Jopo la majaji limefikia uamuzi wa makosa yote matano ya Sean "Diddy" Combs.
Wakiwa katika chumba cha mahakama majaji walitaja mashtaka na hukumu zake.
Kwa muhtasari wa kile tulichosikia mahakamani, ni mchanganyiko wa hukumu za hatia na zisizo na hatia:
Kosa la njama za ulaghai: hana hatia
Ulanguzi wa ngono wa Cassie Ventura: hana hatia
Usafirishaji wa ukahaba wa Ventura na wengine: ana hatia
Ulanguzi wa ngono wa mwanamke anayejulikana kama "Jane": hana hatia
Usafirishaji kwa ajili ya ukahaba wa "Jane" na wengine: ana hatia
Majaji walichukua saa 13 kufikia uamuzi
Kwa jumla, majaji walijadili kwa saa 13 kwa siku tatu ili kufikia uamuzi wa pamoja juu ya mashtaka dhidi ya Combs.
Kesi hiyo imekuwa ikifanyika huko New York tangu mwezi Mei. Muda mwingi wa mahakama hiyo ulilenga kesi ya mwendesha mashtaka.
Upande wa utetezi unataka Combs aachiliwe kwa dhamana
Timu ya wanasheria na wakili wa Combs, Marc Agnifilo ameomba mteja wake aachiliwe kutoka kizuizini.
Amekuwa gerezani tangu alipokamatwa Septemba mwaka jana.
Agnifilo anapendekeza dhamanai ya $1m.
REPLY HAPA
image quote pre code