Afyaclass Bongo Social UGONJWA WA KICHOCHO,VISABABISHI VYAKE,DALILI,VIPIMO,MATIBABU NA MADHARA YAKE

 UGONJWA WA KICHOCHO HUSABABISHWA NA NINI?


Huu ni ugonjwa ambao husababishwa na vimelea ambao kwa kitaalam hujulikana kama aina ya SCHISTOSOMA.


MTU HUAMBUKIZWAJE?


Ugonjwa huu huambikizwa kupitia maji yenye vimelea hivi vya SCHISTOSOMA vinapopenya kwenye Ngozi ya mtu.


DALILI ZA UGONJWA WA KICHOCHO


  1. Kupata maumivu makali ya Tumbo
  2. Kujisaidia kinyesi chepesi kilichochanganyika na Damu
  3. Kukojoa Damu wakati wa haja ndogo
  4. Kupatwa na hali ya kikihozi
  5. Kupata Homa
  6. Kuanza kuwashwa sana na Ngozi
  7. Pamoja na mwili kuchoka kupita kiasi

VIPIMO VYA KICHOCHO NI PAMOJA NA

  • kipimo cha Damu
  • Kipimo cha Mkojo
  • Kupigwa X-ray ya tumbo
  • Au kupigwa Ultrasound ya Tumbo


MATIBABU YA UGONJWA WA KICHOCHO


Ugonjwa huu hutibika kupitia Dawa aina ya PRAZIQUANTEL ambapo mgonjwa atapewa Dose moja tu,hilo tatizo litaisha.


MADHARA YA UGONJWA WA KICHOCHO


Ni pamoja na kupatwa na Magonjwa ya Figo pamoja na Saratani ya Kibofu cha Mkojo.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




You, Mehreen and others

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD