Mfahamu Kijana aliyerekodi video ya ajali ya Air India ambayo ulimwengu wote uliiona

Mfahamu Kijana aliyerekodi video ya ajali ya Air India ambayo ulimwengu wote uliiona

#1


Kila mara Aryan Asari aliposikia sauti ya ndege, alikuwa akitoka nje ya nyumba kuitafuta.

Kuangalia ndege lilikuwa jambo la kawaida kwake, baba yake Maganbhai Asari alisema.

Aryan alipenda sauti ya mngurumo ya injini iliyojaa hewani na kisha ikaongezeka zaidi ndege ilipokuwa ikipita juu yake, ikiacha nyuma nyuzi za chaki angani.

Alhamisi iliyopita, kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 alikuwa kwenye mtaro wa nyumba ya Bw Asari katika jiji la Ahmedabad, akitengeneza video za ndege, wakati ndege ya Air India Dreamliner 787-8 ilipoanguka mbele ya macho yake na kuwaka moto, na kuwaua 241 waliokuwa ndani. Takribani watu 30 pia walipoteza maisha ardhini.



"Niliiona ndege. Ilikuwa ikishuka na kushuka. Kisha ikayumba na kuanguka mbele ya macho yangu," aliiambia BBC Gujarati katika mahojiano mapema wiki hii.

Video hiyo, ambayo sasa ni kidokezo muhimu kwa wachunguzi wanaojaribu kutafuta chanzo cha ajali hiyo, imezua gumzo kupitia vyombo vya habari na kumweka Aryan , mwanafunzi wa shule ya sekondari katikati ya moja ya majanga mabaya zaidi ya anga katika historia ya nchi.

"Tumejawa na maombi ya mahojiano. Wanahabari wamekuwa wakizunguka nyumba yangu usiku na mchana wakiomba kuzungumza naye," Bw Asari aliambia BBC.

Tukio hilo na lililofuata tangu wakati huo, limekuwa na "athari mbaya" kwa Aryan, ambaye ameumizwa na kile alichokiona. "Mwanangu anaogopa sana hadi ameacha kutumia simu yake," Bw Asari alisema.

REPLY HAPA


image quote pre code