Showing posts with label Jukwaa la Sheria. Show all posts
Showing posts with label Jukwaa la Sheria. Show all posts

Baltasar ahakumiwa miaka 8 gerezani kwa kosa la ubadhirifu wa Fedha za Umma Afyaclass Forum •

Baltasar ahakumiwa miaka 8 gerezani kwa kosa la ubadhirifu wa Fedha za Umma 



Mahakama ya Mkoa wa Bioko nchini Equatorial Guinea imemhukumu Baltasar Ebang Engonga, Mkuu wa zamani wa Shirika la Taifa la Upelelezi wa Masuala ya Kifedha (NFIA), kifungo cha miaka Minane Jela kwa kosa la ubadhirifu wa Fedha za Umma na kujipatia mali kinyume cha sheria.

Engonga, pamoja na Maafisa wengine Watano waandamizi, walipatikana na hatia ya kuiba mamia ya maelfu ya dola kutoka hazina ya taifa na kutumia fedha hizo kwa maslahi yao binafsi.

Mahakama pia imewaamuru kulipa faini kubwa. Engonga atakuwa na faini ya dola 220,000, wakati maafisa wengine walioshitakiwa kama washirika walipata kifungo cha miaka mitatu.

Baltasar Ebang Engonga ni Mpwa wa Rais Teodoro Obiang Nguema, ambaye amekaa madarakani tangu 1979 na ana umri wa miaka 82, Engonga alikuwa mmoja wa wale wanaodhaniwa kuwa na nafasi ya kurithi madaraka ya Rais. 

Hukumu hii inaashiria changamoto kubwa za uwajibikaji wa viongozi serikalini, hasa katika nchi yenye utajiri wa mafuta lakini pia changamoto za ubadhirifu wa kifedha.

Mbali na mashtaka ya kifedha, Engonga amejipatia umaarufu wa aibu baada ya video kadhaa za ngono kuenea mitandaoni, Video hizo zinamhusisha akiwa na wake wa maafisa wengine wa serikali.

0 Comment

P Diddy akutwa na hatia dhidi ya Makosa mawiliAfyaclass Forum •

Jopo la majaji limefikia uamuzi wa makosa yote matano ya Sean "Diddy" Combs.



Wakiwa katika chumba cha mahakama majaji walitaja mashtaka na hukumu zake.

Kwa muhtasari wa kile tulichosikia mahakamani, ni mchanganyiko wa hukumu za hatia na zisizo na hatia:

Kosa la njama za ulaghai: hana hatia

Ulanguzi wa ngono wa Cassie Ventura: hana hatia

Usafirishaji wa ukahaba wa Ventura na wengine: ana hatia

Ulanguzi wa ngono wa mwanamke anayejulikana kama "Jane": hana hatia

Usafirishaji kwa ajili ya ukahaba wa "Jane" na wengine: ana hatia

Majaji walichukua saa 13 kufikia uamuzi

Kwa jumla, majaji walijadili kwa saa 13 kwa siku tatu ili kufikia uamuzi wa pamoja juu ya mashtaka dhidi ya Combs.

Kesi hiyo imekuwa ikifanyika huko New York tangu mwezi Mei. Muda mwingi wa mahakama hiyo ulilenga kesi ya mwendesha mashtaka.

Upande wa utetezi unataka Combs aachiliwe kwa dhamana

Timu ya wanasheria na wakili wa Combs, Marc Agnifilo ameomba mteja wake aachiliwe kutoka kizuizini.

Amekuwa gerezani tangu alipokamatwa Septemba mwaka jana.

Agnifilo anapendekeza dhamanai ya $1m.

0 Comment

Hatma ya Msanii Diddy kujulikana hivi karibuniAfyaclass Forum •

Juni  23,2025 upande wa mashtaka ulipeleka shahidi wa 34 na wa mwisho ambaye ni Afisa Maalum wa Usalama wa Ndani Joseph Cerciello, ambaye ushuhuda wake uliangazia siku 28 kutoka mwanzo wa kesi mpaka sasa.



Marekani. Mahakama ya jijini Manhattan imeendelea na kesi ya Sean “Diddy” Combs ambapo kwa sasa inaelezwa kesi hiyo ipo ukingoni huku hatma ya rapa huyo kujulikana hivi karibuni.

Juni  23,2025 upande wa mashtaka ulipeleka shahidi wa 34 na wa mwisho ambaye ni Afisa Maalum wa Usalama wa Ndani Joseph Cerciello, ambaye ushuhuda wake uliangazia siku 28 kutoka mwanzo wa kesi mpaka sasa.

Katika ushahidi wake Afisa Cerciello alieleza kuwa uchunguzi ulionesha mifumo yote ambayo Diddy alikuwa akiitumia kusafirisha wanawake kwa ajili ya biashara za kingono akitumia ushawishi wake katika muziki ili kudhibiti wanawake hao.

Aidha Cerciello alionesha rekodi za safari, mawasiliano ya kidigitali, video na mashahidi waliolazimisha kushiriki kwenye matukio ya kingono.

Katika siku hiyo hiyo tukio jingine ambalo liliwashangaza wengi ni baada ya mawakili wa Diddy akiongozwa na Marc Agnifilo kutangaza kutokuwa na mpango wa kupeleka mashahidi kwa ajili ya kumtetea rapa huyo.

Utakumbuka wiki iliyopita mawakili hao walipanga kupeleka mashahidi watatu akiwemo Diddy mwenyewe, msaidizi wa Combs Enterprises pamoja na mtaalamu wa saikolojia. Hata hivyo kwa mujibu wa mwanasheria mstaafu Mark Chutkow ameeleza kuwa uamuzi huo ni wa busara kwani utaepusha maswali yatakayo mchanganya Diddy.

Hata hivyo baada ya ushahidi kukamilika Juni 26 viongozi wa pande zote watatoa hoja zao za mwisho, kisha wajumbe wa mahakama ya kisheria wataanza mjadala wa mwisho na uamuzi wa hatima ya kesi hiyo. Kwa sasa, Diddy amekana mashtaka yote huku akikataliwa dhamana mara tatu kutokana na hofu ya kuwahonga mashahidi.

Baadhi ya mashahidi wa muhimu waliotoa ushahidi wa kuathiriwa na matukio ya kingono ni pamoja na wapenzi wa zamani wa Diddy, Jane na Cassie huku wengine ni pamoja na rapa Kid Cudi, mlinzi wa nyumbani kwa Diddy, Mia, Capricorn Clark, Kerry Morgan, Bryana Bongolan na wengineo.

Diddy anakabiliwa na mashtaka ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, njama ya kihalifu (racketeering) na usafirishaji kwa lengo la kushiriki katika ukahaba. Licha ya kukana mashtaka yote. Endapo rapa huyo atapatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York na kupelekwa moja kwa moja katika gereza la Metropolitan huko Brooklyn. Kesi yake ilianza kusikilizwa Mei 5,2025.

0 Comment

Jaji Masaju ateuliwa kuwa Jaji Mkuu kuchukua nafasi ya Profesa IbrahimAfyaclass Forum •

Jaji Masaju ateuliwa kuwa Jaji Mkuu kuchukua nafasi ya Profesa Ibrahim



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, George Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

Jaji Masaju anachukua nafasi ya Jaji Profesa Ibrahim Juma ambaye amestaafu rasmi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari leo Ijumaa, Juni 13, 2025, Jaji Masaju ataapishwa Juni 15, 2025 katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Masaju amewahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pia, aliwahi kuwa mshauri wa masuala ya kisheria wa Rais mstaafu wa awamu wa nne, Jakaya Kikwete.

0 Comment

Peter Nwachukwu, mume wa mwimbaji maarufu wa injili Osinachi, ahukumiwa kifo kwa kunyongwa Afyaclass Forum •

Peter Nwachukwu, mume wa mwimbaji maarufu wa injili Osinachi, ahukumiwa kifo kwa kunyongwa 



NIGERIA: Mahakama Kuu huko Abuja amemhukumu Peter Nwachukwu, mume wa mwimbaji maarufu wa injili Osinachi, kifo kwa kunyongwa kwa kupatikana na hatia ya mauaji.

Hukumu hiyo, iliyotolewa na Jaji Nwosu-iheme, inatolewa miaka mitatu baada ya kifo cha Osinachi kilichotokea mnamo Aprili 8, 2022.

Kesi hiyo imevutia Watu wengi kwa sababu ya umaarufu wa Osinachi katika muziki wa injili wa Nigeria na jamii ya Wakristo.

Polisi walikuwa wamemkamata Bwana Nwachukwu baada ya mkewe, kufariki akiwa katika hospitali moja huko Abuja.

Ripoti za awali zilikuwa zimependekeza kwamba mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 42 alikuwa mgonjwa wa saratani ya koo, lakini familia yake ilikataa na kudai kwamba alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani.

Walimshutumu mumewe kwa unyanyasajina kusababisha kifo cha mke wake.

Baadaye mahakama iliamuru kwamba arudishwe kizuizini gerezani. Bwana Peter Nwachukwu alishtumiwa kwa "vitendo vya vurugu na kumshambulia mkewe na ufahamu kuwa kifo hicho kitakuwa ni matokeo ya matendo yake."

Mashahidi 17, pamoja na watoto wawili, waliitwa na upande wa mashtaka wakati wa kesi hiyo. Hati 25 pia zilitolewa kama kithibitisho mbele ya mahakama.

Marehemu Osinachi na mume wake aliyehukumiwa Peter Nwachukwu walijaaliwa watoto wanne.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD