Kuku Zaidi ya millioni 40 kupatiwa chanjo bure
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia imepanga kutoa chanjo za kuku milioni arobaini (40) ambapo jumla ya dozi 19,099,100 za chanjo ya Homa ya Mapafu ya Ng'ombe (CBPP) zimenunuliwa kwa ajili ya kuchanja ng'ombe 19,099,100.
Pia zimepatikana dozi 17,224,200 za chanjo ya Sotoka ya Mbuzi na Kondoo kwa ajili ya kuchanja mbuzi na kondoo 17,224,200, na dozi 40,000,000 za chanjo ya ugonjwa wa kideri/mdondo (ND), ndui na mafua ya kuku kwa ajili ya kuchanja kuku wa asili 40,000,000.
Hata hivyo chini ya Rais Samia, ruzuku ya chanjo na mifumo ya utambuzi wa mifugo imeimarishwa ambapo hadi mwaka 2025 zaidi ya dozi milioni 100 za chanjo zimesambazwa kwa mifugo, huku mfumo wa hereni za kielektroniki ukiwezesha kutambua zaidi ya ng'ombe milioni 3.5.
Hatua hii inalenga kupata ithibati ya WOAH ili Tanzania iweze kuuza mifugo na nyama yake katika masoko ya kimataifa yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 2 kwa mwaka. Aidha, Mradi wa Chanjo Kitaifa umeanzishwa ukiwa na uwezo wa kuzalisha dozi milioni 50 za chanjo za mifugo kwa mwaka, mradi huu umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 216 na unatarajiwa kupunguza gharama za uagizaji chanjo kutoka nje kwa zaidi ya asilimia 70, kuongeza imani ya walaji wa mazao ya mifugo kutoka ndani na nje ya nchi, na kufungua masoko mapya ya kuuza nyama, maziwa na ngozi katika nchi za Mashariki ya Kati na Asia.








image quote pre code