Takribani watu 2,000 wamekufa kwa kipindupindu Congo tangu Januari - UNICEF

Takribani watu 2,000 wamekufa kwa kipindupindu Congo tangu Januari - UNICEF

#1


Maelezo ya picha,Mchimbaji madini akiwekewa dripu katika kituo cha matibabu ya kipindupindu kinachoendeshwa na Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) kufuatia mlipuko wa kipindupindu ambao umeelemea mfumo dhaifu wa afya.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inapambana na mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 25 ambao umeua takriban watu 2,000 tangu Januari, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto limesema Jumatatu.

Katika kisa kimoja, robo ya watoto katika kituo cha watoto yatima cha Kinshasa - 16 kati ya 62 - walikufa siku chache baada ya ugonjwa huo kuenea, UNICEF iliongeza.

Kipindupindu ni ugonjwa mbaya wa kuhara unaoweza kusababisha kifo ambao huenea haraka wakati maji taka na maji ya kunywa ambayo ni machafu.

Mamlaka ya afya ya Afrika mwezi uliopita ilitoa tahadhari kuhusu kuongezeka kwa ugonjwa huo nchini Angola, Burundi na maeneo mengine ya bara, na ongezeko la jumla la 30% la kesi zilizorekodiwa mwaka jana.

Nchini Congo, ukosefu wa maji safi umezidisha ugonjwa huo, na ufadhili zaidi unahitajika kwa ajili ya usafi wa mazingira, usafi na huduma za afya, imesema UNICEF.

Tangu Januari, mamlaka imerekodi kesi 64,427 na vifo 1,888, ikiwa ni pamoja na maambukizi 14,818 na vifo 340 miongoni mwa watoto, UNICEF ilisema. Mikoa 17 kati ya 26 ya nchi hiyo kwa sasa imeathiriwa, shirika hilo liliongeza.

Ni asilimia 43 tu ya watu nchini Congo wanapata huduma za msingi za maji, kiwango cha chini kabisa barani Afrika, na ni asilimia 15 pekee wanaotumia huduma za usafi wa mazingira, kulingana na taarifa hiyo.

Serikali ina mpango wa kutokomeza kipindupindu na bajeti inayopendekezwa ya dola milioni 192, lakini hiyo inasalia kuwa na ufadhili mdogo, imesema UNICEF.

UNICEF inaomba takriban dola milioni 6 mwaka 2026 ili kuendeleza kazi yake.

"Bila ya fedha za ziada na hatua zilizoratibiwa, maisha mengi zaidi yanaweza kupotea," amesema msemaji wa UNICEF, John Agbor.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code