Showing posts with label UNICEF. Show all posts
Showing posts with label UNICEF. Show all posts

Takribani watu 2,000 wamekufa kwa kipindupindu Congo tangu Januari - UNICEFAfyaclass Forum •


Maelezo ya picha,Mchimbaji madini akiwekewa dripu katika kituo cha matibabu ya kipindupindu kinachoendeshwa na Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) kufuatia mlipuko wa kipindupindu ambao umeelemea mfumo dhaifu wa afya.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inapambana na mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 25 ambao umeua takriban watu 2,000 tangu Januari, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto limesema Jumatatu.

Katika kisa kimoja, robo ya watoto katika kituo cha watoto yatima cha Kinshasa - 16 kati ya 62 - walikufa siku chache baada ya ugonjwa huo kuenea, UNICEF iliongeza.

Kipindupindu ni ugonjwa mbaya wa kuhara unaoweza kusababisha kifo ambao huenea haraka wakati maji taka na maji ya kunywa ambayo ni machafu.

Mamlaka ya afya ya Afrika mwezi uliopita ilitoa tahadhari kuhusu kuongezeka kwa ugonjwa huo nchini Angola, Burundi na maeneo mengine ya bara, na ongezeko la jumla la 30% la kesi zilizorekodiwa mwaka jana.

Nchini Congo, ukosefu wa maji safi umezidisha ugonjwa huo, na ufadhili zaidi unahitajika kwa ajili ya usafi wa mazingira, usafi na huduma za afya, imesema UNICEF.

Tangu Januari, mamlaka imerekodi kesi 64,427 na vifo 1,888, ikiwa ni pamoja na maambukizi 14,818 na vifo 340 miongoni mwa watoto, UNICEF ilisema. Mikoa 17 kati ya 26 ya nchi hiyo kwa sasa imeathiriwa, shirika hilo liliongeza.

Ni asilimia 43 tu ya watu nchini Congo wanapata huduma za msingi za maji, kiwango cha chini kabisa barani Afrika, na ni asilimia 15 pekee wanaotumia huduma za usafi wa mazingira, kulingana na taarifa hiyo.

Serikali ina mpango wa kutokomeza kipindupindu na bajeti inayopendekezwa ya dola milioni 192, lakini hiyo inasalia kuwa na ufadhili mdogo, imesema UNICEF.

UNICEF inaomba takriban dola milioni 6 mwaka 2026 ili kuendeleza kazi yake.

"Bila ya fedha za ziada na hatua zilizoratibiwa, maisha mengi zaidi yanaweza kupotea," amesema msemaji wa UNICEF, John Agbor.

0 Comment

Duru ya kampeni ya dharura ya chanjo ya polio yaanza huko GazaAfyaclass Forum •

Chanjo Gaza: WHO, UNICEF na UNRWA waanza uchanjaji zaidi ya watoto 44,000

Mashirika ya Umoja wa Mataifa WHO, UNICEF na UNRWA wameanzisha kampeni ya pamoja ya Uchanjaji watoto waliokosa huduma muhimu za kuokoa maisha kutokana na miaka miwili ya machafuko katika Ukanda wa Gaza umeanza kutekelezwa na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, lile la afya duniani, la kuhudumia watoto UNICEF na la kusaidia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA. 

Kampeni hii inayowalenga watoto kuanzia siku moja hadi miaka mitatu, imeanza majuzi tarehe 10 mwezi huu wa Novemba na itaendelea hadi tarehe 18 Novemba. Utoaji wa huduma hizi muhimu za afya kwa maelfu ya watoto unategemea kuheshimiwa kwa usitishaji mapigano kuhakikisha familia, wataalamu wa afya na wahudumu wa kibinadamu wanaweza kufika katika vituo vya chanjo kwa uhuru na usalama.

Video inaanzia katika Kituo cha Afya cha Al-Daraj kilichoko Gaza City, Palestina. Wazazi  wanaume kwa wanawake  wakiwa na watoto wao wamefurika kituoni hapo, wakihudumiwa na wahudumu wa afya kabla ya kupata chanjo.

Refqa Skaik, Afisa wa Kiufundi wa Polio katika WHO, anasema, “kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, UNICEF, Jumuiya Mwezi Mwekundu ya Palestina na sisi WHO, tunatoa utaalamu na msaada wa kiufundi katika utekelezaji wa kampeni hii, hususan kwa kundi la watoto walio chini ya miaka mitatu, wanaokadiriwa kufikia watoto 44,900.”

0 Comment

Dhana Potofu kuhusu kunyonyesha,Wiki ya UnyonyeshajiAfyaclass Forum •

Takwimu za hivi karibuni za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, zinakadiria kuwa unyonyeshaji usio wa kutosha husababisha asilimia 16 ya vifo vya watoto kila mwaka.



Shirika la Afya Duniani (WHO) linahimiza akina mama kuungwa mkono na jamii, familia, na wahudumu wa afya wakati wa kunyonyesha.

Kwa kuunda mifumo rafiki ya unyonyeshaji, na kuheshimu haki ya wanawake ya kunyonyesha wakati wowote, mahali popote, na kukuza usaidizi wa kijamii.

Wiki ya Unyonyeshaji Duniani hufanyika katika wiki ya kwanza ya Agosti kila mwaka.

Lakini bado kuna imani potofu kuhusu unyonyeshaji, ambazo zinaweza kuwazuia wanawake kunyonyesha. 

Titi kuuma sio jambo la kawaida

Kwa siku za awali ni kawaida ziwa kuuma kabla hujazoea. Lakini kunyonyesha hakupaswi kuumiza au kusababisha maumivu makali.

Kuuma kwa chuchu inaweza kuwa ni dalili ya maambukizi au mtoto hanyonyi jinsi ambavyo inatakiwa. Maumivu madogo ya awali ni kawaida, haswa kwa akina mama wanaoanza kuzoea kunyonyesha.

Subiria kabla ya kunyonyesha

Jambo lolote linalohimiza akina mama kunyonyesha ni zuri kwa afya ya binadamu. Hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba mama anapaswa kuvuta muda kabla ya kuanza kunyonyesha baada ya kujifungua.

Kizuizi chochote cha kunyonyesha baada ya kujifungua hakina mashiko ya kisayansi. Na kuna faida nyingi za mtoto kunyonya mara tu baada ya kujifungua.

Kunyonyesha ni lishe kwa mtoto. Pia husaidia kusinyaa kwa mfuko wa uzazi, na kusaidia kuzuia au kupunguza kasi ya kutoka kwa damu baada ya kujifungua.

Pia, katika siku chache za kwanza baada ya kujifungua, mwili wa binadamu hutoa protini maalumu inayoitwa kolostramu, ambayo hufanya maziwa kuzalishwa.

Huwezi kutumia dawa yoyote ikiwa unanyonyesha

Hilo huwa ni swali la kwanza kwa mama popote duniani. Je, dawa yoyote ni salama kwa mtoto wangu?

Ukweli ni kwamba dawa nyingi humfikia mtoto katika kiwango cha chini sana. Ikiwa daktari anasema unahitaji dawa, uliza maswali yako lakini kuna uwezekano mkubwa kuwa dawa hiyo ni salama kutumia.

Kile ambacho mtoto anahitaji zaidi ya yote ni mama mwenye afya. Dawa nyingi zinazoshughulikia maambukizi, uchovu au maumivu zinaweza kuwa salama.

Na dawa ambazo hazipaswi kutumiwa wakati wa kunyonyesha, ni chache sana. Mara nyingi ni kwa ajili ya matibabu ya hali mbaya sana za Kiafya kama vile saratani.

Kuna dawa zingine ambazo unatakiwa kutumia kwa uangalifu kwa kuzingatia hatari na faida. Mwanamke yeyote ambaye anapewa dawa wakati wa kunyonyesha anapaswa kumuuliza daktari maswali.

Mfano dawa za mafua, kupiga chafya au koo kuwasha, ambazo zinafungua mishipa - hizi zinaweza kupunguza mtiririko wa maziwa.

Pia kuwa mwangalifu na dawa za mitishamba kwa sababu huwezi kujua zina nini ndani yake, na nyingi ya dawa hizo hazijafanyiwa utafiti wa kina.

Epuka chakula chenye viungo

Hakuna kitu ambacho mama hapaswi kula anaponyonyesha. Lakini maziwa ya mama yanaweza kuathiriwa na ulaji wako.

Kwa mfano, niligundua nikinywa juisi ya matunda ya jamii ya machungwa, mtoto wangu huwa na hasira sana.

Wakati mwingine unaweza kugundua tabia za mtoto wako kwa chakula ambacho umekula. Lakini hakuna kitu ambacho kinamdhuru au sio sahihi kiafya na ambacho kinahitaji kuepukwa.

Usitumie maziwa ya unga kama unanyonyesha

Mwili wa mwanamke umeumbwa kuwa na uwezo wa kutoa maziwa ya kutosha kwa mtoto wako. Mtoto anaponyonya chuchu, huchochea homoni kutoa kiasi kinachohitajika cha maziwa.

Kwa hivyo, ikiwa unanyonyesha mtoto mdogo, mkubwa au hata mapacha, mwili wako utatoa maziwa ya kutosha.

Ukianza kumpa maziwa ya unga, homoni zitajizuia. Mwili wako hautopata ishara za kutosha kwamba mtoto anahitaji maziwa zaidi.

Ikiwa unakabiliwa na tatizo la uhaba wa maziwa na ukaanza kumpa mtoto maziwa ya kopo, hilo linaweza kukupa nafuu ya muda mfupi, lakini tatizo la uhaba wa maziwa linaweza kuwa kubwa.

Kwa upande mwingine, ikiwa umechoka usiku au ni mgonjwa na mpenzi wako anampa mtoto maziwa ya unga ili apumzike, hiyo haimaanishi huwezi kunyonyesha. Kwa hivyo maziwa ya unga sio jambo baya, lakini yanaweza yasiwe na msaada mzuri.

Usinyonyeshe ukiwa mgonjwa

Hapana, hiyo ni imani potofu. Hali pekee ambayo mtu anapaswa kupata Ushauri wa kina kabla ya kunyonyesha ni ikiwa ana VVU au homa ya manjano. Virusi hivyo vinaweza kupita kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Akina mama wanapokuwa wagonjwa miili yao hutoa kingamwili ambazo pia hulinda watoto wao wachanga. Ni nadra sana kuona ugonjwa wa mama anaenyonyesha ukimpata mtoto.

0 Comment

Watoto wengi zaidi kufa kwa Utapiamlo na ukimbizi Sudan kuliko hata vita yenyewe: UNICEFAfyaclass Forum •

Watoto wengi zaidi kufa kwa Utapiamlo na ukimbizi Sudan kuliko hata vita yenyewe: UNICEF

Vita nchini Sudan ikitimu siku 300 hii leo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema bila rasilimali za kutosha, na njia za kusambaza misaada ya kiutu kuwa wazi, watoto wengi zaidi watakufa nchini humo kutokana na utapiamlo na magonjwa kuliko hata  kutokana na vita yenyewe.

Shirika hilo kupitia taarifa yake iliyotolewa leo huko Port Sudan nchini Sudan linasema kwa sasa utapiamlo umesambaa nchini humo, ukimbizi wa ndani ni mkubwa kuliko eneo lolote duniani na mfumo wa afya umesambaratika na hivyo vigezo hivyo kutishia kuwa sababu ya vifo miongoni mwa watoto kuliko vita yenyewe.

UNICEF inasema inaona viwango vya juu vya matibabu dhidi ya unyafuzi au utapiamlo uliokithiri kwenye maeneo yanayoweza kufikiwa na misaada ya kiutu, na kwamba kwenye maeneo yasiyofikika kutokana na mazingira ya mapigano hali inaweza kuwa mbaya zaidi.

Takribani watoto milioni 3.5 wanatarajiwa kukumbwa na unyafuzi mwaka huu, wakiwemo zaidi ya 700,000 ambao wanatarajiwa kukumbwa na unyafuzi mkali zaidi na hivyo kuhitaji tiba kamilifu ya kuokoa maisha yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell akinukuliwa kwenye taarifa hiyo amesema mchanganyiko hatari wa utapiamlo, ukimbizi na magonjwa unaongezeka kila siku na kwamba “tuna muda mdogo sana kuzuia vifo.”

Wanawake na watoto waliokimbia makazi yao katika eneo la Wakimbizi wa Ndani huko Darfur Magharibi kutokana na mapigano nchini Sudan.

Amesema “tunahitaji njia salama, endelevu na ha uhakika ya kufikisha misaada ya kiutu huko kwenye mapigano na mipakani na tunahitaij msaada wa kimataifa ili kuweza kuendeleza huduma na mifumo ambayo watoto wanategemea ili waweze kuishi.”

Ameongeza kuwa “hatuwezi kuwatelekeza watoto wa Sudan. Bila hatua ya dharura Sudan inaweza kuwa na janga la kizazi na zaidi ya yote, watoto wa Sudan wanahitaji sitisho la mapigano na amani.”

Maeneo ambako UNICEF inataka kufikia zaidi ni Darfur ambayo imeshuhudia mapigano makali zaidi na sasa ina wakimbizi zaidi ya theluthi moja ya watu wote milioni 8 waliofurushwa makwao tangu kuanza kwa mapigano Aprili mwaka jana.

UNICEF inasema inahitaji dola milioni 840 kufikia watu milioni 9.9 wakiwemo watoto milioni 7.6 walioko hatarini zaidi. Hadi sasa UNICEF imepokea asilimia 28 tu ya fedha hizo.

Source: UNICEF

Soma Zaidi hapa kuhusu tatizo la Utapiamlo,Chanzo,dalili na Tiba

Watoto wengi zaidi kufa kwa Utapiamlo na ukimbizi Sudan kuliko hata
vita yenyewe: UNICEF
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD