Tatizo la mgongo wazi,kwa watoto Chanzo,dalili na Tiba yake

Tatizo la mgongo wazi,kwa watoto Chanzo,dalili na Tiba yake

#1

Tatizo la mgongo wazi,kwa watoto Chanzo,dalili na Tiba yake



Tatizo la mgongo wazi(Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku Sehemu ya uti wa mgongo ikiwa wazi kutokana na mifupa au vipingili vya uti wa mgongo kutokufunga vizuri.

Uti wa mgongo hutengenezwa mara tu baada ya mimba kutungwa, ikiwa kuna kasoro katika utengenezaji  wa uti huu basi sehemu fulani ya uti wa mgongo itabaki bila kuzibwa.

Visababishi vya tatizo la Mgongo wazi kwa Watoto

Hakuna Sababu ya moja kwa moja ambayo mpaka sasa inafahamika kusababisha tatizo hili, ila tafiti zinaonyesha Kuna sababu mbalimbali zinazoongeza hatari ya uti wa mgongo kutoziba au mtoto kuwa na tatizo la mgongo wazi, Sababu hizo ni pamoja na;

1. Upungufu wa folic acid(vitamin B9) katika kipindi cha ujauzito

Tafiti zinaonyesha Folic acid husaidia sana kwenye uumbaji mzuri wa Sehemu hii ya uti wa mgongo,hivo upungufu wake huongeza hatari ya Mtoto kuwa na tatizo hili la mgongo wazi.

2. Family History:

Kuwa na historia kwenye familia ya Mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi au kasoro nyingine za neural tube huongeza hatari. 

Wazazi ambao wamepata mtoto mwenye kasoro ya mirija ya neva(Neural tube) wana nafasi kubwa zaidi ya kupata mtoto mwingine aliye na hali sawa na hiyo.

3. Matumizi ya baadhi ya Dawa

Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile valproic acid wakati wa ujauzito kumehusishwa na ongezeko la hatari ya kupata tatizo la mgongo wazi.

Ndyo maana,mama mjamzito anashauriwa kutokutumia dawa zozote pasipo maelekezo kutoka kwa Wataalam wa afya.

4. Kuwa na Ugonjwa wa Kisukari(Diabetes): 

Akina mama wenye ugonjwa wa kisukari, hasa ikiwa haujadhibitiwa vizuri, wana hatari kubwa ya kupata mtoto mwenye tatizo hili la mgongo wazi.

5. Sababu zingine ni pamoja na  Kuwa na tatizo la Unene kupita kiasi au Obesity: 

Pia zipo tafiti zinazoonyesha Unene kupita kiasi kwa mama huweza kuongeza hatari ya matatizo kwenye uti wa mgongo yaani neural tube defects, ikiwemo tatizo hili la Mgongo wazi au spina bifida kwa Mtoto atakayezaliwa.

Dalili za Tatizo la Mgongo wazi kwa Watoto

- Kuwa na uvimbe nyuma chini ya mgongo

- Mtoto Kushindwa kutembea ama kukosa hisia katika miguu

- Mtoto anaweza kushindwa kuzuia haja kubwa pia kwa baadhi ya Watoto

MATIBABU YA MGONGO WAZI

- Kuna tiba ya Upasuaji

- Dawa pamoja na viinilishe

Wanawake wengi walio katika kipindi cha kuzaa na wajawazito hawatumii vyakula vyenye vitamin B au folic acid inavyopaswa,hii pia huongeza hatari za tatizo hili.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

REPLY HAPA


image quote pre code