Kumkabidhi BWANA maisha yako;ni kumpa BWANA au MUNGU nafasi ya kuwa Mwamuzi na Kiongozi wa Kila Kitu kwenye maisha yako.
Hii ina maana huwezi kufanya kitu chochote pasipo kutaka uongozi kutoka kwa Mungu, bila kujali una uzoefu kiasi gani,Elimu kiwango gani,Kipato kiwango gani, au akili kiwango gani... Mungu anaamua na kukuongoza kwa kila kitu.
Zaburi 37:5 Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.
Mithali 3:5-6Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.









image quote pre code