Sarah aeleza jinsi ambavyo alianza kuona dalili za Ugonjwa wa Mpox

Sarah aeleza jinsi ambavyo alianza kuona dalili za Ugonjwa wa Mpox

#1

Sarah aeleza jinsi ambavyo alianza kuona dalili za Ugonjwa wa Mpox

Ni Sarah huyu, mmoja wa waathiriwa wa ugonjwa huo  katika kaunti ya Mombasa nchini Kenya. Maambukizi ya ugonjwa wa mpox kutokana na aina ya virusi vya monkeypox yalizikumba nchi nyingi barani Afrika. Sara anaeleza dalili  za MPOX   alipoanza kuugua, anasema,

"Mimi nilianza tu kusikia  muwasho baada ya siku mbili nikaona vidonda vimetoka vinatoa maji. Vilianza kutoka  kichwani halafu vikafura  kwenye  shingo, nisingeweza kugeuza  shingo, hivyo  nikaona vidonda vinazidi kuongezeka. Ndipo nikachukua hatua ya kwenda hospitalini, nikaangaliwe  shida nini na baada ya hapo walipata kuwa  ni MPOX  na hapo nikapewa  matibabu."

Na ndipo safari ya Sara kuelekea hospitalini. Alipofika hospitali, alilazwa katika wodi moja iliyoko katika kitua cha kutenga kwa ajili ya wagonjwa wa MPOX, anasema..

“Baada ya kufikishwa pale hospitalini. Tuliwekwa kwa  wodi ya wagonjwa wenye MPOX  kwa ajili ya matibabu. Nilikaa kwa muda wa wiki mbili nikifuata masharti ya daktari na kusafisha na maji ya moto na chumvi. Halafu unapaka dawa  uliyopewa ya maji y, na baada ya hapo unameza vidonge vya maumivu. Madaktari wenyewe walikuwa wanakuja wanatuongelesha wakituambia tusiwe na wasiwasi hapa tumekuja mahali sawa.”

UNICEF  na huduma za Umoja wa Mataifa za maji na usafi wa mazingira, WASH imewasaidia  kuunga mkono Idara ya Afya ya Kaunti ya Mombasa na kwa kushirikiana na Serikali ya Kenya waliweza kujenga uwezo wa wahudumu wa afya na wahamasishaji wa afya ya jamii, wakiwafundisha kuhusu ugonjwa wa MPOX.  Dkt. Mohammed Halif ambaye ni  Mkurugenzi wa Kaunti  ya Mombasa,Huduma za Kliniki za Afya, anasema

“Tangu kulipomgundua mgonjwa wa kwanza, tulianzisha mara moja vituo vya uendeshaji wa dharura za afya ya umma kuhusu usafi wa mazingira na kujisafi, na ninaona imekuwa ni jambo la ukarimu sana kwa UNICEF kuja na kutoa vifaa vya kunawia mikono ambavyo tumevigawa katika wanajamii.”

Sarah baada ya kutibiwa, akapatiwa ushauri ya jinsi ya kutangamana na wengine.

“Tuliambiwa kwamba ukishatoka nje mwepukane na mambo  ya ngono sana na pili mambo ya kushikana shikana. Vile nilitoka hospitalini, nilipewa mtungi wa maji na sabuni mche mzima nikaambiwa Mtungi utakuwa  wakuchotea  maji toka mtoni   na kuoga mzuri, usafi uendelee.”

UNICEF imeendelea kuunga mkono hospitali na pia kufanya uhamasishaji ndani ya jamii ili kuhakikisha kwamba visa vitakavyotokea siku za usoni vitashughulikiwa kwa wakati.

Sarah anatamatisha na furaha akisema familia yake pia wamejawa na furaha baada ya kupona, anasema…

“Niliporudi nyumbani watoto walifurahi sana kuniona. Saa hii nafurahia sana, nashukuru napata usingizi, nalala na najihisi niko sawa zaidi sina yale maumivu nilikuwa nayo.”

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code