Showing posts with label chanjo. Show all posts
Showing posts with label chanjo. Show all posts

Kampeni ya chanjo kwa watoto yazinduliwa Ukanda wa GazaAfyaclass Forum •

Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF, afya duniani WHO, linalohudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA na wizara ya afya ya Palestina wamezindua kampeni maalum ya chanjo, lishe na ufuatiliaji wa ukuaji wa watoto katika Ukanda wa Gaza, lengo likiwa ni kuwafikia watoto 44,000 waliokosa huduma muhimu za afya kutokana na vita vilivyodumu kwa miaka miwili.

Taarifa ya pamoja ya mashirika hayo imeeleza kuwa kampeni hiyo itafanyika kwa awamu tatu, Kati ya mwezi huu wa Novemba 2025 mpaka mwezi Januari 2026 ikilenga kuwapatia watoto chanjo dhidi ya magonjwa hatari kama surua, rubella, kifaduro, dondakoo, pepopunda, homa ya ini, kifua kikuu, polio na nimonia.

Awamu ya kwanza itaanza tarehe 9 hadi 18 Novemba 2025. Awamu ya pili na ya tatu za kampeni zinatarajiwa kufanyika Desemba 2025 na Januari 2026, zikiwa na lengo la kurejesha kiwango cha chanjo kama kabla ya vita.

Kabla ya vita, Gaza ilikuwa na kiwango cha chanjo cha zaidi ya asilimia 98 kwa watoto, lakini sasa kiwango cha chanjo kimeshuka chini ya asilimia 70.

0 Comment

Kuku Zaidi ya millioni 40 kupatiwa chanjo bureAfyaclass Forum •

Kuku Zaidi ya millioni 40 kupatiwa chanjo bure

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia imepanga kutoa chanjo za kuku milioni arobaini (40) ambapo jumla ya dozi 19,099,100 za chanjo ya Homa ya Mapafu ya Ng'ombe (CBPP) zimenunuliwa kwa ajili ya kuchanja ng'ombe 19,099,100.

Pia zimepatikana dozi 17,224,200 za chanjo ya Sotoka ya Mbuzi na Kondoo kwa ajili ya kuchanja mbuzi na kondoo 17,224,200, na dozi 40,000,000 za chanjo ya ugonjwa wa kideri/mdondo (ND), ndui na mafua ya kuku kwa ajili ya kuchanja kuku wa asili 40,000,000.

Hata hivyo chini ya Rais Samia, ruzuku ya chanjo na mifumo ya utambuzi wa mifugo imeimarishwa ambapo hadi mwaka 2025 zaidi ya dozi milioni 100 za chanjo zimesambazwa kwa mifugo, huku mfumo wa hereni za kielektroniki ukiwezesha kutambua zaidi ya ng'ombe milioni 3.5.

Hatua hii inalenga kupata ithibati ya WOAH ili Tanzania iweze kuuza mifugo na nyama yake katika masoko ya kimataifa yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 2 kwa mwaka. Aidha, Mradi wa Chanjo Kitaifa umeanzishwa ukiwa na uwezo wa kuzalisha dozi milioni 50 za chanjo za mifugo kwa mwaka, mradi huu umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 216 na unatarajiwa kupunguza gharama za uagizaji chanjo kutoka nje kwa zaidi ya asilimia 70, kuongeza imani ya walaji wa mazao ya mifugo kutoka ndani na nje ya nchi, na kufungua masoko mapya ya kuuza nyama, maziwa na ngozi katika nchi za Mashariki ya Kati na Asia.

0 Comment

Asilimia 60 ya vifo Maniema nchini DRC husababishwa na MalariaAfyaclass Forum •

Asilimia 60 ya vifo Maniema nchini DRC husababishwa na Malaria



Jimbo la Maniema nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hatimaye nalo limechukua hatua ya kukabiliana na Malaria kwa kujumuisha chanjo dhidi ya ugonjwa huo kwenye ratiba ya chanjo kwa watoto.

Hii inafuatia tangazo la shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, kanda ya Afrika la tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka jana wa 2024 ya kwamba DRC imeanza kutumia chanjo dhidi ya Malaria, R21 kwenye mpango wa kitaifa wa chanjo, na hivyo kuongeza mbinu muhimu kwenye zile zilizoko za kudhibiti malaria.

Asilimia 60 ya vifo Maniema husababishwa na Malaria

Kwa mujibu wa Radio Okapi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini DRC, MOUSCO, hatua hiyo imefanyika kwenye mji mkuu wa jimbo la Maniema, Kindu siku ya Jumanne ya Agosti 19.

Kwa mujibu wa Idara ya Afya ya jimbo la Maniema, malaria ndiyo chanzo cha asilimia 60 ya vifo na magonjwa jimboni humo na kwamba watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 na wanawake wajawazito ndio wahanga wakuu wa ugonjwa huu, hali inayohalalisha uharaka wa kuanzishwa kwa chanjo hii.

Walengwa na utekelezaji

Chanjo hii itatolewa kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi 6 hadi miezi 23, katika maeneo yote ya afya ya jimbo la Maniema ikiwa ni sehemu ya mkakati madhubuti wa kinga, unaolenga kupunguza mzigo wa ugonjwa huu katika jamii zilizo hatarini zaidi.

Kupitia mpango huu, Maniema inalenga kupunguza vifo vinavyotokana na malaria na kuimarisha uimara wa mfumo wake wa afya.

Mafanikio ya kampeni hii yatategemea ushirikiano wa familia na utekelezaji bora wa timu za afya katika maeneo ya huduma.

0 Comment

Chanjo huzuia Vifo million 3.5 ila Zaidi ya watoto milioni 14 hawakuchanjwa 2024Afyaclass Forum •

Chanjo huzuia Vifo million 3.5 ila Zaidi ya watoto milioni 14 hawakuchanjwa 2024



Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watoto milioni 14 hawakupata chanjo kabisa mwaka 2024.

Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, chanjo huzuia vifo milioni 3.5 hadi 5 kwa mwaka.

Taarifa ya pamoja ya Shirika la Afya Duniani, WHO, na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto, UNICEF, iliyotolewa Jumanne, imeeleza kuwa barani Ulaya na Asia ya Kati, viwango vya wastani vya chanjo ya watoto vilishuka kwa asilimia 1.

Maafisa wameonya kwamba kuenea kwa habari potofu na kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa kunaongeza pengo la chanjo na kuwaweka malioni ya watoto hatarini.

Nchi tisa ndiyo zimechangia zaidi ya nusu ya watoto wasiokuwa na chanjo duniani.

Nchi hizo ni pamoja na Nigeria, India, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Ethiopia, Indonesia, Yemen, Afghanistan, na Angola.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Catherine Russell, amesema mamilioni ya watoto bado hawajapata chanzo za kuwaepusha na magonjwa yanayoweza kuzuilika, na kwamba jambo hilo linatia wasiwasi.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD