Showing posts with label Miguel Uribe. Show all posts
Showing posts with label Miguel Uribe. Show all posts

Mgombea Urais Afariki dunia Colombia:Miguel Uribe Afyaclass Forum •

Mgombea Urais Afariki dunia Colombia



BOGOTA, COLOMBIA : MGOMBEA  Urais wa Colombia, Miguel Uribe, amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumanne, miezi miwili baada ya kushambuliwa kwa risasi alipokuwa kwenye kampeni za uchaguzi.

Licha ya kuonyesha dalili za kupona katika wiki za hivi karibuni, madaktari walibainisha kuwa mwanasiasa huyo alianza kuvuja damu kwenye ubongo siku ya Jumamosi, hali iliyosababisha kifo chake.

Uribe, aliyekuwa na umri wa miaka 39 na Seneta wa chama cha kihafidhina, alipigwa risasi kichwani na mguuni Juni 7, 2025, wakati akihutubia mkutano wa hadhara jijini Bogota.

Jeshi la polisi limesema watu sita wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo, akiwemo mshambuliaji kijana mwenye umri wa miaka 15.

Kifo cha Uribe, ambaye alitarajiwa kupambana na  Rais Gustavo Petro katika uchaguzi wa mwaka ujao, kimezua hofu ya kurejea kwa Colombia katika wimbi la ghasia za kisiasa.

Chanzo: DW 

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD