Imani Dia Smith Muigizaji wa Disney The Lion King afariki dunia nyumbani kwake

Imani Dia Smith Muigizaji wa Disney The Lion King afariki dunia nyumbani kwake

#1

Imani Dia Smith, anayejulikana zaidi kwa kuigiza nafasi ya Young Nala kwenye filamu ya Disney The Lion King, amefariki dunia katika tukio linalochunguzwa kama mauaji.

Kwa mujibu wa polisi, mwili wake ulipatikana Desemba 21, 2025 nyumbani kwake mjini Edison, New Jersey, baada ya mamlaka kuitikia wito wa dharura. Alikimbizwa hospitalini lakini alithibitishwa kufariki dunia muda mfupi baadaye. Wakati wa kifo chake, Smith alikuwa na miaka 25.

Polisi wamemtaja mpenzi wake, Jordan D. Jackson-Small (miaka 35), kama mshukiwa mkuu katika tukio hilo, na tayari amekamatwa kwa ajili ya hatua za kisheria huku uchunguzi ukiendelea.

Kifo cha Imani Dia Smith kimeacha majonzi makubwa kwa familia, mashabiki na jamii, wengi wakimkumbuka kama msanii mwenye kipaji kikubwa, mwenye ndoto na maono muhimu aliyoanza tangu akiwa mtoto jukwaani Broadway.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code