Kwanini Watu Wakifurahi sana hulia,Tafiti hizi zinajibu

Kwanini Watu Wakifurahi sana hulia,Tafiti hizi zinajibu

#1

Machozi kwa kawaida huonekana kama ishara ya huzuni au maumivu, lakini pia watu hulia wakati wa furaha maishani: harusi, siku ya kuzaliwa, kuungana na uliyempoteza, ushindi katika michezo, au hata tendo la fadhili usilolitarajia.



Machozi ya furaha? Hii inaeleza jinsi ubongo wa mwanadamu unavyoshughulikia hisia kali.

Kulia ni jibu la kibayolojia pindi hisia zinapokuwa kubwa - na haibagui kati ya hisia nzuri na mbaya. Iwe hisia imechochewa na huzuni au furaha, machozi ni matokeo ya ubongo kujaribu kuchakata zaidi ya kile unachoweza kudhibiti kwa wakati huo.

Hisia chanya na hasi, huamsha mfumo wa limbic, sehemu ya ubongo inayohusika katika kuchakata hisia na kumbukumbu. Ndani ya mfumo huu, nyuroni hufanya kazi ya kuwa kengele ya hisia, inapotambua msisimko na kuufanya mwili ujibu.

Mfumo wa amygdala unapopokea hisia kali, huamsha maeneo mengine ya ubongo ikiwa ni pamoja na eneo la hypothalamus, eneo linalodhibiti utendaji kazi wa mwili, kama vile mapigo ya moyo, kupumua na kutoa machozi.

REPLY HAPA


image quote pre code