Mikopo Asilimia 10% ifikie walengwa kikamilifu

Mikopo Asilimia 10% ifikie walengwa kikamilifu

#1

Mikopo Asilimia 10% ifikie walengwa kikamilifu



DAR ES SALAAM: MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ameahidi kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa mpango wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10.

Akizungumza katika Kongamano la Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Ilala lililofanyika leo Juni 14,2025 Dar es Salaam, Mpogolo amesema mikopo hiyo ni mikakati ya Serikali inayolenga kuwezesha wanawake kuwa na nguvu za kifedha na kujikwamua kiuchumi.

“Serikali ya Awamu ya Sita imetupa maelekezo thabiti kuhakikisha mikopo hii inawafikia walengwa hasa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Tutaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wake kwa uwazi na usawa bila kupendelea wala kuangalia upande wowote,” amesema Mpogolo.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, amesema kuwa zaidi ya Sh bilioni 5 zinaenda kuwanufaisha wanawake, jambo linaloonyesha jitihada za serikali kuimarisha nafasi ya mwanamke katika uchumi.

Amesema maandalizi ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vilivyoidhinishwa yamekamilika na mchakato utaanza kwa kufuata sheria, kanuni mpya, na mfumo wa kibenki.

Mikopo ya asilimia 10 ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita za kuleta maendeleo endelevu kwa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu.

REPLY HAPA


image quote pre code