Wachunguzi wapata kinasa sauti kutoka kwa ndege ya Air India iliyoanguka
Wachunguzi wamepata kinasa sauti "cockpit voice recorder (CVR)" kutoka kwenye ndege iliyoanguka ya Air India, hatua muhimu katika kubaini kilichosababisha ajali ya wiki iliyopita.
Kinasa sauti kilikuwa kwenye kisanduku cheusi cha pili cha ndege ya Boeing 787, ambacho maafisa wa India walisema walikipata Jumapili. Kisanduku Cha kwanza, chenye kinasa sauti cha data za safari ya ndege, Kilipatikana ndani ya saa 28 baada ya maafa ya Alhamisi huko Ahmedabad, ambapo takribani watu 279 walikufa,
Wengi wa waathiriwa hao walikuwa kwenye ndege ya AI171 iliyokuwa ikielekea London Gatwick, Na wote isipokuwa mmoja wao walikufa baada ya ndege hiyo kuanguka kwenye majengo muda mfupi baada ya kushindwa kuruka ipasavyo kutoka uwanja wa ndege wa Ahmedabad.
Simu ya mayday ilitumwa na nahodha wa ndege, Sumeet Sabharwal, sekunde chache baada ya ndege kuondoka kwenye njia ya kurukia.
Bado Hakuna ushahidi au maelezo ambayo yametolewa kutoka kwenye uchunguzi huo, unaoongozwa na maafisa wa India kwa usaidizi kutoka Uingereza na Marekani. Habari Zilizoripotiwa hapo awali ziliangazia hitilafu ya injini na matatizo ya kuruka kwa mabawa na vifaa vya kutua ili kufuatilia sababu za ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani.
Takriban Watu 80 kati ya waliofariki walikuwa wametambuliwa na ndugu zao tayari kufikia Jumapili, kulingana na daktari katika hospitali ya Ahmedabad, Rajnish Patel. "Huu ni mchakato wa kina na wa polepole, kwa hivyo unapaswa kufanywa kwa uangalifu tu," Patel alisema
REPLY HAPA
image quote pre code