TATIZO LA KUZAA MTOTO NJITI
Mama mjamzito anatakiwa KUJIFUNGUA mtoto kuanzia Wiki 38 mpaka Wiki 42 huyu mtoto anakuwa amekomaa na akizaliwa anakuwa na uwezo wa Kuishi bila kupata Shida.
Kuna changamoto mbali mbali zinafanya mama anajifungua KABLA YA WAKATI,CHINI YA WIKI 37,huyu mtoto tunamwita PREMATURE au NJITI.
Mtoto kuzaliwa Kabla ya wakati,ni kisababishi kikubwa cha watoto wachanga Kufariki wengi wanapata shida za KUPUMUA na kupata infection kirahisi.
Na chanzo Kikubwa ni Mama anakuwa AMEPATA UCHUNGU KABLA YA WAKATI WAKE(PRETERM LABOUR),Au mama anaanza kutoka maji kabla ya wakati(Preterm Premature rapture of membranes) au kuna changamato zitokanazo na mama zinaweza laazma WATAALAM tumfanye mama apate mtoto kabla ya wakati,mfano mama akiwa na Kifafa cha Mimba,mamama anatakiwa ajifungue HARAKA SANA ndani ya masaa 12 kwahiyo kama hajafika wiki 38,haijalishi(tunafanya kuokoa maisha ya mama).
Na watoto waliozaliwa chini ya wiki 37 wengi wanakuwa na kilo ndogo,lakin pia Hata kama utapata mtoto wa kilo hata 2.5 ukiwa umejifungua kabla ya wiki 37 ni mtoto njiti
Lakin visababishi vikubwa ni;
1. INFECTION kwenye mji wa uzazi(chorioamnionitis)
2.mama akiwa na kisukari huwa pia ni kichangizi
3.mama akiwa na mimba za MAPACHA,kama.mnavyoona hizo picha za mbele,kuna seti kama 3 za mapacha walizaliwa kabla ya wakati,mara chache sana Mama mwenye mapacha akafika wiki 38.
4.lakin pia mama akiwa mdogo ki umri yaan miaka 12 mpaka 15 na mama akiwa mkubwa sana ki umri kuanzia miaka 40 huchangia mama ajifungue kabla ya wakati.
5.uvutaji sigara na kunywa pombe hivi pia Husababisha Sana.
Kujifungua Njiti kunaweza kumpata MWANAMKE YEYOTE YULE.
Na watoto njiti wakipata huduma nzuri(huwa wanakuwa kwenye chumba cha JOTO chini ya uangalizi na kufuatiliwa kila baada ya muda mfupi hali zao na vipimo vya mara kwa mara,ulaji wao,lakin pia Kupewa JOTO kwa Kangaroo method,mtoto huyu anakuwa ngozi kwa ngozi na mama ake au mlezi wake).
Watoto njiti WAKIWA WAKUBWA wanakuwa KAWAIDA KAMA WATOTO WENGINE,na wengi wanakiwaga na Afya sana🥰🥰.
Mungu atulinde wanawake wote kwenye safari zetu za Uzazi.na Pia tukipata watoto njiti,awapiganie kwa ajili Yetu
#Uzazipoint #afyaclass
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



