Damu Kutoka Puani ni Nini?
Damu kutoka puani, kitaalamu huitwa epistaxis, ni hali ambapo damu hutoka kupitia tundu za pua. Inaweza kuwa damu kidogo au nyingi, na mara nyingine huweza kuwatisha watu ingawa mara nyingi si hatari.
Chanzo au Visababishi vya Damu Kutoka Puani:
Visababishi vya kawaida ni pamoja na:
- Ukavu wa hewa (hasa wakati wa baridi au kwenye maeneo yenye kiyoyozi).
- Kupiga chafya au kupenga pua kwa nguvu.
- Kukwaruza pua kwa vidole (kuchokonoa).
- Majeraha ya moja kwa moja kwenye pua (mf. kugongwa).
- Kuathirika kwa mishipa midogo ya damu ndani ya pua.
Visababishi vya kiafya au kimatibabu:
- Shinikizo la damu (Presha ya juu).
- Matumizi ya dawa za kupunguza kuganda kwa damu (mf. aspirin, warfarin).
- Allergies au mafua sugu.
- Magonjwa ya damu (kama hemophilia au leukemia).
- Uvujaji wa damu unaosababishwa na vidonda ndani ya pua.
- Matumizi ya dawa za pua kwa muda mrefu (mf. spray za kutibu allergy au mafua n.k).
Dalili Zinazoambatana na tatizo hili:
- Kutoka damu mfululizo kutoka puani.
- Kuhisi kizunguzungu au uchovu iwapo damu ni nyingi.
- Damu kupita puani hadi kooni (haswa kwa posterior nosebleed).
- Maumivu au hisia ya kuchoma ndani ya pua.n.k.
Nini Cha Kufanya Mara Damu Inapotoka Puani (Huduma ya Kwanza):
-
Kaa chini na uinue kichwa kidogo mbele.
Usilalie nyuma – inaweza kufanya damu ishuke koo. -
Bana pua zote mbili kwa vidole kwa dakika 10-15.
Tumia kitambaa au tissue safi. -
Weka barafu au kitu cha baridi kwenye paji la uso au pua.
-
Usipige chafya au kupenga pua kwa nguvu baada ya damu kukoma.
Matibabu na Tiba
Ikiwa una tatizo hili hasa ikiwa ni mara kwa mara,ongea na Wataalam wa afya kwa Msaada Zaidi
AU KWA USHAURI ZAIDI NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Wakati wa Kumwona Daktari:
- Ikiwa damu inaendelea kutoka baada ya dakika 20 za kubana pua.
- Ikiwa damu inatoka mara kwa mara bila sababu.
- Ikiwa unatumia dawa za kupunguza kuganda kwa damu.
- Ikiwa una historia ya ugonjwa wa damu au shinikizo la damu.
- Ikiwa damu inatoka baada ya kuumia kichwani au ajali.n.k.
Jinsi ya Kuzuia Damu Kutoka Puani:
- Epuka kukwangua/kuchokonoa pua.
- Kunywa maji ya kutosha.
- Epuka kupenga pua kwa nguvu sana.
- Tibu vizuri allergy au mafua.
REPLY HAPA
image quote pre code