakati wa hedhi
  • Kutokuwa na Tarehe maalum ya kuona siku za hedhi n.k

2. Nywele kuota kupita kiasi kwenye maeneo mbali mbali ya Mwili ikiwemo; Usoni, kwenye kidevu au Sehemu zingine za mwili

3. Mwanamke kuwa na Chunusi Usoni,Kifuani au Sehemu ya Juu ya Mgongo

4. Nywele za mwili kupotea au unapata tatizo la hair loss

5. Uke kuwa Mkavu sana,Tatizo la vaginal dryness

6. Kupata maumivu wakati wa tendo

7. Mwanamke kuvuja sana jasho usiku

8. Kupata Maumivu ya kichwa mara kwa mara

9. Chuchu kutoa Maziwa zenyewe wakati sio mjamzito wala hunyonyeshi

10. Kushindwa kubeba Ujauzito n.k


Dalili za Tatizo la Hormone Imbalance kwa Wanaume

Hapa tutazungumzia zaidi kichocheo cha kiume ambacho hujulikana kama Testosterone. Ikiwa Mwanaume huzalishi testosterone ya kutosha, hali hii inaweza kusababisha dalili mbalimbali ikiwemo;

1. Mwanaume kuota Matiti kama Mwanamke,Tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama gynecomastia,

Kwa kiasi kikubwa,Tatizo hili la Mwanaume kuota matiti huhusisha kuongezeka kwa tishu ndani ya tezi za matiti ya Mwanaume, Pamoja na Uwiano usio sawa wa vichocheo vya estrogen pamoja na testosterone,hii ndyo sababu kubwa ya tatizo hili.

2. Mwanaume kupata Maumivu kwenye Matiti

3. Kuwa na Upungufu wa nguvu za kiume au Uume kushindwa kusimama vizuri ambapo kwa kitaalam hujulikana kama erectile dysfunction

4. Mwanaume kupungua kwa ukuaji wa ndevu na ukuaji wa nywele za mwili

5. Misuli kupungua na kukosa nguvu,loss of muscle mass

6. Mifupa kuwa dhaifu,kuvunjika kwa haraka 

7. Mwanaume kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k

Zipo dalili nyingi, hizi ni baadhi tu ya dalili hizo...!!!


Chanzo cha Tatizo la Hormone Imbalance

Zipo Sababu nyingi ambazo huchangia tatizo hili na baadhi ya Sababu hizo ni pamoja na;

1. Matumizi ya vitu vyovyote ambavyo huweza kuongeza au kupunguza baadhi ya vichocheo vya mwili ikiwemo;

- Dawa mbali mbali

- Baadhi ya Njia za Uzazi wa Mpango

- Matibabu ya Saratani kama vile chemotherapy

2. Kuwa na Uvimbe au tumors hasa kwenye maeneo ya tezi kama vile pituitary tumors n.k

3. Kuumia ambako hugusa na kuathiri mfumo wa vichocheo mwilini(endocrine system)

4. Matatizo yanayotokana na Ulaji yaani eating disorders

5. Msongo wa mawazo au stress

6. Lakini pia zipo baadhi ya hali Zingine ambazo huongeza hatari ya kupata tatizo hili kama vile;

  • Kuwa na kisukari aina zote mbili(type 1 and type 2 diabetes)
  • Kuwa na tatizo la Tezi la Thyroid kutokufanya kazi vizuri hali ambayo hujulikana kama hypothyroidism, or underactive thyroid
  • Tezi hili kufanya kazi kupita kiasi,hyperthyroidism, or overactive thyroid n.k

7. Pia hali ya kuwa na kiwango kikubwa cha cortisol n.k

Kumbuka; Nilitaja hali zingine ambazo huhusishwa na mabadiliko haya ya Vichocheo mwilini hasa kwa Mwanamke, hali hizo ni pamoja na;

>Mwanamke kufikia Ukomo wa hedhi(menopause)

>Ujauzito

>Unyonyeshaji

>Tatizo la PCOS

>Matumizi ya baadhi ya dawa, hormone medications kama vile vidonge vya Uzazi wa mpango- birth control pills n.k

Je,Unasumbuliwa na Tatizo hili na hujapata Tiba bado?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Pembe amefariki dunia,Msanii wa vichekesho wa kitamboAfyaclass Bongo Social •

Pembe amefariki dunia,Msanii wa vichekesho wa kitambo

Mwigizaji na Mchekeshaji Mkongwe Nchini Tanzania, Mzee Yusuph Kaimu maarufu Pembe amefariki dunia jioni ya leo October 20,2024 katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa mtu wake wa karibu, Pembe amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.

Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Dar, Francisco Mwinuka almaarufu Pierre, amethibitisha na kueleza kuwa kwa sasa anaelekea Hospitali ya Temeke na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

0 Comment

Maambukizi ya Marburg yapungua nchini RwandaAfyaclass Bongo Social •

Maambukizi ya Marburg yapungua nchini Rwanda

MAAMBUKIZI ya virusi vya ugonjwa wa Marburg nchini Rwanda yamepungua baada ya watu waliokuwa hatarini kuanza kupatiwa chanjo.

Waziri wa afya nchini Rwanda Sabin Nsanzimana amesema tangu serikali kwa kushirikiana na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC kutoa chanjo maambukizi ya ugonjwa huo yamepungua katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

#SOMA ZAIDI HAPA🔗🔥; Kuhusu Ugonjwa wa Marburg,chanzo,dalili

Hatahivyo,Mkuu wa Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC Jean Kaseya amesema licha ya kupungua kwa maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Marburg kwa sasa wanakabiliana na tatizo la Mpox ambalo limeshafika katika nchi sita Barani Afrika.

0 Comment

Chumvi hutibu nini mwilini mwako?,Fahamu hapaAfyaclass Bongo Social •

Chumvi hutibu nini mwilini mwako?,Fahamu hapa

Chumvi ina matumizi kadhaa katika mwili wa binadamu, lakini inapaswa kutumiwa kwa kiasi kwani matumizi yake kupita kiasi yanaweza kuwa na madhara. Hii hapa ni baadhi ya faida na jinsi chumvi inavyosaidia mwilini:

1. Kudhibiti usawa wa maji: Chumvi ina sodiamu, ambayo husaidia kudhibiti usawa wa maji mwilini. Sodiamu husaidia kuhifadhi maji katika mwili na kudhibiti viwango vya maji kwenye seli.

2. Kusaidia kazi ya neva na misuli: Sodiamu katika chumvi ni muhimu kwa mawasiliano kati ya seli za neva na misuli. Hii inasaidia katika kufikisha ujumbe kati ya ubongo na sehemu nyingine za mwili, kuruhusu misuli kujikunja na kulegea.

3. Kudhibiti shinikizo la damu: Chumvi, kwa kiwango sahihi, husaidia kudhibiti shinikizo la damu kwa kusaidia kudhibiti kiasi cha maji kwenye damu na mishipa ya damu. Hata hivyo, chumvi nyingi inaweza kusababisha shinikizo la damu kupanda (hypertension).

4. Kuhifadhi electrolytes mwilini: Chumvi ni chanzo muhimu cha electrolytes, ambazo ni muhimu kwa shughuli nyingi mwilini kama vile kudumisha usawa wa pH na kusaidia moyo kufanya kazi vizuri.

5. Kusaidia usagaji chakula: Chumvi ina uwezo wa kusaidia kuzalisha asidi ya tumbo ambayo ni muhimu katika usagaji wa chakula na kunyonya virutubisho.

Pamoja na faida hizi, ni muhimu kutumia chumvi kwa kiasi, kwani matumizi ya chumvi nyingi yanaweza kusababisha matatizo kama vile shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, na shida za figo. Shirika la Afya Duniani (WHO) linapendekeza matumizi ya chini ya gramu 5 za chumvi kwa siku kwa watu wazima.

Chumvi hufanya chakula chetu kiwe na ladha. Pia ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu. Sodiamu katika chumvi ni muhimu katika kudumisha kiwango sahihi cha maji katika mwili. Pia husaidia seli kunyonya virutubisho.

“Chumvi ni muhimu katika maisha,” anaeleza Paul Breslin, profesa wa sayansi ya lishe katika Chuo Kikuu cha Rutgers nchini Marekani.

"Chumvi ni muhimu sana kwa seli zote, ikijumuisha nyuroni zetu zote, ubongo, mgongo na misuli yetu yote. Pia ni muhimu kwa ngozi na mifupa.”

Na Profesa Breslin anaonya, ikiwa hatuna sodiamu ya kutosha tutakufa.

Upungufu wa sodiamu mwilini husababisha kuchanganyikiwa, hasira, misuli kutofanya kazi vizuri, kutapika, hali ya koma n.k.

Shirika la Afya Ulimwenguni linapendekeza ulaji wa chumvi wa gramu tano kila siku, yenye gramu mbili za sodiamu.

Lakini wastani wa ulaji wa chumvi kimataifa ni karibu gramu 11 kwa siku. Hilo huongeza hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa, saratani ya tumbo, unene, maradhi ya mifupa na ugonjwa wa figo.

WHO inakadiria watu milioni 1.89 hufa kila mwaka kutokana na matumizi ya chumvi kupita kiasi.

Wanaoongoza kutumia chumvi

Katika nchi nyingi, utumiaji wa chumvi kupita kiasi hutokana na kiasi kilichofichwa katika vyakula vilivyochakatwa.

Watu wa Kazakhstan hutumia karibu gramu 17 za chumvi kwa siku, zaidi ya mara tatu ya kiasi kilichopendekezwa.

Maryam anaishi Astana, mji mkuu wa Kazakhstan. Anasema, “ni kutokana na urithi wetu. Kwa karne nyingi tulizunguka misituni, tukiwa na nyama ambazo zilipaswa kuhifadhiwa kwa kutumia chumvi."

"Familia zilihifadhi nyama kwa msimu wa baridi. Wanaweza kuhifadhi ng'ombe mzima, kondoo na hata nusu farasi."

Miaka minane iliyopita, binti wa Maryam alikuwa na matatizo ya kiafya. Daktari wake alimshauri apunguze vyakula vyenye sukari nyingi, mafuta na chumvi nyingi. Familia iliacha mara moja kuongeza chumvi kwenye chakula chao. Na hatimaye Familia ya Mariyam ilizoea maisha bila kuongezwa chumvi.

Chumvi mwilini

Tunapokula chumvi, ladha yake hugunduliwa kwenye ulimi wetu na kaakaa laini la koo.

“Chumvi hutia nguvu mwili na akili zetu,” anasema Profesa Breslin.

Sodiamu huyeyuka kwenye mate. Kisha huingia kwenye seli za ladha na kuamsha seli moja kwa moja.

“Chumvi hupeleka mawimbi ya umeme ambayo huamsha mawazo na hisia. Kwa hivyo mwili na akili zetu huchangamka.”

Athari katika mwili

Athari ya chumvi kwenye mwili inategemea muundo wa vinasaba wa mtu. Zaidi ya watu bilioni moja duniani kote wanakabiliwa na shinikizo la damu. Kupunguza ulaji wa chumvi kunaweza kusaidia kuzuia hilo na kutibu.

"Unapokuwa na chumvi nyingi, jambo la kwanza ambalo mwili wako hufanya ni kuiyeyusha. Kwa hivyo shinikizo la damu hupanda ili kusukuma maji ya ziada,” anaeleza Claire Collins, Profesa wa Lishe na milo katika Chuo Kikuu cha Newcastle nchini Australia.

"Ikiwa una udhaifu wowote katika mishipa yako ya damu, kama ile ya ubongo, inaweza kupasuka na kusababisha kiharusi."

Nchini Uingereza, wastani wa matumizi ya chumvi umepungua hadi gramu nane kwa siku, ambayo bado ni zaidi ya viwango vilivyopendekezwa. Upunguzaji huo unatokana na kanuni walizowekewa watengenezaji wa chakula kupunguza viwango vya chumvi.

Ulaji wa chumvi unaopendekezwa hutofautiana kutoka nchi hadi nchi. Kipimo cha mkojo kinaweza kugundua ikiwa mwili wako una chumvi nyingi au kidogo.

Namna ya kupunguza chumvi

Hata kama kiwango chako cha chumvi ni cha juu, kupunguza kunaweza kuwa sio rahisi sana. Lakini Prof Collins anatuhimiza tule mkate au pasta au chakula kingine chochote ambacho kina kiwango cha chini cha chumvi.

"Ikiwa unapika chakula chako mwenyewe weka mitishamba na viungo badala ya chumvi."


0 Comment

Jinsi ya Kupunguza Uzito kwa Watu Walemavu wenye KisukariAfyaclass Bongo Social •

Jinsi ya Kupunguza Uzito kwa Watu Walemavu wenye Kisukari

Wagonjwa wa kisukari wanaokabiliwa na matatizo ya ulemavu na wanatakiwa kupunguza uzito, wanahitaji mpango maalumu wa kupungua uzito wa mwili kama walivyoshauriwa.

Kupunguza uzito ni muhimu kwa kudhibiti viwango vya sukari na kupunguza hatari ya matatizo mengine yanayohusiana na kisukari.

Hata hivyo, njia zinazotumika lazima ziwe salama na zinazowezekana kwa hali yao, pasipo kusababisha sukari kushuka mara kwa mara.

Kuwa na mpango lishe bora kwa maana ya kuchagua vyakula vyenye afya. Vyakula vya wanga kama vyenye nyuzinyuzi nyingi ambavyo ni matunda, mboga, nafaka kamili kama vile shayiri, uwele, mtama, mahindi na ngano ambayo haijakobolewa.

Ulaji wa vyakula vya wanga hautakiwi uwe wa kiasi kikubwa, kipimo ni sawa na ngumi moja ya mgonjwa wa kisukari, ni vyema kwa kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu na kusaidia katika udhibiti wa uzito.

Protini kama samaki, kuku, maziwa, maharage na mayai hutoa protini bila kuongeza mafuta yasiyohitajika. Protini husaidia katika kudhibiti hisia za njaa na inaweza kusaidia katika kudumisha misuli.

Vyakula vilivyopikwa kwa mafuta ya mimea kama yale ya olive, parachichi, ubuyu na alizeti. Haya mafuta ni mazuri zaidi kwa wenye kisukari kwa sababu hayana lehemu, lakini pia hayatakiwi kutumika kwa kiasi kikubwa kwenye chakula.

Mboga za majani zina umuhimu mkubwa katika kupunguza uzito na kudhibiti viwango vya sukari kwa sababu ya faida zake nyingi.

Mboga za majani zina kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi, ambazo ni muhimu kwa kudhibiti uzito na viwango vya sukari.

 MADHARA YA KITAMBI KWA WANAUME

Bila shaka umewahi kusikia baadhi ya watu wakisema "kuwa na kitambi sio afya ni Ugonjwa" Kauli hii ina maana kwamba kuwa mnene pamoja na kuwa na vitambi kuna madhara mengi mwilini hivo watu wajitahidi kudhibiti vitambi.

Katika makala hii tumechambua baadhi ya athari za kuwa na vitambi kwa upande wa Wanaume,ambao ndyo kwa asilimia kubwa hupatwa na tatizo hili la kuwa na kitambi,tukiwa na maana kwamba madhara ya kitambi huweza kutofautiana kati ya jinsia moja na nyingine,lakini pia kati ya umri na umri.

MADHARA YA KUWA NA KITAMBI KWA WANAUME NI PAMOJA NA;

1. Kuathiri uzalishwaji wa hormone ya kiume ambayo hujulikana kama Testosterone

2. Kuongeza uzalishwaji wa Hormones za kike kwenye mwili wa Mwanaume

3. Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba,kuwa na kitambi kwa mwanaume kunaongeza uwezekano wa mwanaume kupatwa na tatizo la Saratani ya Tezi Dume yaani Prostate Cancer

4. Kuwa na kitambi kwa Mwanaume huweza kuchangia Mwanaume kuwa na Tatizo la Kupungukiwa na Nguvu za kiume

5. Kuwa na kitambi kwa Mwanaume huweza kuchangia Mwanaume kupungukiwa na hamu ya kufanya tendo la Ndoa

6. Kuwa na kitambi kwa Mwanaume huweza kuchangia Mwanaume kuwa na maumbile madogo sana au kuwa na uume mdogo kuliko kawaida

7. Matatizo mengine ambayo huweza kutokea ni pamoja na;

• Kuwa katika hatari ya kupatwa na magonjwa mbali mbali kama vile; magonjwa ya Moyo,Presha,kisukari pamoja na magonjwa ya Figo

