Vatican yatangaza Tarehe Rasmi ya kuanza mchakato wa kumpata Papa mpyaAfyaclass Bongo Social •

Vatican yatangaza Tarehe Rasmi ya kuanza mchakato wa kumpata Papa mpya



Ofisi ya Habari ya Vatican imetangaza kuwa kikao cha #Conclave cha kumchagua Papa mpya kitaanza rasmi tarehe 7 Mei.

Maamuzi haya yalifikiwa na Makardinali walioko Roma siku ya Jumatatu, wakati wa mkutano wao wa tano wa Maandalizi (#GeneralCongregation).

Conclave hiyo itafanyika ndani ya Kanisa la Sistine lililopo Vatican, ambalo litafungwa katika kipindi hicho maalum.

Wakati huu, dunia nzima inaelekeza macho Vatican, ikisubiri kwa hamu jina la kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki!

0 Comment

Ugonjwa wa nimonia kwa watoto husababishwa na nini?Afyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa nimonia kwa watoto husababishwa na nini?



Dalili za nimonia kwa mtoto, Fahamu hapa

Nimonia(Pneumonia) ni maambukizi ya mapafu ambayo husababishwa na virusi au bakteria, Vijidudu hivi hufanya vifuko vya hewa kwenye mapafu kujazwa na majimaji (kohozi au ute). Hii inafanya kuwa vigumu kupumua na kusababisha mtoto wako kukohoa.

Fahamu: Nimonia huua watoto zaidi kuliko ugonjwa mwingine wowote wa kuambukiza.

Ingawa hata watu wazima huweza kupata ugonjwa wa nimonia, ugonjwa huu hushambulia na kuua Watoto Zaidi ulimwenguni kote.

Kila mwaka, Nimonia inaondoa maisha ya zaidi ya watoto 725,000 walio chini ya umri wa miaka 5, ikiwa ni pamoja na karibu watoto wachanga 190,000, ambao wako katika hatari ya kuambukizwa.

Kila siku, angalau Mtoto mmoja hufa kutokana na ugonjwa wa Nimonia kwa kila sekunde 43, na Karibu Vifo vyote vinaweza kuzuilika.

Ni jambo lisilo na udhuru kwamba maelfu ya watoto hawawezi kupata huduma muhimu za afya na matibabu, ambayo yanaweza kuzuia nimonia na kuokoa maisha yao.

Chanzo cha ugonjwa wa Nimonia(pneumona)?

Nimonia ni maambukizi ya mfumo wa kupumua ambayo huathiri mapafu. Maambukizi haya hayana sababu moja – yanaweza kutokana na maambukizi ya vimelea kama vile;

  • bakteria,
  • virusi
  • au fungi

Wakati mtoto ameambukizwa, mapafu yake yanajaa maji na inakuwa vigumu kupumua. Watoto ambao kinga zao hazijakomaa (yaani watoto wachanga) au dhaifu – kama vile wenye utapiamlo, au magonjwa kama VVU – wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa ugonjwa wa nimonia.



Dalili za nimonia kwa mtoto

Fahamu hapa kuhusu dalili za ugonjwa wa pneumonia;

Kwa vile nimonia ni maambukizi ya mapafu, dalili za kawaida ni;

  • kukohoa,
  • kupumua kwa shida
  • na homa.
  • Watoto walio na nimonia kwa kawaida hupumua haraka, au kifua chao kinaweza kuvuta au kujirudisha nyuma wakati wa kuvuta pumzi (kwa mtu mwenye afya njema, kifua hupanuka wakati wa kuvuta pumzi).

– Kupumua haraka na kwa shida

– Kupata homa

– mwili kutetemeka sana

– Kupata maumivu ya misuli ya mwili

– Kukosa hamu ya kula chakula au kunyonya

– Kukohoa

– Kupata maumivu ya kifua

– Kupata Uchovu sana wa mwili

– Mwili kuwa Dhaifu sana

– Kupata kichefuchefu na kutapika n.k

Nimonia inayosababishwa na virusi mara nyingi sio kali kuliko inayosababishwa na bakteria. Dalili kwa kawaida huanza kama mafua. Na zinazidi kuwa mbaya zaidi kwa siku chache.

Nimonia inayosababishwa na bakteria inaweza kuja ghafla na homa kali, kupumua haraka na kukohoa.

Aina zote mbili za pneumonia zinaweza kusababisha kikohozi kwa mtoto kwa wiki kadhaa baada ya homa kukoma.

Nimonia inasambaa Je?

Nimonia inaambukiza na inaweza kuenea kupitia chembechembe zinazopeperuka hewani  kupitia (kikohozi au kupiga chafya). Inaweza pia kusambazwa kupitia vimiminika vingine, kama vile damu wakati wa kujifungua, au kutoka kwenye sehemu zilizochafuliwa.

Jinsi gani Nimonia hugundulika kwa mtoto?

Njia ambazo ugonjwa wa Nimonia huweza kugundulika kwa mtoto ni pamoja na;

  •  physical exam, ikiwa ni pamoja na kuangalia mifumo isiyo ya kawaida ya kupumua na kusikiliza mapafu ya mtoto.
  • chest x-rays
  • Au vipimo vya damu(blood tests)

Matibabu ya Ugonjwa wa Nimonia)pneumonia)

Matibabu ya nimonia inategemea na aina ya nimonia. Katika nchi zinazoendelea, idadi kubwa ya matukio ya nimonia husababishwa na bakteria na inaweza kutibiwa na antibiotics za gharama nafuu.

Hata hivyo watoto wengi wenye nimonia hawapati dawa za kuua vijasumu wanazohitaji kwa sababu wanakosa huduma bora za afya. Sababu nyingine za nimonia ni virusi au mycobacteria (k.m. zile zinazosababisha kifua kikuu) zinazohitaji matibabu mengine. Kifua kikuu haswa mara nyingi hubaki bila kutambuliwa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Peter Nwachukwu, mume wa mwimbaji maarufu wa injili Osinachi, ahukumiwa kifo kwa kunyongwa Afyaclass Bongo Social •

Peter Nwachukwu, mume wa mwimbaji maarufu wa injili Osinachi, ahukumiwa kifo kwa kunyongwa 



NIGERIA: Mahakama Kuu huko Abuja amemhukumu Peter Nwachukwu, mume wa mwimbaji maarufu wa injili Osinachi, kifo kwa kunyongwa kwa kupatikana na hatia ya mauaji.

Hukumu hiyo, iliyotolewa na Jaji Nwosu-iheme, inatolewa miaka mitatu baada ya kifo cha Osinachi kilichotokea mnamo Aprili 8, 2022.

Kesi hiyo imevutia Watu wengi kwa sababu ya umaarufu wa Osinachi katika muziki wa injili wa Nigeria na jamii ya Wakristo.

Polisi walikuwa wamemkamata Bwana Nwachukwu baada ya mkewe, kufariki akiwa katika hospitali moja huko Abuja.

Ripoti za awali zilikuwa zimependekeza kwamba mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 42 alikuwa mgonjwa wa saratani ya koo, lakini familia yake ilikataa na kudai kwamba alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani.

Walimshutumu mumewe kwa unyanyasajina kusababisha kifo cha mke wake.

Baadaye mahakama iliamuru kwamba arudishwe kizuizini gerezani. Bwana Peter Nwachukwu alishtumiwa kwa "vitendo vya vurugu na kumshambulia mkewe na ufahamu kuwa kifo hicho kitakuwa ni matokeo ya matendo yake."

Mashahidi 17, pamoja na watoto wawili, waliitwa na upande wa mashtaka wakati wa kesi hiyo. Hati 25 pia zilitolewa kama kithibitisho mbele ya mahakama.

Marehemu Osinachi na mume wake aliyehukumiwa Peter Nwachukwu walijaaliwa watoto wanne.

0 Comment

WHO yatangaza haya dhidi ya Ukeketaji unaofanywa na wahudumu wa afyaAfyaclass Bongo Social •

WHO yatangaza haya dhidi ya Ukeketaji unaofanywa na wahudumu wa afya



Hatua za haraka zinahitajika ili kudhibiti ongezeko la ukeketaji wa wanawake (FGM) unaofanywa na wahudumu wa afya ("medicalized FGM") na kuwahusisha wahudumu wa afya katika kuzuia tendo hilo, kulingana na mwongozo mpya uliotolewa leo Aprili 28 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO).

Ingawa sekta ya afya ina jukumu muhimu katika kusitisha ukeketaji na kuwasaidia waathirika, ushahidi kutoka maeneo mbalimbali duniani unaonesha kuwa tendo hilo sasa linazidi kufanywa na wahudumu wa afya. Kufikia mwaka 2020, inakadiriwa kuwa wasichana na wanawake milioni 52 walikeketwa na wahudumu wa afya — takriban tukio 1 kati ya kila matukio manne.

Mwongozo mpya wa WHO, unaoitwa ‘Kuzuia ukeketaji wa wanawake na usimamizi wa kiafya wa matatizo yanayotokana na tendo hilo’, unatoa mapendekezo ya kuzuia ukeketaji na pia kuhakikisha huduma za afya za kitaalamu kwa waathirika, ukihusisha hatua kwa sekta ya afya, serikali, na jamii zilizoathirika.

Ni hatari

“Ukeketaji wa wanawake ni ukiukwaji mkubwa wa haki za wasichana na unahatarisha sana afya yao,” anasema Dkt. Pascale Allotey, Mkurugenzi wa WHO wa Afya ya Uzazi na Utafiti, na wa Mpango Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Uzazi wa Binadamu (HRP). “Sekta ya afya ina jukumu la msingi katika kuzuia FGM — wahudumu wa afya wanapaswa kuwa mawakala wa mabadiliko, si watekelezaji wa tendo hili hatari, na pia lazima watoe huduma bora kwa waathirika.”

Ukeketaji mara nyingi hufanywa kwa wasichana wadogo kabla ya kubalehe na unajumuisha taratibu zote zinazokatakata au kuharibu sehemu za siri za wanawake kwa sababu zisizo za kiafya. Ushahidi unaonesha kuwa, haijalishi nani anatekeleza FGM, bado husababisha madhara. Utafiti fulani unaonesha kuwa linaweza kuwa hatari zaidi likifanywa na mtaalamu wa afya, kwa kuwa kuna uwezekano wa kukata kwa kina zaidi. Uwekaji wake katika muktadha wa kiafya pia unaweza kuufanya uonekane kama halali, hivyo kuhatarisha juhudi za kuachana na tendo hilo kwa ujumla.

Kuwashirikisha wahudumu

Kwa sababu hizi, mwongozo mpya wa WHO unapendekeza kuwepo kwa kanuni za kitaaluma zinazokataza waziwazi wahudumu wa afya kufanya FGM. Pia, ukizingatia nafasi yao ya heshima katika jamii, unasisitiza umuhimu wa kuwaelimisha na kuwashirikisha kwa njia chanya wahudumu wa afya katika kuzuia ukeketaji. Mbinu nyeti za mawasiliano zinaweza kuwasaidia kukataa kwa ufanisi maombi ya kufanya FGM huku wakiwapa watu taarifa kuhusu madhara yake ya haraka na ya muda mrefu.

“Utafiti unaonesha kuwa wahudumu wa afya wanaweza kuwa viongozi wa maoni wenye ushawishi katika kubadili mtazamo kuhusu FGM, na wana nafasi muhimu katika kuzuia tendo hilo,” anasema Christina Pallitto, Mtafiti katika WHO na HRP aliyesimamia uundaji wa mwongozo huo mpya. “Kuwahusisha madaktari, wauguzi na wakunga kunapaswa kuwa sehemu kuu ya mikakati ya kuzuia na kukabiliana na FGM, huku mataifa yakijitahidi kumaliza tendo hilo na kulinda afya ya wanawake na wasichana.”

Pamoja na sheria madhubuti na sera, mwongozo unaangazia pia umuhimu wa elimu na uhamasishaji wa jamii. Shughuli za uelimishaji jamii zinazowahusisha wanaume na wavulana zinaweza kuwa na ufanisi mkubwa katika kuongeza maarifa kuhusu FGM, kutetea haki za wasichana, na kusaidia mabadiliko ya mitazamo.

Huduma kwa waathirika

Mbali na kuzuia, mwongozo huu pia unatoa mapendekezo ya kimatibabu ili kuhakikisha waathirika wa FGM wanapata huduma ya huruma na bora ya kiafya. Kutokana na madhara ya muda mfupi na mrefu yatokanayo na FGM, waathirika wanaweza kuhitaji huduma mbalimbali za afya katika hatua tofauti za maisha, kuanzia afya ya akili, usimamizi wa hatari za uzazi, hadi upasuaji wa kurekebisha madhara inapobidi.

Ushahidi unaonesha kuwa, kwa kujitolea ipasavyo na msaada wa kutosha, inawezekana kumaliza FGM. Mataifa kama Burkina Faso, Sierra Leone na Ethiopia yameshuhudia upungufu wa maambukizi kwa wasichana wenye umri wa miaka 15–19 kwa asilimia asilimia 50, asilimia 35 na asilimia 30mtawalia katika kipindi cha miaka 30 iliyopita kupitia hatua za pamoja na dhamira ya kisiasa ya kutekeleza marufuku na kuharakisha uzuiaji.

Tangu mwaka 1990, uwezekano wa msichana kukeketwa umepungua kwa mara tatu. Hata hivyo, FGM bado ni jambo la kawaida katika takriban nchi 30 duniani, na inakadiriwa kuwa wasichana milioni 4 bado wapo hatarini kila mwaka.

0 Comment

Chanzo Cha Tatizo La Uke Kujamba Pamoja Na Tiba YakeAfyaclass Bongo Social •

Chanzo Cha Tatizo La Uke Kujamba Pamoja Na Tiba Yake

Baada ya tafiti mbali mbali kufanyika imeonekana baadhi ya sababu mbali mbali huchangia shida ya uke kujamba,hasa wakati wa kufanya mapenzi, na sababu hizo ni kama;

- Kulegea kwa misuli ya uke,hivo kupelekea uke kuwa wazi  mara nyingi na kuruhusu hewa kuingia na kujaa ukeni. Hivo kusababisha uke kujamba.

- Kuosha uke kwa maji ya moto mara kwa mara pia huchangia hali ya uke kujamba kwani huchangia misuli ya uke kulegea na kusababisha uke kuwa wazi na kusababisha hewa kujaa ukeni.

- Kulala hivo hivo mara tu baada ya kufanya mapenzi bila kujisafisha ukeni, hali hii  huathiri joto la ndani ya uke na kupelekea shida mbali mbali kama hii ya uke kujamba.

Soma: Tatizo la Uke Kulegea,chanzo,dalili na Tiba yake

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Tatizo la Uke kutoa hewa au Uke Kujamba ni tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Vaginal flatulence,vaginal flatus, au queef,

Hali hii ni utoaji wa hewa iliyonaswa kutoka kwenye uke.  Kujaa gesi kwenye uke ni jambo la kawaida kwa Wanawake wengi, Na Mara nyingi hutokea wakati wa kufanya Tendo la Ndoa au mazoezi. Kwa kiasi kikubwa, hali hii haina Athari yoyote kwenye afya ya Uzazi.

Dalili za Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa

-Dalili kubwa ya Uke kutoa hewa ni Kujamba Ukeni,mithili ya Mtu ambaye amejamba kwa njia ya haja kubwa,

Hivo mtu mwenye hali hii huweza kusikia Sauti ya Kijambo Ukeni,kama unavyojamba kawaida.

-Tofauti na Kujamba Kwa kawaida,Kujamba Ukeni hakutoi harufu yoyote mbaya kwa Asilimia kubwa, labda kama una tatizo Lingine la Kiafya.

Hizi ni baadhi ya Dalili za Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa.

Sababu Zingine za Uke Kutoa hewa au Uke kujamba

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu hizo pamoja na Vitu ambavyo huongeza hatari ya Mwanamke kutoa hewa Ukeni;

• Aina za Staili ya Kujamiiana au Kuingiza Kitu kwenye Uke, Kitu kinapoingizwa kwenye uke, kinaweza kusababisha hewa kuingia ndani ya Uke.

• Pia Inawezekana gesi kuingia Ukeni wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, wakati daktari anapoingiza au kuondoa kifaa kama speculum.

• Aina ya Mazoezi na jinsi unavyofanya Mazoezi vinaweza kusababisha hewa kunasa ndani ya uke. 

 Wanawake mara nyingi huripoti gesi Ukeni wakati wa shughuli fulani za kimwili, kama vile kufanya mazoezi aina ya yoga. n.k

• Ujauzito au Kukoma kwa Hedhi,

 Baadhi ya wanawake huripoti matukio zaidi ya kujaa gesi ukeni wakati wa ujauzito au kukoma hedhi.

• Baada ya Kujifungua, 

Wanawake wengi pia huripoti shida hii ya kujamba Ukeni au kutoa hewa Ukeni baada ya kujifungua kwa Njia ya Kawaida.

Kuzaa mtoto na hali zingine zinazoweka shinikizo kwenye tishu za fupanyonga zinaweza kusababisha hili.

• Muundo au Anatomia ya Sakafu ya Pelvic,

Sakafu ya fupanyonga ya kila mtu ni ya kipekee kidogo, na kwa baadhi ya Wanawake inaweza kuwa rahisi zaidi kuliko wengine kutoa hewa iliyonaswa.

• Pia mara chache tatizo la kujaa hewa kwenye uke huhusishwa na fistula ya ukeni,

Fistula ni tundu au mwanya usio wa kawaida unaounganisha uke na kiungo kingine, kama vile kibofu cha mkojo, koloni, au rektamu. 

 Ikiwa fistula imeunganishwa na koloni au rectum, inaweza kusababisha mkusanyiko wa kinyesi kutoka kwa njia ya uke.  

Kuzaa, matibabu ya saratani, kuumia, na taratibu fulani za upasuaji zinaweza kusababisha kuundwa kwa fistula. Mwone daktari wako ikiwa kujamba kwako Ukeni au Hewa inayotoka ukeni ina harufu mbaya, au ukigundua inaambatana na kutokwa kwa maji yasiyo ya kawaida Ukeni.

Jinsi ya Kugundua tatizo la Uke kujamba(Diagnosis of Vaginal Flatulence)

Ingawa hakuna vipimo maalum au taratibu za kubainisha chanzo cha hewa kutoka kwa uke, daktari wako anaweza kufanya uchunguzi wa pelvic ili kudhibiti ikiwa kuna tatizo kubwa zaidi.

Hivo unaweza kufanyiwa na aina zingine za Vipimo kulingana na dalili ulizonazo kwa wakati huo.

Matibabu ya Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa

Matibabu yake asilimia 100% hutegemea na chanzo husika, Hivo baada ya kugundua chanzo utapewa Tiba Sahihi.

Zipo dawa pamoja na Vitu vya Kufanya na Kuzingatia ili kukusaidia hali hii kuisha

NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Hakikisha Unapata Msaada mapema ikiwa Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa linaambatana na matatizo Kama haya;

  • Kutoa harufu mbaya Ukeni
  • Kutokwa na Usaha au uchafu mwingine Ukeni
  • Kutokwa na kinyesi Ukeni
  • Unapata maumivu ukeni
  • Unahisi muwasho mkali
  • Unaumia Ukeni,kwenye mashavu ya uke au wakati wa kujamiiana
  • Unapata maambukizi ya mara kwa mara ya UTI au maambukizi Ukeni

Jinsi ya Kuzuia Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa

Mara nyingi hakuna njia za moja kwa moja za kuzuia hali hii Lakini unaweza kuzingatia baadhi ya mambo;Epuka staili za Mapenzi ambazo hujaza hewa nyingi Ukeni n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


0 Comment

Madhara ya kujichua kwa mwanamke,Fahamu hapaAfyaclass Bongo Social •

Madhara ya kujichua kwa mwanamke,Fahamu hapa

Madhara ya Kujichua kwa Mwanamke

Kujichua (masturbation) kwa Mwanamke ni kitendo cha mwanamke kujigusa sehemu zake za siri kwa lengo la kujiletea msisimko wa kimapenzi au kufika kileleni (orgasm). Ingawa kujichua ni tabia inayofanywa na watu wengi duniani, ikiwa kwa wanaume au wanawake, kuna maswali mengi kuhusu usalama wake na madhara yanayoweza kutokea, hasa kwa wanawake.

Katika makala hii, tutaangazia kwa kina madhara yanayoweza kuhusishwa na kujichua kwa mwanamke, tukiegemea tafiti na maelezo ya wataalamu wa afya.

1. Maumivu ya Sehemu za Siri na Maambukizi

Kujichua mara kwa mara au kwa kutumia nguvu kupita kiasi kunaweza kusababisha:

  • Maumivu au kuvimba kwenye uke na kinembe (clitoris).
  • Kuchubuka kwa ngozi ya sehemu za siri, hasa ikiwa vidole au vifaa vinavyotumika si safi au vina ukali.
  • Maambukizi ya bakteria au fangasi (vaginal infections) yanayoweza kusababishwa na kuingiza vitu visivyo safi ukeni au kwa kuathiri microbiome ya uke.

Ukosefu wa usafi wa mikono au vifaa vinavyotumika kujichua unaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) au maambukizi ya ukeni.

2. Kujeruhi Sehemu za Ndani

Wanawake wengine hutumia vitu au vifaa (sex toys) wakati wa kujichua. Ikiwa vifaa hivi si salama, vinaweza:

  • Kusababisha michubuko au majeraha kwenye ukuta wa uke.
  • Kuvuruga mfumo wa ulinzi wa uke, na kusababisha hatari ya maambukizi.
  • Kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa kutokana na majeraha yaliyopo.

Matumizi mabaya ya vifaa visivyo rasmi au vilivyotengenezwa kwa malighafi zisizo salama (kama plastiki isiyo na kiwango cha matibabu) huongeza hatari ya sumu au kuathiri tishu za ukeni.

3. Athari za Kisaikolojia

Ingawa kujichua mara nyingi huhusishwa na kupunguza msongo wa mawazo (stress relief), ikiwa kuna utegemezi mkubwa, madhara ya kisaikolojia yanaweza kujitokeza, kama vile:

  • Kujihisi na hatia (guilt) kutokana na imani za kidini au kijamii.
  • Kujitenga na watu kwa sababu ya kutumia muda mwingi kwenye kujichua badala ya kushirikiana na wenzako.
  • Kupungua kwa motisha ya mahusiano ya kimapenzi (relationship intimacy issues) kwa sababu kujichua kunakuwa mbadala wa mawasiliano ya kimwili.

Tafiti kutoka Journal of Sex Research zinaonyesha kuwa kujichua kupita kiasi kunaweza kuathiri uwezo wa kujihusisha kihisia na wapenzi wa kweli.

4. Uraibu wa Kujichua (Masturbation Addiction)

Fahamu kujichua kupita kiasi (masturbation compulsivity) inaweza kuwa tatizo kubwa kunapoathiri:

  • Majukumu ya kila siku, kama kazi, masomo, au mahusiano.
  • Afya ya akili, kwa kusababisha hisia za wasiwasi (anxiety) au huzuni (depression).
  • Mtazamo wa kujihisi hafifu (low self-esteem) baada ya kila tukio la kujichua.

Uraibu wa kujichua si suala la mara ngapi mtu anajichua, bali ni pale ambapo mtu anashindwa kujidhibiti na anafanya hivyo kwa namna inayomuathiri maisha yake mengine muhimu.

5. Kupungua kwa Msisimko wa Asili (Natural Sexual Response)

Kujichua mara kwa mara hasa kwa kutumia mbinu kali au vifaa maalum kunaweza:

  • Kupunguza uwezo wa kupata msisimko au kufika kileleni kwa njia ya kawaida wakati wa tendo la ndoa.
  • Kuharibu mchakato wa asili wa kusisimka, kwa sababu mwili unazoea aina fulani ya msisimko unaopatikana tu kwa kujichua.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, ikiwa mwanamke huzoea kujichua kwa kutumia shinikizo kali lisilopatikana katika ngono ya kawaida, anaweza kupata changamoto ya kufikia kileleni akiwa na mwenzi wake.


Hitimisho

Kujichua kwa mwanamke ni tabia inayoweza kusababisha madhara makubwa mwilini, ikiwa kusababisha majeraha, uraibu, matatizo ya kihisia au kuathiri mahusiano, Hivo ni muhimu kutafuta msaada kutoka kwa mtaalamu wa afya ya akili au daktari wa masuala ya afya ya uzazi ikiwa upo kwenye changamoto hii au

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILINE KWA NAMBA +255758286584.

Kumbuka: Mwili wa mwanamke ni wa thamani. Ni muhimu kuuheshimu na kuutunza vizuri ili kudumisha afya ya mwili, akili na mahusiano.


Vyanzo vya kuaminika:

  • Healthline.com: "Is Masturbation Healthy?"
  • ClevelandClinic.org: "Female Masturbation: Benefits and Risks"
  • MedicalNewsToday.com: "Compulsive Masturbation: Symptoms and Treatments"
  • Journal of Sex Research.


0 Comment

Nini Faida ya kutumia Gari kali Siku ya Harusi?Afyaclass Bongo Social •

Nini Faida ya kutumia Gari kali Siku ya Harusi?



Bila shaka ushahudhuria vikao vya sherehe mbalimbali iwe sendoff, harusi na nyingine zenye kufanana na hizo, ukaona namna kamati za maandalizi zinavyohaha kuhakikisha maharusi wanatumia magari mazuri siku ya tukio.

Si ajabu ukaona watu wanafikia hata hatua ya kugombana kuhusu gari la maharusi, huyu akisema aina fulani ya gari ndo nzuri lakini gharama kubwa, mwingine akisema tusijali gharama tuichukue tu kama bajeti ipo. 

Sasa kuna mdau anasema ushawahi kujiuliza faida ya kutumia gari kali ni ipi? Yaani usiku mtu anatumia gari kali kwenye harusi anapelekwa ukumbini kisha hotelini, halafu asubuhi anaondoka na Bajaji kuelekea nyumbani kwake, mbwembwe zote zimeisha! Je tumsaidie mdau mawazo au asubiri kwenye shughuli yake aone?

0 Comment

Wananchi wa Tanzania wanapaswa kuchukua tahadhari dhidi ya SarataniAfyaclass Bongo Social •

Wananchi wa Tanzania wanapaswa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa saratani ili waweze kuwa salama, kutokana na idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwawa saratani kuwa kubwa kidunia.



Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Dkt. JenisterMhagama, katika maadhimisho ya Samia SaluhuOustreach ambao wameweka kambi kwaajili yauchunguzi wa Saratani, Iliyofanyika katika hospitali yaPeramiho iliyopo Halmashauri ya Peramiho wilaya yaSongea, Mkoani Ruvuma. Na kuwasisitiza kujinga naUgonjwa huo wa Saratani.

Amesema, “Athari za ugonjwa wa saratani kiduniakama nilivyosema mwanzo zimekuwa zikiongezeka, natakwimu za mwaka 2018 zinaonyesha kuwa kiduniakati ya watu sita wanaokufa, mmoja amekufakwasababu ya saratani.”

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa athari hizo kamakusipokuwa na mpango mahususi wa kuzuia vifo hivimpaka mwaka 2030 vinaweza kuwa vimeongezeka.    

“Tushirikiane wote kuhakikisha kwamba tunapambanakuzuia hivyo vifo lakini ikiwezekana tupambanekuzuia ugonjwa wa saratani katika nchi yetu yatanzania. Ili tuweze kuwa salama tuweke msisitizokwenye kinga, tuzingatie ulaji unaofaa na hasa kwakuongeza kula mbogamboga, matunda ya kutoshambogamboga nyingi, tupunguze kula vyakula vyenyemafuta, tupunguze chumvi nyingi kwenye chakula, tupunguze kula sukari, tuitikie wito wa mh. raisi kwakufanya mazoezi.”

Aidha Mhagama, kupitia maadhimisho hayo yasaratani, aliwaasa wananchi kujikinga na magonjwamengine ya mlipuko ambayo mengi yanatokana namuingiliano kati ya wanyama pamoja na Binadamukutokana na kuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watupamoja na uharibifu wa mazingira. Amesema,

“Dunia hii inakwenda kwa haraka kwa speed, mabadiliko ni makubwa sana, zamani ilikuwa ukisikiamtu anaugua labda ni malaria, ama surua, magonjwa kama ya polio ambayo tumeshakwisha kuitokomezakatika nchi kwetu,” amesema na kuongeza

“Lakini ongezeko la idadi ya watu duniani, ukijumlishana uharibifu wa mazingira, kumeanza kuwa namuingiliano kati ya binadamu na wanyama wa polini, siku hizi wala huoni ajabu nyani wanakuja kukaa mpaka kwenye nyumba za watu, wamehama porini nikwa sababu ya uharibifu wa mazingira, binadamu wamewaingilia wanyama na wanyama wamewaingilia binadamu.

“Matokeo yake ongezeko la magonjwa mapya ya mlipuko yanayoambukizwa limekuwa nikubwa, huu ni upande mmoja wa dunia tunayoishisasa, na ndiyo maana sasa hivi tunawaambia tuna homaya epoxi homa ya nyani, huko nyuma ungeshangaakusikia kuna homa ya nyani, lakini siku hizi kunahoma ya nyani imeingia kwa bindamu. na niendeleekuwaomba wananchi wa mkoa wa ruvuma kuendeleakuchukua tahadhari.” amesema

0 Comment

Sehemu ya haja kubwa kuuma,chanzo na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

Sehemu ya haja kubwa kuuma,chanzo na Tiba yake



MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo cha tatizo la maumivu makali ya njia ya haja kubwa ni Bawasiri,ila sio kila mtu mwenye maumivu makali sehemu ya njia ya haja kubwa basi ana Bawasiri.

Baada ya kuliona hilo na kukutana na maswali mengi juu ya tatizo hili la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la bawasiri,nmeona nitoe maelekezo kwa kina kuhusu baadhi ya sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kupatwa na tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa ambayo huweza kutokea wakati anajisaidia au hata akiwa amekaa tu.

Sababu au Chanzo cha Maumivu makali sehemu ya Haja Kubwa

BAADHI YA SABABU ZA TATIZO LA MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA NI PAMOJA NA;

1. Tatizo la Bawasiri,kutoka kinyama sehemu ya haja kubwa,kuvimba kwa mishipa ya vein kwenye njia ya haja kubwa, hapa kuna bawasiri ya ndani pamoja na bawasiri ya nje,zote hizi huweza kusababisha maumivu makali ya sehemu ya haja kubwa

2. Mtu Kuwa na tatizo la jipu au majipu ambayo yametokea kwenye njia ya haja kubwa

3. Uwepo wa tatizo la Saratani au Kansa ya sehemu ya haja kubwa kama vile;Anal cancer,Rectum cancer n.k

4. Mtu kupatwa na tatizo la Fistula ambalo hujulikana kama Anal fistula

5. Mtu kupatwa na majeraha yoyote au michubuko kwenye sehemu ya haja kubwa,kutokana na sababu mbali mbali kama vile; kufanya mapenzi kinyume na maumbile yaani Anal sex, kuumia kwenye ajali n.k

6. Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Bacteria,Fangasi, Virusi,Minyoo n.k

7. Maambukizi ya baadhi ya magonjwa ya zinaa yaani sexual transmitted infections(STD's)

8. Magonjwa kama Crohn's, ambapo huu ni ugonjwa ambao huhusisha mtu kuvimba utumbo au kuwa na vidonda ambavyo huweza kuwepo kwenye utumbo lakini pia kwenye Rectum hata kupelekea mtu kuharisha au kujisaidia kinyesi kilichochanganyika na Damu

9. Tatizo la Levator Ani syndrome, ambapo misuli ya sehemu ya haja kubwa huwa dhaifu,kukakamaa,ukavu kupita kawaida,hali ambayo huleta maumivu ya njia ya haja kubwa hasa wakati wa kujisaidia

10. Tatizo la Pelvic Floor Dysfunction,ambapo misuli kwenye eneo lote la nyonga ikiwa ni pamoja na sehemu ya haja kubwa kushindwa kutanuka vizuri

11. Magonjwa mbali mbali ya ngozi kama vile; Psoriasis, maambukizi ya fangasi kwenye njia ya haja kubwa n.k

12. Tatizo la mtu kujisaidia kinyesi kigumu au kwa kitaalam hujulikana kama Constipation

13. Lakini pia kwa wakati mwingine ugonjwa wa Masundosundo au kwa kitaalam Genital warts huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili

VIPIMO VYA TATIZO HILI

Mgonjwa huweza kuchukuliwa history ya tatizo lake lilivyoanza, Kufanyiwa ukaguzi kwa njia mbali mbali kama vile; kuingiza kidole sehemu ya haja kubwa, kutumia kipimo cha Endoscopy n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI LA MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Tiba ya tatizo hili huanza kulingana na sababu za tatizo lenyewe,hivo kama tulivyochambua sababu mbali mbali hapo juu,ndivo na tiba zake huwa mbali mbali, ila kwa ujumla mgonjwa huweza kupata tiba kama vile;

• Matumizi ya baadhi ya dawa za kuondoa kabsa maumivu

• Matumizi ya dawa za kulainisha choo yaani stool softers pamoja na dawa za kulainisha misuli ya sehemu ya haja kubwa

• Kula vyakula na matunda yenye nyuzi nyuzi yaani Fibers kama maembe,machungwa,mapapai,

maparachichi n.k

• Huduma ya upasuaji kwa mgonjwa N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Jinsi ya Kupunguza Au Kuzuia kabsa Maumivu sehemu ya Haja Kubwa

Kuna vitu vya kufanya na Kuzingatia(Do) na kuna vitu vingine hushauriwi kuvifanya kabsa(Don't)

Zingatia mambo Haya(Do);

✓ Hakikisha unakunywa maji mengi kila siku

✓ Kula vyakula vyenye fibre au nyuzi nyuzi za kutosha, ikiwemo mboga za majani na matunda
NB: Maji pamoja na vyakula vya aina hii husaidia kulainisha choo chako na kuzuia tatizo la kupata choo kigumu(Constipation)

✓ Fanya Mazoezi ya mwili mara kwa mara(exercise regularly)

✓ Baada ya Kujisaidia haja kubwa,jisafishe na maji safi, au kama unatumia toilet paper, hakikisha inakuwa laini sio ngumu

✓ Tumia dawa za kutuliza Maumivu ikiwemo paracetamol

✓ Oga na maji ya moto ili kupunguza kuwasha na maumivu n.k

Usifanye kabsa Vitu hivi kama una tatizo hili(Don’t)

× usijikune karibu na sehemu ya haja kubwa

× Ukihisi haja kubwa jisaidie, epuka tabia ya kujibana kwa muda mrefu

× Usitumie nguvu sana wakati wa kujisaidia haja kubwa

× Usitumie sabuni zenye kemikali kali karibu na sehemu ya haja kubwa

× Epuka kula vyakula vyenye viungo vingi au kutumia pombe pamoja na vinywaji vingine vyenye kiwango kikubwa cha caffeine

× Usibebe au kunyanyua vitu vizito sana

× Usitumie dawa jamii ya ibuprofen kama unavuja damu sehemu ya haja kubwa(anus).

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Jeneza la Papa Francis kufunikwa kesho IjumaaAfyaclass Bongo Social •

Jeneza la Papa Francis kufunikwa kesho Ijumaa







Ibada ya kufunga jeneza la Hayati Papa Francis inatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa usiku Aprili 25, 2025, katika Basilika ya Mtakatifu Petro, Vatican.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumatano Aprili 23, 2025 na Mshereheshaji wa Nyumba ya Kipapa Jumatano, jeneza hilo litafungwa saa mbili kamili usiku kwa saa za Ulaya, sawa na saa 3:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

Ibada hiyo itaongozwa na Mwadhama Kardinali, Kevin Joseph Farrell, Camerlengo wa Kanisa Takatifu la Roma, kwa mujibu wa kanuni rasmi za mazishi ya Papa wa Roma (Ordo Exsequiarum Romani Pontificis nn. 66-81).

Mshereheshaji wa maadhimisho ya Kipapa, Askofu Mkuu Diego Ravelli, amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kwamba ibada hiyo ni sehemu ya mfululizo wa taratibu za heshima za mwisho kwa kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani.

0 Comment

Nimefanyiwa upasuaji mara 100 na siachi' Nini Ushauri wako hapaAfyaclass Bongo Social •

Nimefanyiwa upasuaji mara 100 na siachi' Nini Ushauri wako hapa



Abby Wu alikuwa na umri wa miaka 14 tu alipofanyiwa upasuaji wa urembo bandia kwa mara ya kwanza.

Baada ya kupata matibabu ya homoni, uzito wa mwili wa Abby uliongezeka kutoka kilo 42 hadi kilo 62 ndani ya miezi miwili.

Mwalimu wake wa michezo ya kuigiza aligundua mabadiliko hayo ya mwili.

Mwalimu wangu aliniambia, ''ulikuwa nyota lakini sasa umekuwa mnene kupita kiasi. Chagua moja uondoke kwa tasnia hii au upunguze kilo,'' anakumbuka alichoambiwa kipindi hicho akisubiri kufanya mtihani wake wa tamthilia.

Mama yake Abby aliingilia kati na kuamua kumpeleka kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mafuta tumboni na miguuni.

Abby anavuta kumbukumbu jinsi mamake alivyompa motisha akisubiri kufanyiwa operesheni hiyo.

''Kuwa mkakamavu na uingie ufanyiwe. Ukitoka hapo utakuwa mrembo zaidi.''

Upasuaji huo ulimuacha na makovu. Abby alipatiwa dawa za kupunguza uchungu lakini alikuwa macho akifanyiwa operesheni hiyo.

''Ningeona kiasi cha mafuta kilichotolewa mwilini mwangu na damu iliyokuwa ikinivuja,'' anasema.

"Upasuaji ulifanya kazi. Nilijiamini na kuwa na furaha zaidi, siku baada ya siku. Nadhani mama yangu alifanya chaguo sahihi."

Sasa Abby ana umri wa miaka 35 na amefanyiwa upasuaji wa urembo mara mia moja ikimgharimu dola nusu milioni.

Anamiliki kliniki ya ulimbwende katikati mwa mji wa Beijing na amekuwa mtu tajika katika tasnia ya upasuaji wa plastiki nchini China.



Lakini upasuaji huo pia unaathari zake kwa mwili.

Akiwa amekaa mbele ya kioo anajipodoa ili kuficha makovu ya sindano za kupunguza unene usoni, utaratibu anaoufanya kila mwezi ili kuhakikisha uchanga usoni mwake nakuhakikisha hana ngozi zilizolegea baada ya upasuaji wa kupunguza taya uliondoa mifupa mingi.

Lakini anasisitiza kuwa hajutii upasuaji wa urembo aliyofanya kufikia sasa akiamini kuwa mamake hakukosea kumuanzisha katika ulimbwende huu.

0 Comment

Ugonjwa wa Amoeba: Sababu, Dalili na MatibabuAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Amoeba: Sababu, Dalili na Matibabu

Ugonjwa wa amoeba ni ugonjwa hatari unaosababishwa na kimelea(parasite) kinachoitwa Entamoeba histolytica.

Entamoeba histolytica  ni kimelea kwenye kundi la anaerobic parasite na kwa mara ya kwanza hupatikana kwenye Utumbo mpana(colon);

Ingawa kutokana na Sababu zisizofahamika, kimelea hiki kina uwezo wa kutoka na kupita moja kwa moja mpaka kwenye Ini na kusababisha tatizo ambalo hujulikana kwa kitaalam kama amoebic liver abscesses."

Kimelea hiki kinaishi kwenye Utumbo wa binadamu na kinaweza kusababisha ugonjwa wa amoeba kwa mtu yeyote anayekula au kunywa kitu kilichoambukizwa na kimelea hiki.

Katika makala hii, tutajifunza kuhusu sababu, dalili na matibabu ya ugonjwa wa amoeba.

KUMBUKA; amoebiasis-Ndyo ugonjwa wenyewe ambao chanzo chake ni kimelea au parasite anayejulikana kama Entamoeba histolytica.

NANI YUPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA AMOEBA(AMOEBIASIS)?

Ingawa mtu yoyote anaweza kuugua Ugonjwa wa amoeba, Tatizo hili huwapata sana watu ambao wanaishi kwenye mazingira machafu,

Lakini Pia baadhi ya Tafiti zinaonyesha Ugonjwa wa Amoeba(amoebiasis) huwapata sana Wanaume wanaoshiriki Mapenzi na wanaume wenzao

Sababu ya Ugonjwa wa Amoeba:

Ugonjwa wa amoeba husababishwa na kimelea kinachoitwa Entamoeba histolytica,

Kimelea hiki hupatikana kwenye kinyesi cha mtu aliyeambukizwa na kinaweza kuambukiza mtu mwingine kupitia chakula au maji yaliyoambukizwa.

Mbali na hilo, mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwa kugusa vitu vilivyoambukizwa kwa mikono iliyochafuliwa na kimelea hiki.

Dalili za Ugonjwa wa Amoeba:

Baadhi ya dalili za ugonjwa wa amoeba ni pamoja na:

  1. Mtu Kuharisha mara kwa mara
  2. Mtu Kupata Maumivu ya tumbo
  3. Kupoteza hamu ya kula
  4. Kuhisi Kichefuchefu pamoja na Kutapika
  5. Kuhisi kizunguzungu n.k

Katika baadhi ya matukio, ugonjwa huu unaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi ya kiafya kama vile;

  • kuvuja kwa damu kwenye utumbo
  • Pamoja na maambukizi kwenye ini.

DALILI ZA UGONJWA WA AMOEBA NI PAMOJA NA;

- Mgonjwa kujisaidia kinyesi chenye vitu kama makamasi

- Mgonjwa kuanza kupata maumivu ya tumbo sana mithili ya tumbo kusokota

- Mgonjwa kuanza kujisaidia choo kilaini sana

- Mgonjwa kuharisha au kujisaidia haja kubwa ya maji maji sanaa

- Mgonjwa kujisaidia kinyesi ambacho kimechanganyika na damu

- Mgonjwa kutoa hewa kwa njia ya haja kubwa mara kwa mara(kujamba)

- Mgonjwa kupata maumivu ya tumbo,Kifua na viungo mbali mbali vya mwili

- Joto la mwili la mgonjwa kupanda au mgonjwa kuwa na Homa

- Mgonjwa kupatwa na tatizo la kupungukiwa na damu 

- Kupoteza appetite ya chakula kabsa

- Mgonjwa kupatwa na hali ya kichefu chefu pamoja na kutapika

- Mgonjwa kupungua uzito wa mwili na kukonda

KUMBUKA; Moja ya njia ya mtu kupata vimelea hivi vya amoeba ambavyo husababisha ugonjwa huu wa amiba ni pamoja na kunywa maji machafu sana.

Maji ambayo yamechanganyika ma kinyesi cha mtu ambaye alikuwa na vimelea hivi vya amoeba.

Matibabu ya Ugonjwa wa Amoeba:

Matibabu ya ugonjwa wa amoeba hutegemea kiwango cha ugonjwa na dalili zinazojitokeza,

Dawa za kuuwa vimelea hivi vinavyosababisha Ugonjwa wa amoeba hutumiwa kutibu ugonjwa huu.

Matibabu ya maumivu ya tumbo pia yanaweza kutolewa kwa wagonjwa ambao wanapata maumivu makali.

Kwa kuongezea, lishe bora ni muhimu katika kusaidia kupona haraka kwa ugonjwa huu.

Kuzuia Ugonjwa wa Amoeba:

Kuzuia ugonjwa wa amoeba ni muhimu sana ili kuepuka madhara ya kiafya. Baadhi ya njia za kuzuia ugonjwa huu ni pamoja na:

✓ Kufuata kanuni zote za usafi wa mazingira

✓ Kunywa maji safi na salama

✓ Kula chakula kilichoandaliwa vizuri

✓ Nawa Mikono kwa Sabuni na Maji safi kabla ya kula au kunywa kitu chochote

#SOMA ZAIDI Hapa Ugonjwa wa Amiba

Conclusion(Hitimisho):

Ugonjwa wa amoeba ni ugonjwa unaosababishwa na kimelea kinachoitwa Entamoeba histolytica. Kimelea hiki kinaishi kwenye Utumbo wa binadamu na kinaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya.

Ni muhimu kufuata kanuni zote za usafi wa mazingira na kula chakula kilichoandaliwa vizuri ili kuzuia ugonjwa huu. Kama unapata dalili za ugonjwa wa amoeba, ni muhimu kuwahi Hospital ili kupata matibabu sahihi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Masharti kwa watu wanaotaka kwenda kusoma nje ya nchiAfyaclass Bongo Social •

Masharti kwa watu wanaotaka kwenda kusoma nje ya nchi



Serikali imesema utaratibu ni lazima waombaji wa vyuo vya nje wapate barua za kuwatambulisha na kuwasaidia kupata vyuo na kozi wanazokwenda kusoma.

Dodoma. Serikali ya Tanzania imetoa maelekezo na masharti kwa watu wanaotaka kwenda kusoma nje ya nchi ikiwamo kuwa na barua  maalumu inayotolewa na Serikali ili kujua wanakwenda kusoma nini na katika chuo gani.

Maagizo hayo yametolewa leo Jumatano Aprili 23, 2025 na Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ng’wasi Kamani.

Mbunge huyo ameuliza upi mkakati wa Serikali katika kuhakikisha vijana wanaohitimu masomo nje ya nchi wakiwemo waliosoma katika nchi za Afrika Mashariki wanasajiliwa katika mifumo ya elimu nchini.

Mbunge huyo amesema kwa sasa vijana waliosoma nje ya nchi wapo mitaani wanahangaika, kwani wanakataliwa kusajiliwa na taasisi husika kwa madai ya kutokutambua elimu zao.

”Nitoe wito na ushauri kwa wale wanaotaka kwenda nje, wahakikishe wanapata cheti cha kutambua  wanakwenda kusoma chuo gani na taaluma ipi,  kuwalinda wao na taaluma zisiweze kuleta athari nje ya nchi,” amesema Kipanga.

Kipanga amesema vijana wanaotaka kwenda kusoma nje wanatakiwa kupewa hati ya ruhusa (cheti) kabla ya kwenda nje kusoma, Serikali itawezesha kutambua chuo na kozi anaporudi iweze kutambua na kumsajili kutokana na taaluma aliyopata.

Kuhusu Serikali kuwasaidia waliosoma Vyuo vya Afrika Mashariki, amesema usajili wa wahitimu kutoka vyuo vya nje ya nchi ikiwa ni pamoja na vya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hufanywa na mamlaka za usajili au bodi za kitaaluma kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

Amesema kabla ya usajili muhitimu hutakiwa kupeleka vyeti vya taaluma Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na wale wa stashahada na cheti huvipeleka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kuvithibitisha, kufanya ulinganifu wa sifa na kiwango cha elimu. “Hivyo napenda kuwasihi wahitimu wote kutoka vyuo vya nje ya nchi kufuata utaratibu uliopo ili kupata usajili.

0 Comment

FMD yagunduliwa katika mifugo nchini Slovakia na HungaryAfyaclass Bongo Social •

FMD yagunduliwa katika mifugo nchini Slovakia na Hungary



Wizara ya kilimo ya Brandeburg, imesema kuwa Shirika la Dunia la Afya ya Wanyama liliidhinisha ombi la kuondoa vizuizi katika eneo lililoathiriwa siku ya Jumatatu.

Mripuko huo wa kwanza nchini Ujerumani katika zaidi ya miaka 35, uligunduliwa kwenye kundi la nyati huko Hönow, nje kidogo ya Berlin, mnamo mwezi Januari.

Baadaye, halmashauri kuu ya Ulaya iliamuru kuwekwa vizuizi umbali wa kilomita 6 kutoka eneo la mripuko , kuzuia usafirishwaji wa wanyama kutoka eneo hilo, huku nchi kadhaa zikitangaza kupiga marufuku uagizaji wa bidhaa za kilimo za Ujerumani.

Uchunguzi wa kina wa ugonjwa huo wa FMD kwa wanyama wa kufugwa na wa porini kwenye eneo lililoathirika umebainisha kutokuwepo kwa ugonjwa huo, hali iliyosababisha kuondolewa kwa vizuizi hivyo.

Kutokana na hali hiyo, Ujerumani imerejea katika hali yake ya kutokuwa na ugonjwa wa FMD bila chanjo.

Kwa kawaida, katika nchi za Umoja wa Ulaya, wanyama hawapatiwi chanjo ya ugonjwa huo wa FMD kwasababu unachukuliwa kuwa umetokomezwa kabisa kwenye eneo hilo.

FMD yagunduliwa katika mifugo nchini Slovakia na Hungary

Hata hivyo, hivi karibuni, maambukizi ya FMD yamegunduliwa katika mifugo nchini Slovakia na Hungary.

Waziri wa Kilimo wa Brandenburg Hanka Mittelstädt, ameonya kuwa bado kuna hatari ya ugonjwa huo wa wanyama kuingia tena Ujerumani kutoka maeneo yaliyoambukizwa, hasa kwa njia ya usafirishaji wa chakula au wanyama.

0 Comment

Wanne watajwa katika kinyang'anyiro cha kuwa Papa mpyaAfyaclass Bongo Social •

Wanne watajwa katika kinyang'anyiro cha kuwa Papa mpya



Maelezo ya picha,Wanaotajwa kuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwa Papa (kushoto kwenda kulia) Kadinali Peter Kodwo Appiah Turkson, kadinali Pietro Parolin, kadinali Luis Antonio Gokim Tagle, na kadinali Fridolin Ambongo Besungu

Uamuzi wa nani atakayechaguliwa kuwa Papa ajaye unaweza kuwa na athari kubwa kwa Kanisa Katoliki na waumini wake wapatao bilioni 1.4 duniani kote. Lakini pia huu ni mchakato mgumu na usiotabirika kwa sababu nyingi.

Baraza la Makadinali litakutana kwa faragha ndani ya Kanisa la Sistine ili kujadili na kupiga kura hadi jina moja litakaposhinda.

Kwa kuwa asilimia 80 ya makardinali walipewa wadhifa na Papa Francis mwenyewe, hii itakuwa mara yao ya kwanza kumchagua papa, huku wakileta mtazamo mpana wa kimataifa.

Kwa mara ya kwanza katika historia, chini ya nusu ya Makadinali wapiga kura watakuwa kutoka Ulaya.

Na ingawa uteuzi huo ulifanywa na Papa Francis, haukuwa wa upande mmoja, yaani si wa mrengo wa "kizamani" pekee wala "wa kisasa" pekee.

Kwa hivyo, ni vigumu zaidi kutabiri nani atakayechaguliwa kuwa Papa ajaye.

Je, makardinali wanaweza kumchagua Papa kutoka Afrika au Asia? Au wataegemea mmoja wa watendaji waandamizi wa Vatican?

Haya hapa ni baadhi ya majina yanayotajwa kama warithi wa Francis, na majina mengine yanatarajiwa kujitokeza katika siku zijazo.

Pietro Parolin

Uraia: Muitalia

Umri: 70

Kardinali Parolin ni mtu wa maneno machache kutoka Italia, ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Jimbo la Vatican chini ya Papa Francis cheo kinachomfanya kuwa mshauri mkuu wa Papa.

Pia anasimamia Curia ya Roma, ambayo ni utawala mkuu wa Kanisa.

Kwa kuwa amewahi kufanya kazi kama "naibu papa", anaweza kuonekana kuwa miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa.

Wengine wanamwona kama mtu anayependelea diplomasia na mtazamo wa kidunia zaidi ya kushikilia misingi ya mafundisho ya Kanisa, jambo ambalo linaweza kuwa udhaifu kwa baadhi lakini nguvu kwa wengine.

Hata hivyo, amewahi kukosoa ndoa za jinsia moja, akisema kura ya mwaka 2015 iliyozipitisha nchini Ireland ilikuwa "pigo kwa ubinadamu".

Ingawa watabiri wanaweza kumpa nafasi, Parolin anafahamu methali maarufu ya Kiitaliano kuhusu uchaguzi wa papa: "Anayeingia kwenye uchaguzi akiwa tayari ni papa, atatoka akiwa tu kardinali."

Japokuwa Italia imetoa mapapa 213 kati ya 266 waliopita, haijatoa Papa kwa miaka 40 sasa, na mwelekeo wa Kanisa kuhamia nje ya Ulaya unaweza kuzuia Italia kutoa mwingine kwa sasa.

Luis Antonio Gokim Tagle*

Uraia: Mfilipino

Umri: Miaka 67

Je, Papa ajaye anaweza kutoka Asia?

Kadinali Tagle ana uzoefu mkubwa wa kiutume yaani amekuwa kiongozi wa Kanisa anayefanya kazi moja kwa moja na waumini badala ya kuwa mwanadiplomasia wa Vatican au mtaalamu wa sheria za Kanisa.

Kanisa Katoliki lina ushawishi mkubwa nchini Ufilipino, ambako takriban asilimia 80 ya watu ni Wakatoliki. Kwa sasa nchi hiyo ina Makadinali watano idadi ambayo inaweza kuwa na uzito ikiwa wote watamuunga mkono.

Yeye ni wa msimamo wa wastani, na amekuwa akifananishwa na Papa Francis kutokana na msisitizo wake juu ya masuala ya kijamii na huruma kwa wahamiaji.

Amesema wazi kupinga utoaji mimba, akilitaja kama "aina ya mauaji", jambo linaloendana na msimamo wa Kanisa kwamba uhai huanza wakati wa kutungwa kwa mimba.

Lakini mwaka 2015, alipokuwa Askofu Mkuu wa Manila, alitoa wito kwa Kanisa kufikiria upya ukali wake dhidi ya mashoga, waliotalikiana, na akina mama wasio na waume, akisema kuwa ukali huo umesababisha majeraha ya kudumu na kuacha watu wakihisi "wamewekwa alama".

Ameshawahi kutajwa kuwa kati ya wanaopewa nafasi ya kuwa Papa tangu mwaka 2013.

Alipoulizwa miaka 10 iliyopita kuhusu tetesi hizo, alijibu: "Nazichukulia kama utani! Zinachekesha."

Fridolin Ambongo Besungu*

Uraia: Mkongo

Umri: Miaka 65

Inawezekana kabisa Papa ajaye akatokea Afrika, ambako Kanisa linaendelea kushamiri.

Kadinali Ambongo ni mmoja wa wanaopewa nafasi, akiwa ametoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Ameshika wadhifa wa Askofu Mkuu wa Kinshasa kwa miaka saba na aliteuliwa kuwa kadinali na Papa Francis.

Ni mkosoaji mkubwa wa ndoa za jinsia moja, akisema kuwa "muungano wa watu wa jinsia moja ni kinyume na maadili ya kitamaduni na ni uovu wa asili."

Ingawa Ukristo ni dini kubwa DRC, Wakristo nchini humo wamekumbana na mateso na vifo kutoka vita vya wenyewe kwq wenyewe. Katika mazingira hayo, Kadinali Ambongo anaonekana kama mtetezi imara wa Kanisa.

Lakini mwaka 2020, alieleza msimamo wa kuvumiliana kidini, akisema: "Wa-Protestanti wabaki wa-Protestanti, Waislamu wabaki Waislamu. Tutashirikiana nao, lakini kila mtu abaki na utambulisho wake."

Kauli kama hizo zinaweza kuwafanya baadhi ya makadinali kujiuliza kama anakubaliana kikamilifu na mtazamo wa Kanisa wa kueneza injili kote ulimwenguni.

Peter Kodwo Appiah Turkson*

Uraia: Mghana

Umri: Miaka 76

Kama atachaguliwa, Kardinali Turkson atakuwa Papa wa kwanza kutoka Afrika katika kipindi cha miaka 1,500.

Kama Ambongo, amewahi kusema hatamani nafasi hiyo. "Sina hakika kama kuna mtu anayetamani kuwa Papa," aliiambia BBC mwaka 2013.

Alipoulizwa kama Afrika ina nafasi nzuri ya kutoa Papa kutokana na ukuaji wa Kanisa barani humo, alisema uchaguzi wa Papa haupaswi kuzingatia takwimu tu, kwa sababu "vigezo hivyo huchanganya mwelekeo."

Yeye alikuwa Mghana wa kwanza kuteuliwa kuwa Kadinali, mwaka 2003 chini ya Papa Yohane Paulo II.

Ni mpiga gitaa aliyecheza kwenye bendi ya muziki wa funk, na anajulikana kwa ushwwishi wake wenye nguvu.

Kama Makadinali wengi kutoka Afrika walivyo, yeye pia ana misimamo ya kihafidhina.

Hata hivyo, amepinga sheria kali dhidi ya mashoga katika nchi kama Ghana.

Katika mahojiano ya 2023 na BBC, wakati Ghana ilikuwa inajadili muswada wa kuwahukumu watu wa LGBTQ+, Turkson alisema kuwa "ushoga haupaswi kuhesabiwa kama kosa."

Lakini mwaka 2012, aliwahi kukosolewa kwa kutoa kauli za kuchochea hofu kuhusu kuenea kwa Uislamu barani Ulaya katika kongamano la maaskofu Vatican, jambo ambalo baadaye aliomba msamaha.

Via:Bbc

Papa mpya anachaguliwa vipi?22 Aprili 2025

Hizi ndizo saa za mwisho za Papa zilivyokuwa22 Aprili 2025

Mfahamu Kadinali Kevin Farrell, anayeongoza Vatican baada ya kifo cha Papa22 Aprili 2025

Imetafsiriwa na Yusuph Mazimu

0 Comment

Tatizo la fangasi wa ngozi,chanzo,dalili na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

Tatizo la fangasi wa ngozi,chanzo,dalili na Tiba yake








Ngozi kuwa na mabaka mabaka meupe huweza kuwa ni maambukizi ya Fangasi wa ngozi ambapo hujulikana zaidi kama Pityriasis versicolor au tinea versicolor.

Maambukizi haya huweza kushambulia na kuathiri ngozi yako,hali ambayo hufanya ngozi kuwa na mabaka mabaka meupe mfano wa kwenye Picha hapo.

Tatizo la fangasi wa ngozi

Maambukizi ya Fangasi kwenye ngozi kwa Lugha nyingine hujulikana kama mycosis

Kuna mamilioni ya aina za fungi ambao Wanaishi kwenye uchafu, kwenye mimea, kwenye nyumba,na kwenye ngozi yako. Wakati mwingine, fangasi hawa wanaweza kusababisha matatizo ya ngozi kama vile vipele au Rashes

Dalili za Fangasi kwenye Ngozi

Baada ya kushambuliwa na Fangasi kwenye Ngozi,Zipo dalili mbali mbali ambazo huweza kujitokeza kwako, dalili hizo ni pamoja na;

  • Kupata muwasho kwenye ngozi
  • Ngozi kutoka magamba(Scaly skin)
  • Ngozi kuwa nyekundu eneo lililoathiriwa
  • Ngozi kuwa na mabaka mabaka meupe
  • Ngozi kuwa na Vipele au rashes
  • Kuvimba
  • Ngozi kuwa na vitu kama mashilingi(Tazama kwenye picha)
  • Kupata dalili ya malengelenge kwenye ngozi
  • Ngozi kutoa Unga n.k

Aina ya Fangasi kwenye Ngozi

Zipo aina mbali mbali za Fangasi kwenye ngozi,na baadhi ya aina hizo ni pamoja na;

1.Athlete’s foot au tinea pedis:

Hii ni aina ya Fangasi ambao hushambulia Miguu.Fangasi hustawi katika mazingira yenye joto na unyevunyevu kama vile kwenye viatu, soksi, mabwawa ya kuogelea, vyumba vya kubadilishia nguo, na sehemu ambapo wanaoga watu wengi.

Maambukizi haya ni ya kawaida zaidi kwa watu wanaovaa viatu vinavyobana miguu, watu ambao hawabadili soksi mara kwa mara, na kutumia bafu za umma au mabwawa. Kuvu au Fangasi wanaohusika wanaweza huishi kwenye tishu zilizokufa za nywele, kucha za miguu, na tabaka za nje za ngozi, huku Trichophyton rubrum wakiathiri Zaidi maeneo haya.

2. Jock itch au tinea cruris:

Hii ni Aina ya fangasi inayoitwa tinea ambayo husababisha maambukizi haya. Kuvu au Fangasi hawa hustawi katika maeneo yenye joto na unyevunyevu kama vile sehemu za siri, mapajani na matakoni.

Maambukizi ni ya kawaida zaidi wakati wa majira ya joto au katika hali ya hewa ya joto na ya mvua. Jock itch inaonekana kwa dalili kama vile;

  • Kupata upele mwekundu kwenye ngozi,
  • kupata muwasho wa ngozi,
  • kuwa na upele wenye umbo la pete kwenye ngozi(ring-shaped rashes)n.k.

Jock itch inaambukiza kwa kiasi kidogo tu, inaenea kwa mgusano wa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia vitu vilivyobeba kuvu au fangasi hawa. Dalili ni pamoja na:

✓ Kupata muwasho au hali ya kuwaka moto katika eneo la sehemu za Siri au kwenye mapaja

✓ Upele mwekundu wa mviringo na kingo zilizoinuliwa,

✓ Hali ya uwekundu,Kuchubuka, au kupasuka kwa ngozi n.k

3. Ringworm, or tinea corporis:

Ringworm, au tinea corporis, ni maambukizi ya Fangasi wa ngozi yaliyopewa jina kutokana na upele wake wenye umbo la pete na ukingo unaofanana na minyoo.

