WHO yatangaza haya dhidi ya Ukeketaji unaofanywa na wahudumu wa afya

WHO yatangaza haya dhidi ya Ukeketaji unaofanywa na wahudumu wa afya

#1

WHO yatangaza haya dhidi ya Ukeketaji unaofanywa na wahudumu wa afya



Hatua za haraka zinahitajika ili kudhibiti ongezeko la ukeketaji wa wanawake (FGM) unaofanywa na wahudumu wa afya ("medicalized FGM") na kuwahusisha wahudumu wa afya katika kuzuia tendo hilo, kulingana na mwongozo mpya uliotolewa leo Aprili 28 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO).

Ingawa sekta ya afya ina jukumu muhimu katika kusitisha ukeketaji na kuwasaidia waathirika, ushahidi kutoka maeneo mbalimbali duniani unaonesha kuwa tendo hilo sasa linazidi kufanywa na wahudumu wa afya. Kufikia mwaka 2020, inakadiriwa kuwa wasichana na wanawake milioni 52 walikeketwa na wahudumu wa afya — takriban tukio 1 kati ya kila matukio manne.

Mwongozo mpya wa WHO, unaoitwa ‘Kuzuia ukeketaji wa wanawake na usimamizi wa kiafya wa matatizo yanayotokana na tendo hilo’, unatoa mapendekezo ya kuzuia ukeketaji na pia kuhakikisha huduma za afya za kitaalamu kwa waathirika, ukihusisha hatua kwa sekta ya afya, serikali, na jamii zilizoathirika.

Ni hatari

“Ukeketaji wa wanawake ni ukiukwaji mkubwa wa haki za wasichana na unahatarisha sana afya yao,” anasema Dkt. Pascale Allotey, Mkurugenzi wa WHO wa Afya ya Uzazi na Utafiti, na wa Mpango Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Uzazi wa Binadamu (HRP). “Sekta ya afya ina jukumu la msingi katika kuzuia FGM — wahudumu wa afya wanapaswa kuwa mawakala wa mabadiliko, si watekelezaji wa tendo hili hatari, na pia lazima watoe huduma bora kwa waathirika.”

Ukeketaji mara nyingi hufanywa kwa wasichana wadogo kabla ya kubalehe na unajumuisha taratibu zote zinazokatakata au kuharibu sehemu za siri za wanawake kwa sababu zisizo za kiafya. Ushahidi unaonesha kuwa, haijalishi nani anatekeleza FGM, bado husababisha madhara. Utafiti fulani unaonesha kuwa linaweza kuwa hatari zaidi likifanywa na mtaalamu wa afya, kwa kuwa kuna uwezekano wa kukata kwa kina zaidi. Uwekaji wake katika muktadha wa kiafya pia unaweza kuufanya uonekane kama halali, hivyo kuhatarisha juhudi za kuachana na tendo hilo kwa ujumla.

Kuwashirikisha wahudumu

Kwa sababu hizi, mwongozo mpya wa WHO unapendekeza kuwepo kwa kanuni za kitaaluma zinazokataza waziwazi wahudumu wa afya kufanya FGM. Pia, ukizingatia nafasi yao ya heshima katika jamii, unasisitiza umuhimu wa kuwaelimisha na kuwashirikisha kwa njia chanya wahudumu wa afya katika kuzuia ukeketaji. Mbinu nyeti za mawasiliano zinaweza kuwasaidia kukataa kwa ufanisi maombi ya kufanya FGM huku wakiwapa watu taarifa kuhusu madhara yake ya haraka na ya muda mrefu.

“Utafiti unaonesha kuwa wahudumu wa afya wanaweza kuwa viongozi wa maoni wenye ushawishi katika kubadili mtazamo kuhusu FGM, na wana nafasi muhimu katika kuzuia tendo hilo,” anasema Christina Pallitto, Mtafiti katika WHO na HRP aliyesimamia uundaji wa mwongozo huo mpya. “Kuwahusisha madaktari, wauguzi na wakunga kunapaswa kuwa sehemu kuu ya mikakati ya kuzuia na kukabiliana na FGM, huku mataifa yakijitahidi kumaliza tendo hilo na kulinda afya ya wanawake na wasichana.”

Pamoja na sheria madhubuti na sera, mwongozo unaangazia pia umuhimu wa elimu na uhamasishaji wa jamii. Shughuli za uelimishaji jamii zinazowahusisha wanaume na wavulana zinaweza kuwa na ufanisi mkubwa katika kuongeza maarifa kuhusu FGM, kutetea haki za wasichana, na kusaidia mabadiliko ya mitazamo.

Huduma kwa waathirika

Mbali na kuzuia, mwongozo huu pia unatoa mapendekezo ya kimatibabu ili kuhakikisha waathirika wa FGM wanapata huduma ya huruma na bora ya kiafya. Kutokana na madhara ya muda mfupi na mrefu yatokanayo na FGM, waathirika wanaweza kuhitaji huduma mbalimbali za afya katika hatua tofauti za maisha, kuanzia afya ya akili, usimamizi wa hatari za uzazi, hadi upasuaji wa kurekebisha madhara inapobidi.

Ushahidi unaonesha kuwa, kwa kujitolea ipasavyo na msaada wa kutosha, inawezekana kumaliza FGM. Mataifa kama Burkina Faso, Sierra Leone na Ethiopia yameshuhudia upungufu wa maambukizi kwa wasichana wenye umri wa miaka 15–19 kwa asilimia asilimia 50, asilimia 35 na asilimia 30mtawalia katika kipindi cha miaka 30 iliyopita kupitia hatua za pamoja na dhamira ya kisiasa ya kutekeleza marufuku na kuharakisha uzuiaji.

Tangu mwaka 1990, uwezekano wa msichana kukeketwa umepungua kwa mara tatu. Hata hivyo, FGM bado ni jambo la kawaida katika takriban nchi 30 duniani, na inakadiriwa kuwa wasichana milioni 4 bado wapo hatarini kila mwaka.

Reply


image quote pre code