Dhana Potofu kuhusu kunyonyesha,Wiki ya Unyonyeshaji

Dhana Potofu kuhusu kunyonyesha,Wiki ya Unyonyeshaji

#1

Takwimu za hivi karibuni za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, zinakadiria kuwa unyonyeshaji usio wa kutosha husababisha asilimia 16 ya vifo vya watoto kila mwaka.



Shirika la Afya Duniani (WHO) linahimiza akina mama kuungwa mkono na jamii, familia, na wahudumu wa afya wakati wa kunyonyesha.

Kwa kuunda mifumo rafiki ya unyonyeshaji, na kuheshimu haki ya wanawake ya kunyonyesha wakati wowote, mahali popote, na kukuza usaidizi wa kijamii.

Wiki ya Unyonyeshaji Duniani hufanyika katika wiki ya kwanza ya Agosti kila mwaka.

Lakini bado kuna imani potofu kuhusu unyonyeshaji, ambazo zinaweza kuwazuia wanawake kunyonyesha. 

Titi kuuma sio jambo la kawaida

Kwa siku za awali ni kawaida ziwa kuuma kabla hujazoea. Lakini kunyonyesha hakupaswi kuumiza au kusababisha maumivu makali.

Kuuma kwa chuchu inaweza kuwa ni dalili ya maambukizi au mtoto hanyonyi jinsi ambavyo inatakiwa. Maumivu madogo ya awali ni kawaida, haswa kwa akina mama wanaoanza kuzoea kunyonyesha.

Subiria kabla ya kunyonyesha

Jambo lolote linalohimiza akina mama kunyonyesha ni zuri kwa afya ya binadamu. Hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba mama anapaswa kuvuta muda kabla ya kuanza kunyonyesha baada ya kujifungua.

Kizuizi chochote cha kunyonyesha baada ya kujifungua hakina mashiko ya kisayansi. Na kuna faida nyingi za mtoto kunyonya mara tu baada ya kujifungua.

Kunyonyesha ni lishe kwa mtoto. Pia husaidia kusinyaa kwa mfuko wa uzazi, na kusaidia kuzuia au kupunguza kasi ya kutoka kwa damu baada ya kujifungua.

Pia, katika siku chache za kwanza baada ya kujifungua, mwili wa binadamu hutoa protini maalumu inayoitwa kolostramu, ambayo hufanya maziwa kuzalishwa.

Huwezi kutumia dawa yoyote ikiwa unanyonyesha

Hilo huwa ni swali la kwanza kwa mama popote duniani. Je, dawa yoyote ni salama kwa mtoto wangu?

Ukweli ni kwamba dawa nyingi humfikia mtoto katika kiwango cha chini sana. Ikiwa daktari anasema unahitaji dawa, uliza maswali yako lakini kuna uwezekano mkubwa kuwa dawa hiyo ni salama kutumia.

Kile ambacho mtoto anahitaji zaidi ya yote ni mama mwenye afya. Dawa nyingi zinazoshughulikia maambukizi, uchovu au maumivu zinaweza kuwa salama.

Na dawa ambazo hazipaswi kutumiwa wakati wa kunyonyesha, ni chache sana. Mara nyingi ni kwa ajili ya matibabu ya hali mbaya sana za Kiafya kama vile saratani.

Kuna dawa zingine ambazo unatakiwa kutumia kwa uangalifu kwa kuzingatia hatari na faida. Mwanamke yeyote ambaye anapewa dawa wakati wa kunyonyesha anapaswa kumuuliza daktari maswali.

Mfano dawa za mafua, kupiga chafya au koo kuwasha, ambazo zinafungua mishipa - hizi zinaweza kupunguza mtiririko wa maziwa.

Pia kuwa mwangalifu na dawa za mitishamba kwa sababu huwezi kujua zina nini ndani yake, na nyingi ya dawa hizo hazijafanyiwa utafiti wa kina.

Epuka chakula chenye viungo

Hakuna kitu ambacho mama hapaswi kula anaponyonyesha. Lakini maziwa ya mama yanaweza kuathiriwa na ulaji wako.

Kwa mfano, niligundua nikinywa juisi ya matunda ya jamii ya machungwa, mtoto wangu huwa na hasira sana.

Wakati mwingine unaweza kugundua tabia za mtoto wako kwa chakula ambacho umekula. Lakini hakuna kitu ambacho kinamdhuru au sio sahihi kiafya na ambacho kinahitaji kuepukwa.

Usitumie maziwa ya unga kama unanyonyesha

Mwili wa mwanamke umeumbwa kuwa na uwezo wa kutoa maziwa ya kutosha kwa mtoto wako. Mtoto anaponyonya chuchu, huchochea homoni kutoa kiasi kinachohitajika cha maziwa.

Kwa hivyo, ikiwa unanyonyesha mtoto mdogo, mkubwa au hata mapacha, mwili wako utatoa maziwa ya kutosha.

Ukianza kumpa maziwa ya unga, homoni zitajizuia. Mwili wako hautopata ishara za kutosha kwamba mtoto anahitaji maziwa zaidi.

Ikiwa unakabiliwa na tatizo la uhaba wa maziwa na ukaanza kumpa mtoto maziwa ya kopo, hilo linaweza kukupa nafuu ya muda mfupi, lakini tatizo la uhaba wa maziwa linaweza kuwa kubwa.

Kwa upande mwingine, ikiwa umechoka usiku au ni mgonjwa na mpenzi wako anampa mtoto maziwa ya unga ili apumzike, hiyo haimaanishi huwezi kunyonyesha. Kwa hivyo maziwa ya unga sio jambo baya, lakini yanaweza yasiwe na msaada mzuri.

Usinyonyeshe ukiwa mgonjwa

Hapana, hiyo ni imani potofu. Hali pekee ambayo mtu anapaswa kupata Ushauri wa kina kabla ya kunyonyesha ni ikiwa ana VVU au homa ya manjano. Virusi hivyo vinaweza kupita kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Akina mama wanapokuwa wagonjwa miili yao hutoa kingamwili ambazo pia hulinda watoto wao wachanga. Ni nadra sana kuona ugonjwa wa mama anaenyonyesha ukimpata mtoto.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code