Afyaclass Bongo Social TANZIA:Boaz Sanga,Mwanachuo St. Augustine (SAUT) afariki kwa kuzama Ziwa Viktoria

TANZIA:Boaz Sanga,Mwanachuo St. Augustine (SAUT) afariki kwa kuzama Ziwa Viktoria.

Mwanachuo wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha St. Augustine (SAUT), Mwanza, Boaz Sanga amefariki dunia baada ya kuzama wakati akiogelea kwenye Ziwa Viktoria, tukio lililotokea jana, Mei 1, 2024.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mwanza, SF Kamila Laban, amesema kijana huyo alifikwa na mauti katika eneo la Sweya alikokuwa anaogelea na wenzake baada ya kuingia kwenye eneo lenye kina kirefu.

SACF Kamila amesema baada ya Zimamoto kufika eneo la tukio zoezi la kumtafuta liliendelea hadi usiku bila mafanikio na leo Mei 02, 2024 wamefanikiwa kuupata mwili wake pembezoni mwa mawe ziwani hapo.

You, Mehreen and others

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD