Tanzania na nchi zingine 35 huenda zikazuiwa kuingia Marekani
Utawala wa Rais Donald Trump unafikiria kuongeza vizuizi vya kusafiri kwa kuzifanya Nchi nyingine 36 ikiwemo Tanzania ziwekwe kwenye orodha ya Nchi za kuchunguzwa zaidi na ambazo Raia wake watazuiwa kuingia Marekani.
Japokuwa bado Serikali ya Marekani haijatoa tamko rasmi kuhusu Nchi hizi 36, ipo barua ya siri iliyovuja kutoka Mamlaka za Marekani ambayo Vyombo vya Habari Marekani ikiwemo Reuters na Washington Post vimeiona ikitaja Nchi hizo 36 ambazo zinaweza kusitishiwa moja kwa moja au kupewa zuio la muda fulani la Raia wake kuingia Marekani.
Nchi hizo 36 ni pamoja na Tanzania, Angola, Antigua na Barbuda, Benin, Bhutan, Burkina Faso, Cabo Verde, Cambodia, Cameroon, Cote D’lvoire, Democratic Republic of Congo, Djibouti, Dominica, Ethiopia, Egypt, Gabon, The Gambia, Ghana, Kyrgyzstan, Liberia, Malawi, Mauritania, Niger, Nigeria, Saint Kitts and Nevis, Saint Lucia, Sao Tome and Principe, Senegal, South Sudan, Syria, Tonga, Tuvalu, Uganda, Vanuatu, Zambia na Zimbabwe.
Miongoni mwa wasiwasi ambao Marekani imeutaja kuwa ni vikwazo ambavyo nchi hizo 36 zinapaswa kuvishughulikia ndani ya siku 60 ni pamoja na nchi hizo kushindwa kushirikiana kikamilifu na Marekani katika kurahisisha uondokaji wa Raia wake kutoka Marekani ambao walikuwa wametakiwa kuondoka wakiwemo Raia wa nchi hizo ambao wamezidisha muda wa visa waliotakiwa kuendelea kukaa Marekani na hivyo kubaki Marekani kinyume cha sheria badala ya kurudi makwao (over staying).
Sababu nyingine ni Serikali za nchi zilizotajwa kukosa uwezo au kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuzalisha nyaraka za vitambulisho zinazoweza kuaminika na pia pasipoti za nchi hizo kuwa na usalama unaotiliwa shaka kiusalama.
Sababu nyingine ni Raia wa nchi hizo kuhusika katika matendo ya ugaidi nchini Marekani, au kufanya matendo ya chuki dhidi ya Wayahudi na Marekani ambapo taarifa hiyo imeweka wazi kuwa sio kila mapungudu yaliyotajwa yanaigusa kila nchi iliyoorodheshwa bali kila nchi ina tatizo moja au zaidi kati ya yaliyotajwa na inatakiwa kuyashungulia ndani ya siku 60.
REPLY HAPA
image quote pre code