Showing posts with label Jukwaa la Historia. Show all posts
Showing posts with label Jukwaa la Historia. Show all posts

Howard Tucker,daktari mzee zaidi kuwahi kufanya kazi dunianiAfyaclass Forum •

Howard Tucker,daktari mzee zaidi kuwahi kufanya kazi duniani

Daktari wa Marekani, Howard Tucker, ametunukiwa rasmi rekodi ya Dunia ya Guinness (Guinness World Records) kama daktari mzee zaidi kuwahi kufanya kazi duniani, baada ya kuendelea na taaluma yake hadi akiwa na umri wa miaka 103.

Tucker, ambaye amekua mtaalamu wa magonjwa ya neva (neurologist), aliendelea kuwahudumia Wagonjwa wake kwa bidii hadi miezi miwili tu kabla ya kufariki dunia tarehe 22 Desemba 2025, uvumilivu wake kazini umevutia watu wengi duniani, ukionyesha kuwa umri si kikwazo kwa kujituma na kujitoa.

Kwa mujibu wa taarifa, maisha yake yalijikita katika taaluma ya tiba kwa zaidi ya miongo kadhaa, akihudumia jamii na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Sekta ya Afya.

Hadithi ya maisha yake sasa inaelezwa zaidi kupitia Mjukii wake, ikilenga kuhamasisha vizazi vijavyo kuhusu umuhimu wa kujituma, kujifunza na kufanya kazi kwa moyo wote hadi uzeeni.

0 Comment

Mariam Nabatanzi Mwanamke kutoka Uganda Aliyepata Watoto 44Afyaclass Forum •

Mariam, kutoka wilaya ya Mukono, Uganda, alijifungua watoto 44 kufikia umri wa miaka 36!



SABABU YA AJABU:

Madaktari waligundua ana hali ya kipekee ya vinasaba (genetic condition) inayosababisha kutoa mayai mengi kwa wakati mmoja (hyperovulation).

Alianza kuzaa akiwa na umri wa miaka 12.

Alichopata: Mapacha 6 mara 5, mapacha 4 mara 4, na mapacha 3 mara 3, pamoja na watoto wachache wa mmoja mmoja.

Aliomba kufanyiwa upasuaji wa uzazi kuzuia kupata watoto zaidi, lakini alichelewa kusaidiwa.

0 Comment

Kisa cha kushangaza Dunia, Lina Medina – Mtoto wa Miaka 5 Aliyepata Mimba na KujifunguaAfyaclass Forum •

Lina Medina alipelekwa hospitali na wazazi wake wakidhani ana uvimbe tumboni. Lakini baada ya vipimo, madaktari waligundua kitu kisichotarajiwa kabisa: alikuwa na mimba ya miezi saba!



Lina alijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji (Caesarean section) akiwa na umri wa miaka 5 na miezi 7 tu, na mpaka leo ndiye msichana mdogo zaidi kuwahi kupata mimba na kujifungua katika historia ya binadamu.

Sababu ya Kushangaza:

Lina alikuwa na hali nadra sana ya kiafya inayoitwa "precocious puberty", ambapo mtoto anapitia mabadiliko ya kubalehe akiwa bado mdogo sana – Lina alianza hedhi akiwa na miezi 8!

Hakujulikana wazi nani aliyemsababishia mimba, lakini baba yake alishikiliwa kwa muda na baadaye kuachwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi.



🌍 Umuhimu katika historia ya afya:

Kisa hiki kilithibitisha kuwa ubalehe wa mapema sana unaweza kutokea, hata kama ni nadra mno.

Pia kilisababisha mijadala mikali kuhusu haki za watoto, maadili, na udhibiti wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto.

👶📌 Baada ya Tukio:

Mtoto aliyezaliwa aliitwa Gerardo Medina, aliishi mpaka akiwa na miaka 40 kabla ya kufariki kwa ugonjwa wa uboho.

Lina Medina hakuwahi kusema hadharani kuhusu kisa chake. Alikataa mahojiano yote kwa miaka mingi.

0 Comment

Mtoto Azaliwa ndani ya Ndege na kupewa tiketi ya bure ya Kusafiri ndani ya ndege Maisha yake yoteAfyaclass Forum •

Mwaka 2022 Mwanamke mmoja raia wa Yemen, Hiyam Nasr Naji Daaban, alijifungua akiwa ndani ya ndege ya EgyptAir iliyokuwa ikisafiri kutoka London kuelekea Cairo mnamo Septemba 16. Akiwa angani katika anga la Ujerumani, Daaban alianza uchungu wa uzazi na rubani akaomba kibali cha kutua kwa dharura mjini Munich, lakini mama huyo alijifungua kabla ya ndege kutua. 



Baada ya tukio hilo, kampuni ya EgyptAir ilitangaza kumpa mtoto huyo tiketi ya kusafiri bure maisha yake yote kwa ndege zao kama zawadi maalum. Picha ya mtoto huyo pamoja na salamu za pongezi kwa mama Daaban na mwenyekiti wa EgyptAir, Rushdi Zakaria, zilitumwa kupitia Twitter ya kampuni hiyo. 

Tukio hili linafuatia matukio mengine ya watoto kuzaliwa angani, ikiwemo mtoto aliyezaliwa ndani ya ndege ya Jet Airways mwaka 2017 na kupewa tiketi ya maisha, huku baadhi ya mashirika mengine kama Emirates yakiwa hayajatoa zawadi kama hiyo kwa watoto waliozaliwa katika ndege zao.

0 Comment

Sikukuu ya sabasaba,Historia ya sikukuu ya sabasabaAfyaclass Forum •

SabaSaba ni sikukuu katika nchi ya Tanzania inayoadhimishwa tarehe saba, mwezi wa saba (7 Julai) ambayo lengo lake ilibadilishwa kutokana na mabadiliko ya historia na siasa.



Asili ya Saba Saba ilikuwa kuundwa kwa chama cha Tanganyika African National Union (TANU) kwenye tarehe 7 Julai ya mwaka 1954. Chama hiki kiliongozwa na Julius Nyerere kikawa chama tawala wakati wa uhuru wa Tanganyika kilichoendelea kuongoza siasa ya nchi baada ya kushika viti vyote vya bunge.

Mwaka 1963 Nyerere pamoja na uongozi wa chama waliamua kupeleka nchi kwenye mfumo wa chama kimoja kisheria. Hivyo mwaka 1964 siku ya kuzaliwa kwa chama yaani "Saba Saba Day" iliorodheshwa katika sheria ya sikukuu za umma (Public Holidays Ordinance Act)[1].

Tangu mwaka 1967 TANU ilitangaza itikadi ya Ujamaa kama siasa rasmi na hapo ilitumia mara nyingi lugha ya kukazia "wakulima na wanfayakazi" jinsi ilivyokuwa kawaida katika vyama vilivyofuata itikadi ya usoshalisti duniani. Hivyo sikukuu ya chama ya Saba Saba iliadhimishwa pia kama "sikukuu ya wakulima na wafanyakazi". Mtindo huu uliendelea kutumiwa pia baada ya mwaka 1977 ambako TANU iliungana na Chama cha Afro-Shirazi (ASP) cha Zanzibar kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Baada ya muungano wa TANU na ASP kuwa CCM sikukuu ikaitwa mara ningi "siku ya wakulima" kwa kufuatana na wito wa kisiasa "Siasa ni Kilimo" uliokazia maendeleo ya taifa kwa njia ya kuboresha kilimo nchini.

Saba Saba ilikuwa sikukuu ya umma maana yake ofisi za serikali na makampuni, maduka makubwa na shule zote zilifungwa. Katika miji yenye makao makuu ya mkoa na mara nyingi pia penye makao makuu ya wilaya kulikuwa na maonyesho, wakati mwingine pamoja na mikutano ya hadhara ambako watu walisikia hotuba za viongozi wa chama na serikali. 

Kwenye maonyesho kulikuwa na mazao, mifugo na bidhaa za tasnia za eneo pamoja na bidhaa nyingine. Miji mingi nchini Tanzania huwa na maeneo ya Saba Saba (Saba Saba Grounds). Sherehe zilitokea hadi ngazi ya kijiji.

Kati ya maonyesho haya ni hasa Maonyesho ya Saba Saba ya Dar es Salaam (Dar es Salaam International Trade Fair, Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam) ambayo ni maarufu kama tukio la kitaifa na la kimataifa inayoendelea kuvuta wageni wengi hadi leo[2].

Via:Wikipedia.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD