Afyaclass Bongo Social WhatsApp kuja na njia ya kutumia Username kuwasiliana



WhatsApp iko mbioni kuanzisha mfumo mpya wa username utakaomruhusu mtumiaji kuwasiliana bila kutumia namba ya simu. Badala yake, watu wataweza kuwasiliana kwa kutumia majina ya watmiaji (usernames), hatua inayolenga kuimarisha faragha na usalama.

Mfumo huu unaweza kurahisisha mawasiliano kati ya watu wasiofahamiana, hasa kwa wale watakaoamua kufanya usernames zao ziwe za wazi kama majukwaa ya mengine ya mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, WhatsApp pia inafanya kazi ya kuongeza ulinzi zaidi kupitia kipengele kipya cha username PIN. Hii itamaanisha mtu hatoweza kukuandikia chochote hadi ajue PIN yako ya siri, hata kama anajua username yako.

Kwa kifupi:

Unaweza kuwasiliana bila kutoa namba ya simu

Username yako ikijulikana, mtu anaweza kukuandikia

Lakini ili kuanzisha mazungumzo, atahitaji kujua PIN yako

Kipengele hiki bado kiko kwenye majaribio (beta) na hakijaanza kutumika kwa watumiaji wote. Lengo ni kuongeza faragha bila kuathiri urahisi wa mawasiliano.

You, Mehreen and others

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD