Daktari feki anayefanya upasuaji wa mabusha na Tezi Dume akamatwa Njombe

#1

Polisi Mkoani Njombe inamshikilia Muhamed Abdalah Athuman (43) Mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Wilayani Ludewa, Mtaalamu wa tiba asiyekuwa na vyeti kwa tuhuma za kufanya upasuaji wa mabusha na tezi dume huku pia akiwa na box zaidi ya 23 za vifaa tiba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Hassan Banga amethibitisha kushikiliwa kwa Mtuhumiwa huyo pamoja na Ibarahim Mgimba (25) ambaye ni Dereva wa bodaboda akituhumiwa kuhusika kusafirisha bidhaa na kuzificha wakati Polisi wakimtafuta Mtuhumiwa.

“Huyu anasema ni Mtaalamu wa tiba lakini hana vyeti tumemkamata akiwa na vifaa tiba mbalimbali box zaidi ya 23 na amekuwa akiwatibu Watu akifanya upasuaji wa kuondoa mabusha na upasuaji wa tezi dume bila kuwa na vyeti”

Consultation ya Afya Moja kwa Moja

Mimi ni Dr. Ombeni Mkumbwa. Nakupa ushauri wa kitaalamu kuhusu tatizo lolote la kiafya kwa siri, haraka na uhakika.

WhatsApp

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code