Hii ni baada ya kuahidi kuwaachia 'watoto wake 106' utajiri wa £17bn'
Kliniki ya uzazi ya Moscow inawapa wanaotarajia kuwa akina mama nafasi ya kupata mtoto kupitia kwa, Pavel Durov, mmoja wa wajasiriamali waliofanikiwa zaidi nchini Urusi bila malipo.
Durov, bilionea mwanzilishi wa jukwaa la ujumbe la Telegram, amezaa watoto sita na wapenzi watatu tofauti. Lakini kijana huyo mwenye umri wa miaka 40 anaaminika kuwa na zaidi ya Watoto 100 baada ya kutoa mbegu za kiume kwa wingi kwa wanandoa wengi katika nchi 12 tofauti.
Kliniki ya AltraVita IVF, kituo kilichoko kusini-magharibi mwa mkoa wa Akademicheskaya wa Moscow pia kilifichua kuwa tajiri huyo wa teknolojia atafadhili utaratibu mzima.
"Pavel Durov yuko tayari kufadhili itifaki zote za IVF zinazotumia manii yake. Ni mchango wa ukarimu sana kwa jamii kutoka kwa mtu ambaye anataka kuwasaidia wale wanaotamani kuwa wazazi," ofa kwenye tovuti ya AltraVita inaeleza.
Akizungumza na RTVI Urusi, Mkurugenzi Mtendaji wa AltraVita Sergei Yakovenko - pia profesa msaidizi wa fizikia ya viumbe katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Moscow - alithibitisha kuwa ofa hiyo ni ya kweli na akaeleza kuwa alikuwa rafiki wa muda mrefu wa mwanzilishi wa Telegram.
Katika mahojiano wiki hii na jarida la Ufaransa la Le Point, tajiri huyo wa kiteknolojia alitangaza kuwa anapanga kuwaachia watoto wake wote utajiri wake wa pauni bilioni 17, akiongeza kwamba haoni tofauti kati ya watoto aliowapata kwa njia ya kawaida na wale waliotoka kwa msaada wa manii.
"Wote ni watoto wangu na wote watakuwa na haki sawa," Durov alisema. 'Sitaki watengane baada ya kifo changu.'
Lakini hakuna hata mmoja wao atapata pesa taslimu kwa miaka 30, aliongeza.
"Nataka waishi kama watu wa kawaida, wajenge maisha yao wenyewe, wajifunze kujiamini, waweze kuunda - wasiwe tegemezi kwenye akaunti ya benki."
REPLY HAPA
image quote pre code