Showing posts with label magonjwa ya wanawake. Show all posts
Showing posts with label magonjwa ya wanawake. Show all posts

Ndizi 1 tu husaidia kupunguza na kuondoa Maumivu wakati wa HedhiAfyaclass Forum •

Kwa Mwanamke anayepata maumivu makali wakati wa hedhi anaelewa jinsi maumivu hayo yanavyokuwa. Sasa hapa kuna kitu rahisi ambacho kinaweza kusaidia kidogo - ndizi.

Ndizi zina magnesiamu na vitamini B6, ambazo zote zina jukumu la kulegeza misuli na kupunguza Mkazo. Maumivu ya hedhi hutokea kwa sababu uterasi yako inasisimka na kubana zaidi(Contracts) ili kutoa utando wake. Magnesiamu husaidia kulegeza misuli laini, ambayo inaweza kupunguza nguvu ya mikazo hiyo. Utafiti fulani pia unaonyesha kwamba viwango vya kutosha vya magnesiamu vinaweza kupunguza prostaglandini -ambayo husababisha maumivu yanayoambatana na mikazo.

Hivi ndivyo ndizi inavyoweza kukusaidia wakati wa hedhi:

• Magnesiamu ndani yake husaidia kulegeza misuli ya uterasi

• Vitamini B6 inaweza kupunguza uvimbe,Mkazo na mabadiliko ya hisia

• Sukari asilia hutoa nishati ya haraka ikiwa unahisi dhaifu sana mwilini

• Potasiamu husaidia kuzuia maumivu ya misuli na uchovu

Ndizi moja haitaondoa kabsa maumivu makali, lakini inaweza kuwa msaada wa kupunguza maumivu na wa asili kama sehemu ya lishe bora kwa ujumla.

 Kwa matokeo bora, changanya na:

• Kunywa maji Vizuri,Uji au maziwa,Tangawizi,Maji ya uvuguvugu n.k.

• Kufanya mazoezi mapesi kama kujinyoosha au kutembea

• Kutumia Warm compress kwenye tumbo la chini

• Kulala vya kutosha n.k.

Kumbuka: Ikiwa maumivu yako ya hedhi ni makali, Hali inazidi kuwa mbaya, au yanaathiri maisha yako ya kila siku, ni muhimu kushauriana na mtaalamu wa afya. Hali kama vile endometriosis au PCOS zinahitaji mwongozo sahihi wa kimatibabu. Na Kwa ushauri zaidi unaweza kutuma Neno Afyaclass Inbox.

0 Comment

Kupata Damu Ya Hedhi Nyeusi inaashiria nini?Afyaclass Forum •

Kupata Damu Ya Hedhi Nyeusi inaashiria nini?

Kupata damu ya hedhi nyeusi mara nyingi si tatizo kubwa, bali inaashiria damu ya zamani iliyokaa muda mrefu ndani ya mji wa mimba (uterasi) kabla ya kutoka. Damu inapokaa muda, hukosa hewa (oxidation) na kuwa rangi ya kahawia au nyeusi.

Tuangalie nini huashiria Damu ya Hedhi ikitoka Nyeusi,Hapa kuna maana mbalimbali:

1. Damu ya zamani kutoka

Hii Huonekana mwanzoni au mwishoni mwa hedhi,na inakuwa;

  • Kiasi kidogo
  • Na Haina harufu kali

Hii huwa ni kawaida.

2. Mzunguko wa hedhi kuchelewa

Kama hedhi ilichelewa, damu inaweza kuwa nzito na nyeusi

Huambatana na maumivu kidogo ya tumbo

3. Mabaki ya mimba (kama Mimba iliwahi kuharibika)

Kama Mimba iliharibika na kukuwa na mabaki ndani,Damu nyeusi inaweza kutoka kwa siku kadhaa,Na Huambatana na maumivu makali au damu nyingi.

4. Maambukizi ya Kwenye Via vya Uzazi (kama PID au UTI kali)

Ikiwa tatizo ni maambukizi haya,Damu nyeusi yenye na harufu mbaya sana inaweza kutoka,Lakini pia unaweza kupata dalili Zingine kama vile;

  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Maumivu ya tumbo la chini au Chini ya Kitovu

Hapa inahitaji kuonana na daktari au Kuongea na Wataalam wa afya kwa Ushauri wa haraka.

5. Dalili za mimba changa (implantation bleeding)

Damu kidogo sana, rangi kahawia au nyeusi huweza kutokea kabla ya tarehe ya hedhi, hii ikiwa inaashiria Mimba changa inapojishikiza kwenye mji wa Mimba,Damu hii kitaalamu hujulikana kama Implantation bleeding.

Kumbuka: Hakikisha Unaongea na daktari kama damu inatoka nyeusi na Inaambatana na Dalili hizi;

  • Kuna harufu kali sana
  • Unapata Maumivu makali ya tumbo
  • Damu nyingi isiyo ya kawaida
  • Hali inaendelea miezi kadhaa

Je,Una tatizo hili na hujapata Tiba bado? 

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mwanamke Afyaclass Forum •

Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mwanamke 

Watu wengi huhusisha kimakosa maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa wanawake na matatizo ya uzazi pekee. Hii si sahihi. Hali nyingi za kiafya zinaweza kusababisha Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mwanamke, na utambuzi sahihi ni muhimu kwa matibabu bora kwa wanawake wa rika zote.

Chanzo cha Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mwanamke 

Maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa mwanamke yanaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, Nitayaeleza kwa lugha rahisi ili uweze kujitathmini, lakini bado ni muhimu kumuona mtaalamu kama maumivu ni makali au yanaendelea.

1. Maumivu ya Siku za Hedhi

Maumivu haya yanaweza kuhusiana na siku za hedhi, hasa kabla au wakati wa hedhi kutokana na kukaza kwa mfuko wa uzazi.

2. Maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya Mwanamke(PID) yanaweza kusababisha maumivu chini ya kitovu, na mara nyingi huambatana na uchafu usio wa kawaida ukeni, harufu mbaya au maumivu wakati wa kujamiiana.n.k.

3. Tatizo la Uvimbe kwenye kizazi(Fibroids) au Tatizo la Vivimbe maji(Ovarian cysts)

Ovari cysts pia husababisha maumivu ya upande mmoja au chini ya tumbo kwa Wanawake wengi,

Uvimbe kwenye kizazi ni uvimbe ambao huonekana sana kwa wanawake hasa wenye umri wa miaka 30-40. Ingawa baadhi ya wanawake wanaweza kuwa hawana dalili zozote, wengine wanaweza kupata maumivu ya tumbo, maumivu ya mgongo, maumivu wakati wa tendo la ndoa, au ugumu wa kupata mimba.

Lakini pia tatizo la Endometriosis ambalo huhisha tishu za uterasi kukua nje ya uterasi(mfuko wa uzazi), Hali hii mara nyingi huhusishwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu na inaweza kuchangia Mwanamke asipate Ujauzito.

4. Maambukizi kwenye njia ya Mkojo(UTI)

Sababu nyingine ni matatizo ya mfumo wa mkojo ikiwemo Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) husababisha maumivu chini ya kitovu, hisia ya kuchoma wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara au mkojo wenye harufu kali n.k. Na Wakati mwingine maumivu huongezeka unapobana mkojo.

5. Tatizo la Mimba kutunga nje ya Kizazi(Ectopic pregnancy)

Mimba kutunga nje ya kizazi hutokea wakati kiinitete kinapopandikizwa na kukua nje ya uterasi(mfuko wa uzazi), Na mara nyingi hutokea kwenye mirija ya uzazi yaani fallopian tubes.

Hii ni hali inayohatarisha maisha,na hali hii huweza kuambatana na dalili mbali mbali ikiwemo; maumivu makali ya tumbo (mara nyingi huonekana upande mmoja), kutokwa na damu ukeni, kichefuchefu, na kizunguzungu. Hapa Ushauri wa haraka wa kimatibabu unahitajika.

6. Magonjwa ya Zinaa-Sexually Transmitted Infections (STIs)

Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mwanamke yanaweza kusababishwa pia na magonjwa ya zinaa kama vile;

Dalili zingine ni pamoja na maumivu wakati wa kukojoa, kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni, na kutokwa na damu isiyo ya kawaida katikati ya hedhi. Ushauri wa haraka wa kimatibabu ni muhimu ili kuzuia maambukizi na matatizo Zaidi.

7. Tatizo la Mawe kwenye Figo(Kidney Stones)

Tatizo hili pia huweza kusababisha hali ya Maumivu hasa pale Mawe haya Yanaposogea, yanaweza kusababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu.

8. Kwa Upande wa mfumo wa chakula pia unaweza kuwa chanzo

Gesi tumboni, kuvimbiwa, au matatizo ya utumbo kama IBS husababisha maumivu ya chini ya tumbo yanayokuja na kuondoka. Kama maumivu yapo zaidi upande wa kulia na yanaongezeka taratibu, Tatizo la appendicitis au kidole tumbo(Appendix) pia huanza kama maumivu chini ya kitovu kisha kuhamia upande wa kulia.

Kwa mwanamke aliye katika umri wa kupata ujauzito, mimba pia ni chanzo muhimu cha kuzingatia. Maumivu chini ya tumbo yanaweza kuwa ya kawaida mwanzoni mwa mimba, lakini kama yanaambatana na damu ukeni, kizunguzungu au maumivu makali upande mmoja, inaweza kuwa mimba nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancy) ambayo ni hatari na huhitaji matibabu ya haraka.

Je,Una tatizo hili na hujapata Tiba bado?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Soma pia Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Mjamzito https://www.afyaclass.com/2024/09/maumivu-ya-chini-ya-kitovu-kwa-mjamzito.html

Rejea Link:

https://www.vinmec.com/eng/blog/what-is-dull-lower-abdominal-pain-in-women-1

https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/24530-lower-abdominal-pain

https://www.medicalnewstoday.com/articles/319931

0 Comment

Mbegu kutoka ukeni baada ya tendo chanzo chake na TibaAfyaclass Forum •

Mbegu kutoka ukeni baada ya tendo chanzo chake na Tiba

Tatizo la mbegu kutoka nje ya Uke baada ya tendo la ndoa chanzo kikubwa ni nini



Tatizo la mbegu kutoka nje baada ya tendo la ndoa ni jambo linalowahusu wanandoa au wapenzi wengi, hasa wale wanaojaribu kupata mtoto. Kwa kawaida, baada ya mwanaume kumwaga mbegu ndani ya uke, ni kawaida kiasi kidogo cha shahawa kurudi nje. Hata hivyo, ikitokea kiasi kikubwa kinatoka mara kwa mara, inaweza kuwa sababu ya kushindwa kupata mimba, japo si mara zote.

Sababu Zinazowezekana za Mbegu kutoka Nje:

  1. Mwili wa mwanamke kuwa wima haraka baada ya tendo
    – Kusimama au kwenda bafuni mara moja baada ya tendo kunaweza kusababisha mbegu kutoka kabla hazijaingia ndani vizuri.

  2. Shughuli ya misuli ya uke
    – Misuli ya uke inaweza kushindwa kuzuia mbegu ndani, hasa kama hakuna mshikamano mzuri wa misuli ya nyonga.

  3. Wingi wa shahawa
    – Wakati mwingine, kama mwanaume anatoa shahawa nyingi kupita kiasi, ni kawaida nyingine kutoka nje kwa sababu nafasi ya uke haitoshi kuziweka zote mara moja.

  4. Kutoingia kwa uume vizuri
    – Ikiwa uume haujaingia vizuri au tendo limefanyika kwa haraka sana, mbegu huweza kumwagwa karibu na mlango wa uke na kutoka kirahisi.

  5. Uwezekano wa matatizo ya mlango wa kizazi
    – Kama mlango wa kizazi (cervix) hauko katika nafasi nzuri ya kupokea mbegu (mfano mwanamke akiwa juu), mbegu haziwezi kuelekezwa vizuri ndani.

Je, hali hii ni tatizo kubwa?

Kwa kawaida, si tatizo kubwa na haitoshi peke yake kueleza kuwa Sababu ya Mwanamke kutokubeba mimba ingawa inaweza kuchangia pia. Kwa Wanawake wengi, kiasi cha mbegu kinachobaki ndani kinatosha kabisa kwa ajili ya kurutubisha yai. Kwa hiyo, ikiwa mnaendelea kufanya tendo mara kwa mara katika kipindi cha ovulation, kuna uwezekano mkubwa wa kushika mimba.

Njia za kusaidia kupunguza tatizo hili:

  1. Kubadilisha mikao ya tendo la ndoa:
    – Mikao kama mwanamke akiwa chini (missionary style) inasaidia mbegu kuingia zaidi na kukaa kwa muda mrefu.

  2. Kubaki umelala kwa mgongo baada ya tendo:
    – Mwanamke abaki amelala dakika 15–30 baada ya tendo, akiegesha mto chini ya nyonga ili mbegu ziende juu kuelekea kwenye kizazi.

  3. Epuka kusimama au kuoga haraka baada ya tendo

  4. Tumia mazoezi ya nyonga (Kegel exercises)
    – Husaidia kuimarisha misuli ya uke na kuzuia mbegu kutoka kwa haraka.

Wakati wa Kumwona Daktari:

Fikirieni kuonana na daktari au mtaalamu wa afya ya uzazi iwapo:

  • Mmejaribu kupata mimba kwa zaidi ya miezi 12 bila mafanikio.
  • Kuna dalili nyingine kama maumivu wakati wa tendo, kutokwa na uchafu usio wa kawaida, au hedhi isiyo ya kawaida.
  • Unashuku tatizo la uzazi kwa mmoja wenu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD