Showing posts with label Uchaguzi wa Wabunge. Show all posts
Showing posts with label Uchaguzi wa Wabunge. Show all posts

Orodha ya Wabunge Walioteuliwa kugombea Ubunge na Majimbo yao,Makonda,Baba Levo ndaniAfyaclass Forum •

Orodha ya Wabunge Walioteuliwa kugombea Ubunge na Majimbo yao,Makonda,Baba Levo ndani

-Paul Makonda

Chama cha Mapinduzi kimemteua Paul Makonda kuwa Mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika Jimbo la Arusha Mjini.

Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Amos Makalla amesema hayo leo August 23,2025 wakati akitangaza maamuzi ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.


Baba Levo:Kugombea Kigoma Mjini

Chama cha Mapinduzi kimemteua Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo) kuwa Mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika Jimbo la Kigoma Mjini.

Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Amos Makalla amesema hayo leo August 23,2025 wakati akitangaza maamuzi ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

0 Comment

Makada 24 wajitokeza kumrithi Ndugai KongwaAfyaclass Forum •

Wagombea 24 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua fomu kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge mstaafu na Mbunge wa jimbo hilo, Hayati Job Ndugai. Tukio hilo limefanyika jana, Agosti 12, 2025.



Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa CCM kuanza upya mchakato wa kujaza nafasi hiyo, baada ya Hayati Ndugai kuibuka mshindi kwenye kura za maoni zilizopigwa Agosti 4, 2025, ambapo alipata kura 5,690 na kuwashinda wagombea wengine tisa waliopitishwa na vikao vya juu vya uteuzi wa chama.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala, amesema kati ya wagombea 24 waliochukua fomu, watatu ni wanawake na 21 ni wanaume.

“Wale wote tisa waliopitishwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa pamoja na Hayati Ndugai wamechukua fomu. Pia, tunazo sura mpya 10 katika idadi hiyo,” amesema Mkaugala.

CCM Wilaya ya Kongwa ilitangaza kuanza upya mchakato wa kuchukua fomu Agosti 11, 2025, mara baada ya kumalizika kwa shughuli za maziko ya Hayati Ndugai.

0 Comment

Majaliwa aahirisha kugombea Ruangwa 2025Afyaclass Forum •

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, hatogombea tena Ubunge wa Ruangwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kama alivyoahidi mara kadhaa ikiwemo juzi akiwa Bungeni, chanzo cha kuaminika kimeiambia AyoTV.



Waziri Mkuu Majaliwa ambaye amekuwa Mbunge wa Ruangwa kwa miaka 15 kuanzia mwaka 2010, aliteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 katika awamu ya tano chini ya Hayati Dr. John Pombe Magufuli na kisha kuaminiwa na awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuhudumu katika nafasi hiyohiyo baada ya Rais Magufuli kufariki.

 Via:MillardAyoUPDATES

0 Comment

Ester Bulaya achukua fomu ya Ubunge jimbo la BundaAfyaclass Forum •

Aliyekuwa Mbunge wa viti maalum Ester Bulaya amechukua fomu ya kuwania Ubunge wa jimbo la Bunda mkoani Mara kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.



Ester Bulaya amechukua fomu hiyo leo June 30 2025, akilenga kuchuana na watia nia wengine akiwemo Mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake Robert Maboto.

Ester Bulaya kabla kurejea CCM amewahi kuwa Mbunge wa Vijana kupitia CCM Mwaka 2010, na baadae kwenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kuwa Mbunge wa kuchaguliwa Mwaka 2010 -2015 jimbo hilo kupitia CHADEMA, Mwaka  2010 - 2020 Mbunge wa Viti Maalum. 

Leo Bulaya amekabidhiwa fomu ya kutia nia ya Ubunge ndani ya chama hicho na Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda, Evodia Zumba.

0 Comment

Jesca Magufuli achukua form ya Ubunge Viti MaalumAfyaclass Forum •

Jesca Magufuli ambaye ni Mtoto wa Rais wa awamu ya tano Hayati Dr. John Pombe Magufuli, leo June 28 2025 amechukua rasmi fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa.

Jesca ni Binti ambaye amejipambanua kama sauti ya matumaini kwa Vijana na Wanawake wa Tanzania akisimamia maadili, haki na maendeleo jumuishi ambapo amelenga kupeleka nguvu mpya ya kijana Bungeni, kusimamia ajenda za maendeleo kwa Vijana, Wanawake na Jamii kwa ujumla huku akihakikisha UVCCM inasikika, inaonekana na inawakilishwa kwa heshima katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nipo tayari kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu, umoja na kwa kutanguliza maslahi ya Vijana na Wanawake, Geita inapeleka sauti ya mabadiliko chanya,” amesema Jesca Magufuli mara baada ya kuchukua fomu hiyo leo.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD