JE NAWEZA KUJIFUNGUA KWA NJIA YA KAWAIDA BAADA YA KUFANYIWA OPERATION MIMBA ILIYOPITA?

JE NAWEZA KUJIFUNGUA KWA NJIA YA KAWAIDA BAADA YA KUFANYIWA OPERATION MIMBA ILIYOPITA?

#1

JE NAWEZA KUJIFUNGUA KWA NJIA YA KAWAIDA BAADA YA KUFANYIWA OPERATION MIMBA ILIYOPITA?

Swali kutoka INBOX.

JE,naweza kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya kufanyiwa Operation mimba iliyopita?????? Jibu Lake ni NDIYO/HAPANA.


Kuna sababu inayofanya Mtu afanyiwe Operatio(POST iliyopita INA MAELEZO),mfano sababu zilizo very common ni Nyonga kuwa finyu,CPD,mtoto kuwa mkubwa,mtoto kupata shida ya kupumua,njia kutofunguka etc(SOMA POST YA NYUMA)


Sasa,mtu aliefanyiwa OPERATION

Ili ajifungue kawaida mimba inayofuata,kuna VIGEZO...ili ujaribishe ku push,trial of scar

Vigezo hivi:


1.kwanza kabisa mshono uwe Umepona kabisa,uwe una miaka mitatu angalau,sio umefanyiwa Op leo,ndani ya miez 6 una Mimba,hapo Ni hatari ukipata uchungu,uchungu unaweza fanya MSHONO kwenye kizazi uchanike


2.sababu iliyokufanya ufanyiwe OP Iliyopita isiwe ni sababu Endelevu,iwe ni sababu ya mimba iliyopita Tu,mfano mtoto kaa alikuwa na kilo 5,mimba ya sasa anakio 3,unaweza Push,lakin kama nyonga yako ni Finyu,una contracted pelvis hiyo ni sababu  endelevu,kama ilikuwa finyu zaman itakuwa finyu Tu na sasa hivi,so hapo Op tena.... 


3.lakin ukiachana na sababu za juu hizo Mbili,

Usiwe na shida au na doubt yeyote juu ya kuweza ku push...

Iwe clear kabisaa hauna pingamiz nyingine,yaan njia ifunguke,mtoto awe kageuka vizur,kashuka vizuri.....


N:B Kwanin TUNAOGOPA MTU ASIZAE KAWAIDA Baada ya OP???? 

Hofu kubwa ni KUCHANIKA kwa mshono uliopo kwenye kizazi(rupture of uterus).


Kizazi KIKICHANIKA,

1.Mama anaweza poteza mtoto maana

2.anaweza Tolewa kizazi maana kinakuwa kinamwaga sana damu na wakat mwingine  anaweza shonwa damu zikawa hazikati na kulazimu kung'olewa kizazi.

3.Kumwaga Damu kunasababisha VIFO VINGI sana vya hawa wamama(PPH).


USHAURI kwa Wenye MISHONO(PREVIOUS SCAR)A


1.usiige kisa mtu fulani aliPush japo alikuwa na mshono na wewe Unataka


2.ukiwa na Mshono Mapema mpange na Dr wako Kifuatacho juu ya Kujifungua kwako,na kama ni UPASUAJI,basi mapema tareh ikifika Nenda,hutakiwi Kusubir uchungu.


3.Epuka Kupewa dawa na shangazi,Bibi,sijui mkunga wa mtaan,Dawa za Ku boost uchungu uchanganye,Hizi huwa zinafanya UCHUNGU Mkali sana na kama una mshono,Rahis sana kuchanika.


4.epuka Kupata MIMBA kabla Mwanao Hajafika MIAKA MIWILI.


#trialofscar #uzazi #caesariansection

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code