Fangasi hawa huambukiza na wanaweza kuenea kwa kugusana moja kwa moja na watu walioambukizwa au wanyama au kwa kugusa nguo au samani zilizochafuliwa.

Joto na unyevu vinaweza kusaidia kuenea kwa maambukizi. Dalili zake ni pamoja na;

  • kidonda chekundu, cha duara na bapa chenye ngozi ya magamba – ambapo sehemu ya nje ya kidonda inaweza kuinuliwa, huku katikati ikionekana kawaida.
  • Upele mithili ya Pete nyekundu au viraka vinavyoweza kuingiliana.

3. Yeast infections:

Maambukizi ya fangasi hawa kwenye ngozi yako huitwa cutaneous candidiasis. Aina ya fangasi iitwayo candida husababisha maambukizo haya inapokua sana.

Mara nyingi fangasi hawa hupatikana katika sehemu zenye joto, unyevunyevu, zilizopasuka za mwili wako, ikijumuisha kwapani,sehemu za siri au kwenye kinena. Mara nyingi hutokea kwa watu wenye fetma au ugonjwa wa kisukari. Pia, ikiwa unatumia antibiotic, kuna uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya chachu yaani yeast infection.

4. Onychomycosis:

Onychomycosis ni maambukizi ya Fangasi ambayo huathiri sana kwenye vidole vya miguu au vidole vya mikono. Maambukizi haya Husababisha kucha zako kubadilika rangi, kuwa nene, na wakati mwingine kujitenga na eneo la kucha kujishikiza.

Hali hiyo ni ya kawaida zaidi kwa watu wazima kutokana na matatizo kama vile mtiririko mbaya wa damu, matatizo ya mfumo wa kinga, na kisukari. Onychomycosis huathiri kucha za Miguu mara nyingi zaidi kuliko kucha za Vidole kwa sababu hukua polepole zaidi, huwa na mtiririko mdogo wa damu, na kwa kawaida huwa katika hali ya giza na unyevu unyevu.

Uvaaji wa Viatu vinavyobana sana,Soksi chafu au zenye unyevu unyevu,hukuweka kwenye hatari Zaidi ya kupata maambukizi haya.

Sababu zinazoongeza Hatari ya kupata Maambukizi ya Fangasi kwenye Ngozi;

Una uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya Fangasi kwenye ngozi ikiwa:

– Unamawasiliano ya karibu au kugusana(Close contact) na mtu au mnyama aliyeambukizwa

– Unaazima viatu au nguo ambazo zina fangasi hatari

– Unatumia dawa jamii ya antibiotics kwa muda mrefu Zaidi

– Una uzito kupita kiasi

– Una magonjwa kama kisukari

– Unatatizo la kutoa jasho  sana

– Unavaa Viatu vinavyobana sana,Soksi chafu au zenye unyevu unyevu

– Kuwa na mfumo wa kinga dhaifu

– Kuishi katika mazingira ya joto au mvua

– Unavaa nguo za kubana au viatu ambavyo havina mzunguko mzuri wa hewa n.k.

Matibabu ya Fangasi hawa

Zipo Dawa za antifungal za aina mbali mbali za kupata yaani Topical antifungals, na Za Vidonge vya Kunywa,

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Papa Francis afariki dunia akiwa na umri wa miaka 88Afyaclass Bongo Social •

Papa Francis afariki dunia akiwa na umri wa miaka 88



 #BREAKING: Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, amefariki dunia April 21,2025 kwenye Jumatatu ya Pasaka akiwa na umri wa miaka 88 ambapo Vatican imethibitisha na kusema Papa amefia kwenye makazi yake Vatican na taarifa zaidi kuhusu kifo chake zitatolewa.

Papa ambaye alizaliwa mwaka 1936 hivi karibuni amepitia changamoto ya upumuaji hadi kuhitaji mashine ya kusaidia kupumua na amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kiafya ikiwemo maambukizi ya mapafu(nimonia) hadi kupelekea kulazwa kwa wiki kadhaa kabla na baadaye afya yake kuimarika.

0 Comment

Tatizo la Mchafuko wa damu,chanzo,dalili na TibaAfyaclass Bongo Social •

 


Tatizo la Mchafuko wa damu,chanzo,dalili na Tiba

Mchafuko wa damu; hiki ni kiswahili ambacho watu wamezoea kukitumia lakini maana yake ni “maambukizi kwenye damu-blood infection”

Endapo damu yako imepimwa na kuonekana ina viini vya magonjwa kama vile bacteria n.k utaambiwa damu yako ni Chafu au una tatizo la mchafuko wa damu.

Maambukizi kwenye damu kwa Lugha nyingine tunaita Blood Infection au kwa kitaalam Zaidi wanatumia neno “Sepsis”

Sepsis ni nini?

Sepsis ni pale ambapo mwili wako unakuwa na mwitikio mkali dhidi ya maambukizi kwenye damu. Wakati huo mfumo wako wa kinga, ambao kwa kawaida unakukinga dhidi ya vijidudu, huanza kushambulia tishu za mwili wako.

Hii husababisha uvimbe unaoweza kusababisha uharibifu wa viungo. Pia ni kawaida kwa mabonge ya damu kuundwa hali ambayo hupunguza mtiririko wa damu kwenye viungo vyako vya ndani, na kusababisha visipate virutubisho na oksijeni inayohitajika.

Mchafuko wa damu huhusisha kuwa na vimelea vya magonjwa kwenye damu, vimelea hivo ni pamoja na;

  • Bacteria(asilimia kubwa)
  • Fangasi
  • Virusi
  • Parasites

Chanzo cha Mchafuko wa damu

Kama tulivyosema, haya ni maambukizi ya viini vya magonjwa kwenye damu, viini hivi ni pamoja na bacteria, parasites, fangasi au viruses.

Unaweza kupata maambukizi kwenye damu kwa njia mbali mbali ikiwemo;

  • Kupitia IV lines kama upo hospitalini,
  • Kwenye vidonda
  • Kupitia mpira ya mkojo(urinary catheters)
  • vyakula unavyokula ikiwemo nyama n.k

Maambukizi haya huweza kupelekea tatizo la Sepsis;

– Pneumonia

– UTI-Urinary tract infections

– maambukizi kwenye kidole tumbo-appendix (appendicitis)

– Maambukizi tumboni(Abdominal infection)

– Maambukizi kwenye Ini au kifuko cha nyongo

– Maambukizi kwenye Ubongo au Uti wa mgongo

Aina ya Bacteria wanaosababisha mchafuko wa damu

Aina ya Bacteria wanaosababisha kwa kiasi kikubwa mchafuko wa Damu(Sepsis) ni pamoja na;

  • Staphylococcus aureus (S. aureus),
  • Streptococcus pyogenes (S. pyogenes),
  • Klebsiella spp.,
  • Escherichia coli (E. coli),
  • Pamoja na Pseudomonas aeruginosa (P. aeruginosa)

Watu ambapo wapo kwenye hatari ya kupata Mchafuko wa Damu

Watu ambapo wapo kwenye hatari ya kupata mchafuko wa damu ni pamoja na;

• Wenye kinga dhaifu ya Mwili

• Wenye magonjwa kama vile;

• Wajawazito

• Ambao wameshawahi kupata tatizo la mchafuko wa damu hapo kabla

• Wenye umri wa Zaidi ya miaka 65, hasa hasa ikiwa wana matatizo mengine ya kiafya

• Waliowahi kulazwa hospital kwa kuugua sana muda mrefu au kufanyiwa Upasuaji

• Wanaotumia mpira wa mkojo(Urinary cathers) au mipira ya kupumulia(breathing tubes)

• Wenye Vidonda vikubwa, kuungua au kupata majeraha mbali mbali kwenye ngozi

Dalili za Mchafuko wa damu

Hizi hapa ni baadhi ya dalili za mchafuko wa damu;

1. Kuwa na Homa

2. Mwili kutetemeka sana

3. kupata shida ya kukosa pumzi au kupumua kwa shida

4. Kuwa na dalili kama za kuchanganyikiwa

5. Joto la mwili kushuka sana

6. Kukojoa kidogo sana kuliko kawaida au kutokukojoa kabsa.

7. Mapigo ya Moyo kwenda mbio

8. Kuhisi kichefuchefu na kutapika

9. Kupata tatizo la Kuharisha

10. Mwili kuchoka sana, kuwa dhaifu au kukosa nguvu

11. Kutoa sana jasho

12. Kupata maumivu makali ikiwemo ya kichwa n.k

13. Kupata upele kwenye ngozi(Skin rashes)

14. Kuhisi kizunguzungu

15. Kuhisi usingizi sana

16. Ngozi kuwasha sana n.k

Ukiona dalili hizi hakikisha unapata Msaada Mapema au;

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Kampeni ya chanjo dhidi ya polio kwa watoto yazinduliwa ukanda wa Ziwa ChadAfyaclass Bongo Social •

Kampeni ya chanjo dhidi ya polio kwa watoto yazinduliwa ukanda wa Ziwa Chad



Mawaziri wa afya kutoka Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Niger, Nigeria na Chad wamekutana leo huko N'Djamena Chad kuzindua kampeni ya pamoja ya chanjo dhidi ya polio kwa watoto zaidi ya milioni 83 walio na umri wa chini ya umri wa miaka mitano katika Ukanda wa Ziwa Chad.

Hii ni hatua muhimu katika kukabiliana na kirusi cha polio cha aina ya pili kinachosambaa katika eneo hili. Imesema taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO huko N'Djamena mji mkuu wa Chad.

Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, WHO inasema kirusi hiki kimegunduliwa katika mazingira ya maji taka na kwa watu waliopatwa nacho katika nchi za Cameroon, Niger, Nigeria na Chad, ambapo jumla ya visa 210 viliripotiwa, 140 kati ya hivyo vikisababisha ugonjwa wa kupooza.

Ingawa Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, haijaripoti kisa chochote, bado kuna hatari kubwa ya maambukizi kuvuka mipaka limeonya shirika la WHO.

Limeongeza kuwa Kampeni za chanjo kati ya Aprili 2024 na Januari 2025 zilifanikiwa kuwafikia watoto milioni 12. Ili kuongeza kinga, kampeni nyingine ya pamoja itafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 28 Aprili 2025, ikilenga maeneo ya mipakani yenye hatari kubwa na usimamizi hafifu wa afya.

Wahudumu wa afya zaidi ya milioni moja kushiriki kampeni

Kwa mujibu wa WHO kampeni hii itaendeshwa na wahudumu wa afya wapatao milioni 1.1, wakiwemo watoa chanjo, watoa elimu ya afya na wasimamizi.

Mawaziri wa afya pia watafanya kikao cha ndani kujadili changamoto, takwimu za ugonjwa huo na ushirikiano wa kuvuka mipaka, kwa mujibu wa Mpango wa Kikanda wa Kutokomeza Polio Afrika 2024-2025.

Waziri wa Afya wa Chad, Mhe. Dkt. Abdelmadjid Abderahim amesema “Ukanda wa Ziwa Chad unasalia kuwa eneo muhimu katika mapambano yetu dhidi ya polio. Kwa kushirikiana kama kanda, tunaimarisha dhamira yetu ya kuutokomeza ugonjwa wa polio kabisa.

Mashirika ya kimataifa kama WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, Wakfu wa Gates, Muungano wa chanjo duniani Gavi na Rotary International yanaunga mkono juhudi hizi, pamoja na jamii na viongozi wa maeneo husika. Mkutano huo unaambatana na Wiki ya Chanjo Afrika yenye kaulimbiu “Chanjo kwa wote inawezekana”.

WHO imesema mpango huu ni mfano wa mshikamano katika afya ya kimataifa ili kujenga mustakabali usio na polio kwa watoto wa Ukanda wa Ziwa Chad na zaidi.

0 Comment

kutokwa na uchafu kwa mjamzito,Kutokwa na uchafu ukeni kwa mjamzitoAfyaclass Bongo Social •

kutokwa na uchafu kwa mjamzito,Kutokwa na uchafu ukeni kwa mjamzito



Kutokwa na uchafu ukeni kwa mjamzito ni jambo la kawaida katika ujauzito, lakini pia linaweza kuwa ishara ya matatizo fulani kulingana na rangi, harufu, kiasi, au maumivu yanayoambatana nalo. Hapa nitakupa maelezo ya kina kuhusu hali hii:


1. Uchafu wa Kawaida kwa Mjamzito

Katika kipindi cha ujauzito, mwili wa mwanamke hupitia mabadiliko makubwa ya homoni, hasa ongezeko la homoni ya estrogeni na mtiririko wa damu kwenye via vya uzazi. Hii husababisha uzalishaji wa ute zaidi ukeni ambao:

  • Unajulikana kama leukorrhea (ute mwepesi, mweupe).
  • Hauna harufu kali.
  • Unaweza kuwa na muundo wa ute ute au maji maji.
  • Unazidi kadri ujauzito unavyosonga mbele.

Uchafu huu ni wa kawaida na husaidia kuzuia maambukizi kwa kuosha na kuondoa vimelea vinavyoingia ukeni.


2. Aina za Uchafu Usio wa Kawaida kwa Mjamzito

Zifuatazo ni aina za uchafu ambazo si za kawaida na zinaweza kuashiria tatizo:

a. Uchafu wa Njano au Kijani

  • Mara nyingi huashiria maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama Trichomoniasis au Gonorrhea.
  • Huambatana na harufu mbaya, kuwashwa, au Maumivu wakati wa kukojoa.

b. Uchafu wa Kijivu

  • Unaweza kuwa ishara ya bacterial vaginosis (BV) — maambukizi yanayosababishwa na kutowiana kwa bakteria wa asili ukeni.
  • Huambatana na harufu kama ya shombo la samaki, hasa baada ya tendo la ndoa.

c. Uchafu mweupe mzito kama Maziwa mtindi

  • Huashiria maambukizi ya fangasi (yeast infection).
  • Huchangamana na muwasho mkali, uwekundu ukeni na maumivu wakati wa tendo la ndoa au kukojoa.

d. Uchafu wenye damu

  • Katika miezi ya mwanzo, unaweza kuwa dalili ya kuharibika kwa mimba au ujauzito kutunga nje ya mfuko wa Kizazi (Ectopic pregnancy).
  • Katika hatua za mwisho, unaweza kuashiria kuanza kwa uchungu wa kujifungua.
  • Pia unaweza kuwa kutokana na erosion ya Cervix au tendo la ndoa.

e. Uchafu mwingi kupita kiasi

  • Ingawa ute huongezeka, kama ni mwingi sana hadi kulowesha kabsa nguo za ndani, inaweza kuashiria kupasuka kwa chupa ya uzazi (amniotic fluid leak) — hasa kama hauna rangi, hauna harufu au una harufu ya bleach.

3. Dalili Zinazotakiwa Kumuona Daktari Haraka

Mjamzito anapaswa kuwasiliana na daktari au mkunga haraka ikiwa atakumbana na:

  • Uchafu wenye harufu kali.
  • Wenye Rangi isiyo ya kawaida (njano, kijani, kijivu, au damu nyingi).
  • Muwasho, uchungu, au uwekundu sehemu za siri.
  • Maumivu Makali sana ya tumbo Chini ya kitovu.
  • Homa au kuhisi uchovu kupita kiasi.
  • Mabadiliko ya ghafla ya uchafu — kiasi au muundo.n.k.

4. Hatua za Kujikinga na Maambukizi

  • Osha sehemu za siri kwa maji safi na sabuni isiyo na kemikali kali.
  • Epuka kujisafisha kwa kutumia vidhibiti vya harufu au dawa ukeni (douching).
  • Vaa nguo za ndani safi na zisizobana.
  • Tumia chupi zenye Material ya pamba.
  • Epuka ngono isiyo salama au isiyo na kinga.
  • Kunywa maji ya kutosha na kula lishe bora ili kuimarisha kinga ya mwili.

Hitimisho

Kutokwa na uchafu ukeni wakati wa ujauzito ni hali ya kawaida, lakini mabadiliko yoyote yasiyo ya kawaida yanapaswa kuchukuliwa kwa uzito. Uchunguzi wa mapema unaweza kusaidia kuzuia matatizo makubwa kwa mama na mtoto.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

TANZIA: Mwigizaji Caren afariki DuniaAfyaclass Bongo Social •

 TANZIA: Mwigizaji Caren afariki Dunia



Mwigizaji Caren amefariki Dunia leo April 15,2025 akiwa anapatiwa matibabu nchini India kutokana na maradhi ya tumbo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda wa zaidi ya miaka 8 .

Taarifa hizo zimethibitishwa na Mdogo wake Safinewin Rwegasira ambaye alienda nae India licha ya kuwa yeye aliwahi kurudi kwa ajili ya kumuangalia Mama yao ambaye ni Mgonjwa pia.

Mdogo wa Careen amesema mara ya mwisho kuongea na Dads yake ilikuwa usiku wa kuamkia leo na alikuwa kwenye hali nzuri tu alimuahidi Mama yao kuwa hatamani kufariki ili arejee mzima aweze kutimiza yale aliyoahidi.

“Nimeongea nae, alikuwa yuko vizuri tu Dada yangu akawa anaongea na Mama anamwambia Mama yangu naomba Mungu nisife kabla yako, sijatimiza ahadi zangu zote nilizokuahidi, alikuwa anatarajiwa kurudi tarehe 22, alikuwa amemaliza operation zote”

0 Comment

Wazazi nchini Uganda wakubali chanjo ya Malaria kwa watotoAfyaclass Bongo Social •

Wazazi nchini Uganda wakubali chanjo ya Malaria kwa watoto



Wazazi nchini Uganda wamekubali chanjo ya malaria kwa watoto wa chini ya umri wa miaka miwili, wakitarajia kuwa hatua hiyo itakuwa suluhu ya kudumu kufuatia shida na gharama za matibabu ya ugonjwa huo kwa watoto.

Afisa mkuu wa afya katika wilaya ya Apac Daktari James Odongo,  ameiambia DW kwamba ni vyema kuona zoezi hilo la kutoa chanjo limeanzia wilaya hiyo ambayo kwa muda mrefu imetambuliwa kuwa yenye kiwango cha juu cha visa vya wagonjwa wa malaria.

Mtu mmoja huumwa na mbu 1,500 kila mwaka

Daktari Odongo amesema kuwa katika wilaya hiyo, mtu mmoja huumwa na mbu 1,500 kila mwaka na asilimia 80 ya mbu hao wana vijidudu vya Malaria.

Wanawake wengi waliitikia mwito huo wa kuwapeleka watoto wao wenye miezi sita kupata chanjo hiyo. Kulingana na baadhi ya wazazi, licha ya kuwa na mashaka na chanjo hiyo mpya miongoni mwa chanjo zingine kwa watoto, wanasema ni afadhali kuliko madhila na gharama za kuwatibu watoto wao kila mara.

Ongezeko la aina mpya ya mbu sugu Afrika mashariki latishia vita dhidi ya Malaria

Hata hivyo, mmoja kati ya akina mama amelalamikia madhara yaliyomkumba mwanawe mara tu baada ya kupata chanjo hiyo. Mama huyo anasema , mwanawe alianza kutapika na kuendesha na akaingiwa na wasiwasi kama chanjo hiyo ilikuwa ni salama kwake.

Lakini Alfred Obote mhamasishaji wa kijiji kuhusu masuala ya afya maarufu kama VHT amesema hali hiyo hutokea ikiwa mtoto alikuwa anaugua malaria wakati alipopata chanjo.

Obote anasema hajasikia kisa chochote kuhusu madhara hayo lakini mama huyo amethibitisha kwamba mtoto huanzia kwenye hatua ya kwanza ya kupimwa kubaini ikiwa damu ina vijidudu vya Malaria.

Akina mama wajawazito ndio waathirika wakubwa wa Malaria

Akina mama wajawazito pia wametajwa kuwa waathirika wakubwa wa malaria katika wilaya hiyo. Wanakosolewa kwa kutokwenda kupata ushauri wakati wa ujauzito ili kupata kinga itakayowasaidia wao na watoto walio tumboni.

Daktari Odongo anaelezea kuwa tatizo kubwa la kuwatibu akina mama hao ni kwamba wanahitaji kuongezwa damu mwilini na mara nyingi vituo vya damu havina damu ya kutosha na iliyo stahiki kulingana na muhitaji, hali inayosababisha baadhi kufariki.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD