Ongeza kumtafuta Mungu 2026,hii ndyo akili ya kutoka

Ongeza kumtafuta Mungu 2026,hii ndyo akili ya kutoka

#1

Ongeza kumtafuta Mungu 2026,hii ndyo akili ya kutoka

Mtu anayemtafuta Mungu ndye mwenye akili kuliko wote, Lakini Shetani hupofusha Fikra za Watu kwa nguvu Zote ili waone kumtafuta Mungu ni kupoteza muda,Kukosa cha kufanya,Kuwa Maskini n.k..

"Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu(Zaburi 14:2)".

Fikra Zako zifunguke Katika Jina la Yesu,Uuone Ukuu wa MUNGU kuliko ngome za mawazo anazojenga adui kwenye fikra zako, angusha ngome hizo,Na Mungu aweke Kiu ndani yako ya kumtafuta kwenye Kila Jambo.

Aweke Kiu kama ya Daudi,anasema katika Zaburi 27:4 "Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake".

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code