• kuwa katika hatari ya kupatwa na tatizo la choo kigumu yaani Constipation mara kwa mara

• Kuwa katika hatari ya kupatwa na tatizo la Bawasiri

• Kupatwa na matatizo ya kuumwa miguu mara kwa mara, maumivu ya joints,kupatwa na tatizo la miguu kuwaka moto mara kwa mara pamoja na miguu kuvimba

• Uchovu kupita kiasi hata kama umefanya kazi ndogo sana N.k

Hivo basi,Kama una kitambi unashauriwa kutumia njia mbali mbali za kupunguza kitambi ulichonacho ili kuepuka athari zake, Fanya mazoezi ya mwili kila siku angalau kwa dakika 30 au Nusu saa,epuka kula vyakula vya mafuta mengi pamoja na kutumia njia nyingine za kitaalam kwa ajili ya kupunguza uzito na vitambi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Adesi hueneza ugonjwa gani,Soma Hapa kufahamuAfyaclass Bongo Social •

Adesi hueneza ugonjwa gani,Soma Hapa kufahamu

Mbu aina ya aedes aegypti hueneza ugonjwa wa zika, bila kusahau dengue na chikungunya

UGONJWA WA ZIKA,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE

Ugonjwa wa Zika ni ugonjwa ambao husababishwa na Virusi na kusambazwa na mbu aina ya Aedes mosquitoes ambao kwa asilimia kubwa humuuma mtu wakati wa asubuh sana,mchana au jioni,

Mbu huyu aina ya Aedes mosquitoes ndyo huyo huyo ambaye huweza kusambaza ugonjwa wa DENGUE,CHIKUNGUNYA,Pamoja na YELLOW FEVER.

Japo pia watu wengi wenye maambukizi ya virusi wa Zika hawaonyeshi dalili zozote,

DALILI ZA UGONJWA WA ZIKA NI PAMOJA NA;

- Joto la mwili kuwa juu sana au mtu kuwa na homa

- Mtu kupata rashes kwenye ngozi ya mwili wake

- Mtu kupata tatizo la macho kuvimba kwenye conjactiva hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Conjuctivitis

- Mtu Kupata shida ya maumivu kwenye misuli pamoja na maumivu ya joint

- Mtu kupata maumivu ya kichwa cha mara kwa mara

- Mtu kupata uchovu wa mwili kupita kiasi n.k

VIPIMO VYA UGONJWA WA ZIKA NI PAMOJA NA

• Mtu kuchunguzwa dalili za ugonjwa kwa kuulizwa maswali,kuangaliwa na kuchukua histori ya ugonjwa kutoka kwa mgonjwa mwenyewe

• Pamoja na vipimo vya maabara yaani laboratory tests vinavyohusu kuchukua Sample ya Damu,mkojo,jasho,mate au maji maji ya aina yoyote kutoka kwenye mwili wa mgonjwa,

hii ndyo comfirmatory test,vipimo hivi ndyo hutoa uthibitisho kamili kama mgonjwa ana ugonjwa wa zika au hana

MADHARA YA UGONJWA WA ZIKA NI PAMOJA NA

- Mashambulizi ya virus wa zika huweza kumpata mama mjamzito kisha kuleta madhara mbali mbali kama vile;

• Mtoto kuzaliwa na kichwa kidogo kuliko kawaida yaani Microcephaly pamoja na matatizo mengine ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Congenital Zika Syndrome

• Pia huweza kuleta madhara wakati wa ujauzito kama vile; ujauzito kuharibika wenyewe(miscarriage) au mama kujifungua mtoto kabla ya wakati yaani preterm birth

- Pia ugonjwa wa zika huweza kusababisha matatizo kwenye mfumo wa Nerves(Neurologic disorder) kwa Watu wazima na watoto ikiwemo tatizo la; Neuropathy pamoja na myelitis

MATIBABU YA UGONJWA WA ZIKA

✓ Kama ilivyo kwa magonjwa mengi ambayo chanzo chake ni virusi, Hakuna matibabu ya moja kwa moja ya kutibu kabsa au kuondoa kabsa kirusi hiki,

ila kuna matibabu yanayohusu kudhibiti dalili mbali mbali ambazo husababishwa na kirusi hiki kwenye mwili wako, kama vile homa,maumivu ya misuli,joints n.k

Pia kwa wale watu ambao wapo kwenye ukanda ambao kuna Mbu sana wanashauriwa kujikinga na mbu kwa kutumia Net wakati wa usku, pamoja na kuvaa nguo ndefu wakati wa mchana,kutoacha vichaka,au madimbwi ya maji karibu na makazi ya watu pamoja na njia nyingine za kujikinga na Mbu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 DENGUE:

UGONJWA WA DENGUE(chanzo,dalili na tiba yake)

Ugonjwa wa Dengue ni ugonjwa ambao chanzo chake ni virusi ,ugonjwa huu huweza kusambazwa na mbu ambao wamebeba vimelea  hivi.

CHANZO CHA UGONJWA WA DENGUE

Hivo basi kama nilivyokwisha kusema hapo juu ugonjwa wa dengue chanzo chake ni virusi lakini msambazaji mkuu ni mbu jamii ya Aedes aegypti na wakati mwingine hata jamii ya Aedes albopictus huhusika pia.

DALILI ZA UGONJWA WA DENGUE NI PAMOJA NA;

- Joto la mwili la mgonjwa kupanda au mgonjwa kuwa na homa

- Kupata uchovu wa mwili kupita kiasi

- Kupata maumivu makali ya kichwa

- Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya chakula

- Maumivu ya viungo,misuli pamoja na joint kwenye mwili

- Maumivu ya tumbo,kiuno na mgongo

Maeneo ya joto sana, pamoja na hali ya unyevu unyevu huweza kuwa mazingira mazuri sana ya ugonjwa huu

MATIBABU YA UGONJWA WA DENGUE

Homa ya dengue huweza kutibika kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa aina mbali mbali, 

Ushauri wangu kwako ni bora kwenda hospital kufanya vipimo kwanza, kabla ya kuanza matibabu 

Kwa Ushauri zaidi,Elimu, Au Tiba tuwasiliane kwa Namba +255758286584

Karibu Sana..!!

0 Comment

Breaking; Lori la Mafuta Laua Watu Zaidi ya 90Afyaclass Bongo Social •

Breaking; Lori la Mafuta Laua Watu Zaidi ya 90

Zaidi ya Watu 90 Wafariki Dunia Wakijaribu Kuchota Mafuta kwenye Ajali ya Lori

Jeshi la Polisi Nchini Nigeria Limesema Zaidi ya watu 90 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kulipuka kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Msemaji wa Polisi Katika Jimbo la jigawa DSP Lawan Shiisu Adam alisema mlipuko huo ulitokea kwenye barabara kuu ya Taura, huku makumi ya watu wakikimbilia kwenye gari kuchukua mafuta kwenye Lori hilo.

Wakazi walikuwa wakichota mafuta katika lori lililopinduka wakati mlipuko ulipotokea, na kusababisha moto mkubwa ulioua watu 94 papo hapo,” alisema

0 Comment

Maambukizi Ya Malaria Yapungua Hadi Asilimia 8.1 Kwa Mwaka 2015-2022Afyaclass Bongo Social •

Maambukizi Ya Malaria Yapungua Hadi Asilimia 8.1 Kwa Mwaka 2015-2022

Wizara ya afya kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti malaria kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI imepunguza kiwango cha malaria kwa asilimia 45 kutoka 14.8 ya mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 8.1 mwaka 2022.

Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge na Masuala ya Ukimwi kilichofanyika katika ukumbi wa bunge Jijini Dodoma.

Dkt. Mollel amesema kuwa, Serikali imetekeleza mikakati ya udhibiti wa mbu waenezao Malaria kwa njia ya utengamano pamoja na ugunduzi, matibabu na tiba kinga dhidi ya malaria ambapo imewezesha mafanikio hayo kwa takribani miaka 8 na kupunguza wagonjwa wa malaria wanaotibiwa kama wagonjwa wa nje (OPD) kwa asilimia 55.

“Serikali imetekeleza afua mbali mbali kwa takriban miaka minane na kufanikiwa kupunguza kiwango cha malaria kwa asilimia 45 kutoka 14.8 hadi 8.1 pamoja na kupunguza wagonjwa wa nje kwa asilimia 55 ambapo awali walikua ni milioni 7.7 hadi 3.5 kwa mwaka 2023”. Amesema Dkt. Mollel

Aidha, Dkt. Mollel amesema kuwa kwa sasa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria unatekeleza mpango mkakati wa sita wa mwaka 2021 mpaka 2025 wenye lengo la kupunguza kiwango cha chini kutoka asilimia 7.5 (2017) hadi 3.5 ifikapo 2025

Kwa Upande wake Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Bi Bernadeta Mushashu ameishauri serikali kuongeza afua za kutokomeza malaria katika mikoa iliyo katika hatari  ya maambukiza ya malaria kama vile Tabora unaoongoza  kwa asilimia 23.4, Mtwara kwa asilimia 20, Kagera asilimia 18, Shinyanga 16%na Mara 15%.

Aidha ameipongeza Serikali kwa juhudi na malengo ya kuendelea kutekeleza afua za kutokomeza malaria pamoja na kufanikiwa kupunguza mpaka chini ya asilimia katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Dodoma, Singida, Iringa, Songwe, Dar es Salaam na Mwanza.

Hata hivyo wametoa rai kwa wananchi kuendelea kutekeleza ushauri wa madaktari kuhusu matumizi sahihi ya vyandarua pamoja na kuweka mazingira yanayotuzunguka safi na salama  ili kuzuia mazalia ya viluilui ya mbu.

0 Comment

Watu milioni 730 wanakabiliwa na njaa duniani kote-FAOAfyaclass Bongo Social •

Huu ni Ujumbe wa FAO kwa dunia, Siku ya chakula duniani

Jana ilikuwa ni siku ya chakula duniani,Tarehe 16 October, ambako huko Roma, Italia makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, kumefanyika tukio maalum la kuadhimisha siku hiyo, washiriki wakisisitiza umuhimu wa kila mtu duniani kupata chakula bora, cha kutosha, salama na kwa bei nafuu.

Watu wana uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na uhaba wa chakula na utapiamlo ikiwa hawawezi kumudu lishe bora.

Maadhimisho yamefanyika wakati kukiwa na mivutano na mizozo duniani, sambamba na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, mambo ambayo yanachochea mamilioni ya watu duniani kote kukumbwa na njaa huku mabilioni wengine wakiwa hawana uwezo wa kupata lishe bora.

Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa FAO

Akifungua maadhimisho hayo, Mkurugenzi mkuu wa FAO, QU Dongyu amesema maudhui ya siku hii mwaka huu ambayo ni Haki ya Chakula Kwa Maisha Bora na Mustakabali Bora, yamekuja wakati muhimu kukumbusha kwamba watu wote wana haki ya kupata chakula cha kutosha.

“Natoa wito kwa ahadi mpya ya kujenga mifumo ya kilimo cha mazao ya chakula iliyo fanisi, jumuishi, yenye mnepo na endelevu zaidi itakayowezesha kulisha vema dunia.”

Qyu amesema mifumo ya aina hiyo inatakiwa kusaidia wakulima wadogo, wakulima wa kaya na wafanyabiashara wadogo kwenye mnyororo wa thamani ambao katika nchi nyingi ndio msingi wa kuwezesha kuzalisha vyakula tofauti tofauti vyenye lishe na kuwezesha vipatikane na viwafikie watu, na wakati huo huo wakihifadhi tamaduni za asili za vyakula.

Watu milioni 730 wakikabiliwa na njaa duniani kote na wengine zaidi ya bilioni 2.8 wanashindwa kupata lishe bora, “hatuna wakati wa kupoteza, na lazima tuchukue hatua,” amesema Mkurugenzi Mkuu huyo wa FAO

0 Comment

kucha kuingia kwenye nyama,kucha kuota kwenye nyamaAfyaclass Bongo Social •

kucha kuingia kwenye nyama,kucha kuota kwenye nyama

Tatizo la Kucha Kuingia ndani ya nyama za vidole(Ingrown Toenails)

Wakati mwingine, upande wa kucha (kawaida kwenye kidole kikubwa) hukua ndani ya ngozi na inaweza kutokea katika umri wowote ikiwemo kwa wazee.

Kidole chako kinaweza kuvimba, kuumizwa, na kuambukizwa baada ya tatizo hili kutokea. Mtu mwenye tatizo la Miguu kuvuja sana jasho, uzito kupita kiasi, na kisukari yupo kwenye hatari zaidi ya kupatwa na tatizo hili.

Ili kuzuia, epuka kukata kucha zako kuwa fupi sana kuliko kawaida, kuna baadhi ya watu hukata kucha na kuwa fupi zaidi mpaka wanapata maumivu.

Epuka kuvaa viatu vya kubana, n.k Soma zaidi hapa…

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA KUCHA KUINGIA NDANI YA NYAMA ZA KIDOLE.

Ingrown toenails ni tatizo ambalo hutokea mara baada ya chembe ya sehemu ya kucha kutoboa na kuingia kwenye ngozi na hivyo kupelekea athari na maambukizi katika kidole. Kidole gumba cha mguu ndio huathirika zaidi na tatizo hili la kucha kuingia ndani ya nyama ya Kidole.

DALILI ZA TATIZO HILI LA KUCHA KUINGIA NDANI YA NYAMA ZA KIDOLE NI PAMOJA NA;

1. Mtu kupata Maumivu makali kwenye kucha pamoja na kidole

2. Kidole kilichoathirika na shida hii kuvimba

3. Kutoa maji maji kidoleni

4. Tishu zenye rangi nyekundu kuota eneo hilo

VIHATARISHI ZA KUTOKEA KWA NA TATIZO LA KUCHA KUINGIA NDANI YA NYAMA ZA KIDOLE NI PAMOJA;

1. Mtu Kuvaa viatu vinavyobana sana mara kwa mara

2. Mtu Kukata sanaa sehemu ya pembeni ya kucha

3. Matatizo mengine ya ukucha

4. Mtu kupata Ajali zinazohusisha miguu

Mojawapo ya njia ya kuzuia tatizo hili la kucha kuota na kuingia ndani ya nyama ya kidole ni pamoja na kukata kucha vizuri na kutokuvaa viatu vya kubana sana.

Matibabu yake hutegemeana na hatua au ukubwa wa tatizo, Ila mojawapo ya Tiba ni kukata na kuondoa kucha hii.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Kitandani kuna mamilioni ya bakteria, fangasi, wadudu na virusiAfyaclass Bongo Social •

Kitandani kuna mamilioni ya bakteria, fangasi, wadudu na virusi

Fahamu kwamba kitanda chako kinaweza kuwa na mamilioni ya bakteria, fangasi, wadudu na virusi. Ingawa Kila mmoja wetu anadhani kitanda chake ni mahali pazuri sana pa kukaa, ndyo ni Sahihi lakini je unajua pia unaweza kupata vimelea wengi wa magonjwa kitandani?

 Kitandani kuna joto ambalo linaweza kutengeneza mazingira mazuri kwa Vimelea wa magonjwa kukua, pamejaa jasho, mate, chembechembe za ngozi zilizokufa na ndio chakula kwa ajili ya vimelea hao.

Mfano, vijidudu vidogo sana vinavyoishi kwenye vumbi. Tunamwaga seli za ngozi milioni 500 kwa siku, vijidudu hivyo hula seli hizo. Kwa bahati mbaya, vidudu hivyo na mabaki yake (kinyesi) vinaweza kusababisha mzio, pumu pamoja na tatizo la ukurutu.

Mashuka ya kitanda ni kimbilio la bakteria pia. Mwaka 2013, watafiti katika Taasisi ya Pasteur de Lille huko Ufaransa walichunguza mashuka ya kitanda cha hospitali na kugundua yamejaa bakteria wa Staphylococcus, ambao hupatikana zaidi kwenye ngozi ya binadamu.

Ingawa spishi nyingi za staphylococcus hazina madhara, lakini baadhi, kama vile S. aureus, wanaweza kusababisha maambukizi ya ngozi, chunusi na hata nimonia kwa wagonjwa walio na kinga dhaifu.

"Watu hubeba bakteria wengi katika ngozi zao," anasema Manal Mohammed, mwanabiolojia wa Chuo Kikuu cha Westminster nchini Uingereza.

"Ingawa bakteria hawa kwa kawaida hawana madhara, ila wanaweza kusababisha ugonjwa mbaya ikiwa wataingia mwilini kupitia majeraha ya wazi, ambayo ni ya kawaida hospitalini," anasema Manal.

Vitanda vya hospitali

Mwaka 2018, wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Ibadan nchini Nigeria walipata bakteria wa E. koli katika mashuka ya kitanda cha hospitali ambayo hayajafuliwa, pamoja na bakteria wengine wa pathogenic wanaojulikana kusababisha maambukizi ya njia ya mkojo, nimonia, kuhara, homa ya uti wa mgongo na sumu katika damu.

Mwaka 2022, watafiti walikusanya sampuli kutoka kwenye vyumba vya wagonjwa waliolazwa hospitalini kwa ugonjwa wa mpox. Waligundua kuwa kitendo cha kubadilisha shuka la kitanda hutoa chembe za virusi kwenye hewa.

Mwaka 2018, mfanyakazi wa afya wa Uingereza inaaminika alipata ugonjwa huo baada ya kuambukizwa virusi wakati akibadilisha mashuka ya kitanda cha mgonjwa.

"Mashuka ya hospitalini huoshwa kwenye maji makali ya moto, ambayo huua bakteria wengi," anasema David Denning, profesa wa magonjwa ya kuambukiza katika Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza.

Isipokuwa bakteria wa C. difficile, ambaye husababisha kuhara, hasa kwa watu wazee. Kuosha kunaweza kuharibu nusu ya bakteria C. difficile, lakini seli za bakteria hao ni vigumu kufa. Hata hivyo, viwango vya maambukizi ya C. difficile vimepungua nchini Uingereza.

Bila shaka, kuna uwezekano mkubwa wa kupata bakteria wa pathogenic katika kitanda cha hospitali ambapo mgonjwa amelala kuliko katika kitanda cha mtu mwenye afya.

Vitanda vya Nyumbani

Mwaka 2013, kampuni ya vitanda ya Marekani ya Amerisleep ilichukua sampuli kutoka katika foronya ambayo haikuwa imeoshwa kwa wiki moja. IIikuwa na takribani bakteria milioni tatu kwa kila nchi ya mraba - takribani mara 17,000 zaidi ya bakteria waliopo kwenye sinki la choo.

Mwaka 2006, Denning na wenzake walikusanya mito sita kutoka kwa marafiki na familia. Mito hiyo ilikuwa ikitumika mara kwa mara na ilikuwa na umri wa kati ya miezi 18 na miaka 20. Mito yote ilikuwa na fangasi, hasa aina ya Aspergillus fumigatus - ambao hupatikana kwa wingi kwenye udongo.

"Unazungumza mabilioni au matrilioni ya chembe za fangasi kwenye kila mto," anasema Denning.

"Chanzo cha kupatikana fangasi wengi ni kwa sababu wengi wetu tunatokwa na jasho usiku. Pia sote tuna wadudu wa vumbi vitandani mwetu, na kinyesi cha wadudu hao hutoa chakula kwa fangasi. Na kisha jioni mto hupata joto kwa sababu kichwa chako hulala hapo, kwa hivyo kuna unyevu, kuna chakula, na kuna joto.”

Kwa kuwa wengi wetu huwa hatuoshi mito yetu, fangasi huishi katika hali ya utulivu na wanaweza kuishi kwa miaka. Hata kama utaosha foronya, fangasi wanaweza kuishi katika halijoto ya hadi nyuzi joto 50C (122F), na kwa vyovyote vile kuosha mito au foronya kunaweza kuifanya iwe na unyevu zaidi, na hivyo kuruhusu kukua zaidi.

0 Comment

Mtanzania wa Kwanza Agundulika na Maambukizi ya Homa ya Nyani (Mpox)Afyaclass Bongo Social •

Mtanzania wa Kwanza Agundulika na Maambukizi ya Homa ya Nyani (Mpox)

WIZARA ya Afya imethibitisha kisa cha kwanza cha Mtanzania, kubainika amepata maambukizi ya homa ya nyani (Mpox). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Aidha, imesema Tanzania iko salama na hakuna mgonjwa wa Mpox aliyebainika hapa nchini hadi sasa.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Roida Andusamile, amesema Mtanzania huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 32, alibainika kuwa na ugonjwa huo akiwa nchini Zambia.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa umma leo tarehe 11 Oktoba 2024, amesema taarifa ya kisa hicho waliipata jana kutoka mamlaka za serikali ya Zambia.

“Mtanzania huyu alivuka mpaka kutoka Tanzania kwenda Zambia mnamo tarehe 02 Septemba, 2024 kupitia mpaka wa Tunduma (Tanzania) na Nakonde (Zambia), akiwa hana dalili zozote za ugonjwa wa Mpox,” amesema Roida.

Amesema mwezi mmoja baadaye yaani tarehe 02 Oktoba 2024, akiwa nchini humo, alikwenda katika kliniki mojawapo ambapo alipata matibabu ya awali na kuchukuliwa vipimo tarehe 04 Oktoba 2024, ambavyo vilithibitisha kuwa na maambukizi hayo.

“Tarehe 08 Oktoba 2024, vipimo vya maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii ya Zambia vilithibitisha kuwa ni ugonjwa wa Mpox. Mgonjwa huyu bado anapata matibabu nchini Zambia…dalili za ugonjwa wa Mpox huweza kuonekana kati ya siku 3 hadi 21 tangu kuambukizwa. Hivyo, kwa kuwa Mtanzania huyu alianza kuonesha dalili mwezi mmoja baada ya kutoka nchini, ni dhahiri kuwa hakutoka nchini akiwa na maambukizi,” amefafanua.

Ameipongeza serikali ya Zambia kwa kubaini ugonjwa huo mapema, kumhudumia mgonjwa na kutoa taarifa kwa wakati.

Amesema Tanzania inaendelea kushirikiana na Zambia kufuatilia hali ya mgonjwa na kuhakikisha anapona na kurejea nchini, akiwa na afya njema.

“Wizara inapenda kuwahakikishia kuwa, bado Tanzania iko salama na hakuna mgonjwa wa Mpox aliyebainika hapa nchini hadi sasa. Wizara inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu na itaendelea kutoa taarifa kwa umma.

“Wizara inatoa wito kwa jamii kuendelea kuzingatia kanuni za usafi, kutopeana mikono na kutoa taarifa kwa kutumia namba 199 ili kwa pamoja tuhakikishe ugonjwa huu hauingii nchini,” amesema Roida.

0 Comment

Tatizo la busha,chanzo,dalili na TibaAfyaclass Bongo Social •

Tatizo la busha,chanzo,dalili na Tiba

Busha ni tatizo ambalo huhusisha kuvimba kwa eneo la korodani au uvimbe ndani ya vifuko vya korodani(Scrotum) unaosababishwa na kujaa maji.

Tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama hydrocele

Tatizo la busha au hydrocele ni aina ya uvimbe kwenye korodani, au mfuko wa ngozi unaoshikilia korodani. Uvimbe huu hutokea wakati majimaji yanapojikusanya kwenye kifuko chembamba kinachozunguka korodani. Hydroceles ni kawaida pia kwa watoto wachanga”

Dalili za Tatizo la Busha

Mara nyingi ishara pekee ya busha ni uvimbe usio na uchungu au maumivu kwenye korodani moja au zote mbili.

Uvimbe huo unaweza kufanya korodani ya mtu mzima kuhisi nzito. Kwa ujumla, maumivu yanaongezeka wakati uvimbe unaongezeka. Wakati mwingine, eneo lenye kuvimba linaweza kuwa dogo asubuhi na kubwa baadaye mchana.

Vitu hivi huongeza hatari ya Kupata tatizo la busha

Busha nyingi zipo wakati wa kuzaliwa. Tafiti zinaonyesha Angalau asilimia 5% ya wanaume waliozaliwa wana busha,

Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, ambao huzaliwa zaidi ya wiki tatu kabla ya tarehe zao za kuzaliwa, wana hatari kubwa ya kuwa na busha pia.

Sababu za hatari za kupata Tatizo la busha baadaye maishani ni pamoja na:

  • Kupata Jeraha au kuvimba ndani ya korodani.
  • Maambukizi, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya zinaa.n.k

Madhara ya Tatizo la busha ni yapi?

Mara nyingi si tatizo lenye hatari kubwa au madhara zaidi ni la kawaida, Na pia haliathiri uwezo wa kupata mtoto kama baadhi ya watu wanavyosema.

Ingawa pia busha linaweza kuhusishwa na shida za kiafya ambazo zinaweza kusababisha madhara makubwa. Kuna uhusiano wa hydrocele na Matatizo haya:

• Maambukizi au tumor.

Na matokeo yake inaweza kusababisha korodani kutengeneza kiwango kidogo cha manii au zisifanye kazi vizuri kama kawaida.

• Hernia ya inguinal.

Hii inaweza kusababisha matatizo ya kiafya ambayo huweza kutishia maisha.

Chanzo cha tatizo la busha

Tatizo la hydrocele au Busha ni tatizo la kujaa kwa maji kwenye mfuko wa korodani za mwanaume.

SABABU AU CHANZO CHA TATIZO LA BUSHA NI NINI?

Tatizo la Busha au hydrocele huweza kusababishwa na vitu mbali mbali ikiwemo;

– hali ya eneo la Kuzunguka Korodani kuwa na Maji mengi kuliko ilivyokawaida,

– Mirija ya Lymph kwenye Korodani au mishipa ya Damu inayosafirisha damu kutoka kwenye korodani kwenda maeneo mengine ikiwa Imeziba kabsa,

Vyote hivi hupelekea kupungua kwa ufyonzwaji wa maji yanayozunguka eneo la korodani. Hali ambayo hupelekea maji kujikusanya kwenye vifuko vya Korodani.

HIZI NI BAADHI YA SABABU ZA MAJI KUWA MENGI KWENYE ENEO LA KORODANI

• Mtu kupata Majeraha au kuumia kwenye Korodani(Injury)

• Mtu kupata Maambukizi ya magonjwa kwenye eneo la Korodani

• Mtu kupata Maambukizi kwenye mshipa wa-epididymis

• Mtu kupata Maambukizi yanayo sababishwa na vimelea wa filaria (filariasis) wanao sababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.

• Mtu kupata tatizo la Korodani Kujisokota ambapo kwa kitaalam hujulikana kama testicular torsion

• Mtu kupata Uvimbe kwenye korodani yaani testicular tumors,

Hii pia huweza kuchangia uzalishwaji wa maji mengi kwenye korodani.

• Mtu Kufanyiwa upasuaji ambao huweza kuathiri ufyozwaji wa maji kwenye korodani

• Mtu kupata Tiba ya mionzi kipindi cha nyuma. n.k

KUMBUKA; Watu ambao wapo maeneo ya Pwani, wapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la Busha,

Hui ni kutokana na kuwa kwenye hatari zaidi ya kung’atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD