Vyakula vya kuongeza damu mwilini Afyaclass Bongo Social •

Vyakula vya kuongeza damu mwilini 

KUONGEZA WINGI WA DAMU

VYAKULA VYA KUONGEZA DAMU KAMA UNA TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU

Proteins ndani ya Chembe hai nyekundu za damu maarufu kama Haemoglobin(hb) huweza kutumika katika kuangalia kiwango cha Damu ambacho mtu anacho. 

Na kwa kutumia hizo tunaweza kusema mtu huyu ana damu nyingi au ana upungufu wa Damu mwilini.

Kiwango cha kawaida cha Damu kwenye mwili wa binadamu hutofautiana kati ya jinsia moja na nyingine, hapa namaanisha mwanamke na mwanaume,katika kuangalia kiwango sahihi cha Damu ni tofauti kwa jinsia hizi mbili. 

Lakini pia ni tofauti kwa Mama Mjamzito kutokana na hatari ya kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

✓ Mwanaume kiwango sahihi cha Damu ni g/dl 13.5 mpaka 17.5

✓ Kwa mwanamke ambaye si mjamzito,kiwango sahihi cha Damu ni g/dl 12.0 mpaka  15.5, hali hii ya kuwa na kiwango kidogo cha Damu ukilinganisha na mwanaume hutokana na mwanamke kupoteza damu kila anapoingia period au anapopata hedhi

✓ Na kwa mama Mjamzito,kiwango sahihi cha damu hutakiwa kuanzia g/dl 11 au 12 kwenda juu.

Sababu za Upungufu wa Damu Mwilini

BAADHI YA SABABU ZA MTU KUWA NA UPUNGU WA DAMU MWILINI NI PAMOJA NA;

  • Ukosefu wa Madini ya Chuma mwilini
  • Ukosefu wa Vitamin mwilini  hasa hasa Vitamin B12
  • Upungufu wa damu mwilini kwa sababu ya magonjwa kama Kansa, Magonjwa ya Figo na Ukimwi
  • Upungufu wa damu mwilini kutokana na ugonjwa wa MALARIA
  • Upungufu wa damu mwilini kutokana na hali ya damu kushindwa kuganda kwa kitaalam huitwa Coagulopathy
  • Matumizi ya baadhi ya dawa,Sumu,makemiko au magonjwa ambayo huathiri utengenezaji wa Seli nyekundu za Damu(Red blood cells)
  • Tatizo la selimundu au Sickle cell anemia
  • N.K

Vyakula vya kuongeza damu mwilini

BAADHI YA VYAKULA VYA KUONGEZA DAMU MWILINI NI PAMOJA NA;

1. Baadhi ya matunda husaidia kwa kiwango kikubwa katika kuongeza damu mwilini, na matunda hayo ni pamoja na; Matunda Damu, Zabibu, machungwa, maembe,nyanya pamoja na Strawberries.

2. Ulaji wa mbogamboga kama vile matembele,Spinach au Sukuma wiki pia husaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza damu. Pendelea kula mboga mboga hasa hasa mboga jamii ya matembele zitakusaidia sana kuongeza wingi wa damu mwilini.

3. Pendelea kula vyakula vywenye vyanzo vizuri vya Madini aina ya Chuma Kama vile; maharage,nyama ikiwemo maini.

4. Matumizi ya juisi mbali mbali kama juisi ya Rozella,BeetRoot,Tikiti maji, karoti au nyanya huongeza Damu kwa kasi sana. Hivo pendelea kutumia aina hizi za Juisi.

5. Zipo njia nyingine za kuongeza Damu katika mwili wa Binadamu kama vile; matumizi ya Dawa aina ya FEFOL ambapo hapa kuna kiwango kikubwa cha madini ya chuma ambayo yatasaidia utengenezwaji wa haraka wa damu,na hivo kuongeza kiwango cha damu mwilini.

Endapo Mgonjwa yupo katika hali ya hatari ya kuishiwa na damu,zipo njia za haraka kama kutundikiwa damu moja kwa moja kwa njia ya Drip.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Mama baada ya kujifungua tendo la ndoaAfyaclass Bongo Social •

Mama baada ya kujifungua kushiriki tendo la ndoa ni baada ya Muda Gani?

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza hivi tunatakiwa kukaa muda gani ndipo tuanze kufanya mapenzi baada ya Kujifungua?.

Muda sahihi wa kufanya mapenzi baada ya mama Mjamzito kujifungua ni upi?

Je,mama ambaye kajifungua kwa Upasuaji asubiri Muda gani ndipo aanze kushiriki tendo?

Haya ni Maswali ambayo tumekuwa tukikutana nayo mara kwa mara, kwa kuliona hilo,leo tumeamua kukuelezea muda sahihi ambao unashauriwa kitaalam kushiriki tendo la ndoa toka Ujifungue.

Muda sahihi wa kuanza kushiriki tendo la ndoa baada ya kujifungua ni kuanzia Kipindi cha siku 42 au wiki 6 kwani hapa ndyo kipindi kila kitu ikiwemo via vya uzazi vimerudi katika hali ya kawaida. Kipindi hiki hujulikana kitaalam kama postpartum period.

Baada ya kujifungua, mama anaweza kushiriki tendo la ndoa wakati atakapojisikia vizuri na kuwa tayari, lakini kwa kawaida madaktari wanapendekeza kusubiri angalau wiki 4 hadi 6

Lakini pia ikifika siku hizo 42 au wiki 6 sio lazima mwanamke kuanza kulazimishwa kufanya mapenzi kama bado anaona hajawa sawa. Hivo kuna Umuhimu pia wakujua hali ya mwenzako hata kama wiki 6 zimeisha.

Sababu za Kusubiri

Zipo Sababu za kusubiri mpaka kipindi hiki kifike,Sababu hizo ni pamoja na:

  1. Kupona kwa mwili – Ikiwa mama alijifungua kwa njia ya kawaida, inahitaji muda kwa uke na perineum kupona, hasa ikiwa kulikuwa na michubuko au mshono kutokana na mama kuongezewa njia wakati wa kujifungua au kwa kitaalam(episiotomy). Na Ikiwa alifanyiwa upasuaji kwa ajili ya kujifungua yaani C-section kidonda kinahitaji muda wa kupona vizuri.

  2. Kupungua hatari ya maambukizi – Katika wiki chache za kwanza baada ya kujifungua, mlango wa kizazi bado uko wazi, na mama anaweza kuwa na damu ya lochia, ambayo huongeza hatari ya kupata maambukizi. Hapa nazungumzia maambukizi kama vile PID n.k

  3. Kurejea kwa homoni na hamu ya tendo la ndoa – Baadhi ya wanawake wanapitia mabadiliko ya homoni yanayoweza kupunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa, hasa kama wananyonyesha. Hivo kusubri kwa muda kidogo husaidia hamu ya tendo la ndoa kurudi kabla ya kuanza tena kushiriki.

  4. Maumivu na ukavu wa uke – Baadhi ya wanawake katika kipindi hiki wanapata tatizo la ukavu wa uke kutokana na kupungua kwa kichocheo cha estrogeni, jambo linaloweza kusababisha maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa.

Ili kuhakikisha kuwa mama yuko tayari kushiriki tendo la ndoa baada ya kujifungua, ni muhimu kuwasiliana na daktari wake kama huelewi chochote na pia kujadiliana na mwenza wako ili kuwe na uelewa wa pamoja. Ikiwa mama anahisi maumivu au kutokuwa tayari hata baada ya muda huo, ni vyema kusubiri hadi atakapojisikia vizuri.

HIVO basi, kipindi sahihi cha kuanza kufanya mapenzi baada ya mama Kujifungua ni angalau wiki 4 hadi 6 au Siku 42 toka ajifungue hapa tunazungumzia kipindi cha Postpartum period ambapo Via vya uzazi na vitu vingine hurudi kwenye hali yake ya kawaida baada ya kujifungua, Lakini pia na pale ambapo Mama atakapoona mwenyewe kakaa sawa hata kama amefikisha siku 42.

Hii Inatoa ANGALIZO kwamba; Hata kama mwanamke kamaliza siku 42, na bado hajawa sawa au hajajasikia kuanza kufanya Mapenzi,asilazimishwe,kwani yeye mwenyewe ndyo anajua mwili wake jinsi anavyojisikia.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!

0 Comment

Ugonjwa wa Fistula,Chanzo,Dalili Zake na TibaAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Fistula,Chanzo,Dalili Zake na Tiba

Fistula ni nini?

Fistula ni uwazi,tundu au njia isiyotakiwa kati ya sehemu mbili za mwili, kama vile kwenye viungo vya mwili, mishipa ya damu au utumbo.  

Hali hii ya kuwepo kwa uwazi au tundu lisilotakiwa ndyo husababisha vitu kama Mkojo,Haja kubwa au Usaha kutoka Sehemu ambapo havitakiwi kupita.

Mfano; Kutoa Haja kubwa(kinyesi) kwenye Sehemu ya haja ndogo n.k.

Fistula inaweza kusababishwa na Sababu mbali mbali ikiwemo; Kupata majeraha,maambukizi,upasuaji n.k. tutaangalia vizuri kwenye Makala hii ya Leo chanzo chake.

Kitu ambacho watu Wengi hawajui ni kwamba,Wengi wanafikiri Ugonjwa wa Fistula ni kwa Wanawake Tu, Hapana! Ugonjwa wa Fistula huweza kutokea kwa Mwanamke na Mwanaume pia.

Tutazame Aina za Fistula,

Aina za Fistula

Zipo aina nyingi za Fistula,ila baadhi ya aina hizo ni pamoja na hizi;

1. Anal fistula

2. Arteriovenous (AV) fistula

3. Vaginal fistula,Pamoja na aina nyingine nyingi,

Hii Vaginal Fistula, Ndyo aina ya Fistula ambayo huwapata Wanawake Pekee, 

Na aina hii imegawanywa kwenye makundi mbali mbali ikiwemo;

  • RectoVaginal Fistula(RVF)- Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya Njia ya Haja Kubwa na Uke
  • ColoVaginal Fistula(CVF)-Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya utumbo mkubwa na Uke
  • VesicoVaginal Fistula (VVF)- Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya kibofu cha Mkojo na Uke au Njia ya Mkojo ya mwanamke

Chanzo cha Ugonjwa wa fistula

Sababu za kuwa na Fistula hutofautiana kulingana na aina ya fistula uliyo nayo.  Ila Kwa ujumla, sababu zinazowezekana kuwa chanzo cha Fistula ni pamoja na:

1. Kupata maambukizi

Maambukizi ya Magonjwa mbali mbali kama HIV na magonjwa mengine ya Zinaa,uwepo wa Ugonjwa wa Saratani,Ugonjwa wa TB, na Magonjwa katika Utumbo ambapo kitaalam tunasema Intestinal diseases huweza kupelekea Mtu kuwa na tatizo la Fistula.

Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) yanaweza kuongeza hatari ya kupata fistula, hasa fistula ya njia ya haja kubwa(Anal Fistula), Hii ni kutokana na athari zake kwenye mfumo wa kinga, hivyo kufanya watu kushambuliwa zaidi na maambukizo ambayo yanaweza kusababisha fistula katika eneo la anorectal; Hali  hii inachukuliwa kuwa wasiwasi mkubwa kwa watu wanaoishi na VVU. 

2. Kuumia au kupata Majeraha kwenye baadhi ya Sehemu za Mwili(Trauma/injury)

3. Madhara baada ya Upasuaji(Complication of surgery).

Mfano; Majeraha au Tundu ambalo hutokea wakati Mwanamke anajifungua,ambapo linaweza kusabibishwa wakati wa upasuaji,au mgandamizo wa mtoto wakati anatoka,au wakati mama anasaidiwa kutolewa mtoto wakati anajifungua kwa Njia ya kawaida,ambapo hii huhusisha matumizi ya vifaa vyenye ncha kali, Mfano wakati wa procedure inaitwa Episiotomy au Forceps Delivery.

4. Madhara baada ya Matibabu yanayohusisha Mionzi ambapo kitaalam Hujulikana kama RADIATION THERAPY n.k.

Dalili za Ugonjwa wa Fistula,

Dalili za Fistula huweza kutofautiana kulingana na aina ya Fistula,ila kwa Ujumla,Dalili kama hizi huweza kutokea kwa Mgonjwa;

- Kupata Maumivu ndani au kuzunguka eneo la haja kubwa kwenye anus au Rectum, Eneo hili kuvimba,kuwa jekundu zaidi,pamoja na kutoa usaha au haja kubwa pembeni au karibu na tundu la haja kubwa,

Hizi ni dalili za Fistula ya njia ya haja kubwa au Anal fistula.

- Dalili zingine ni kutokwa na Mkojo pasipo Kujizuia (Dalili kubwa na kiashiria kikubwa cha Ugonjwa wa Fistula hasa kwa Wanawake)

- Uchafu wa Haja Kubwa(Kinyesi) kutoka katika Njia ya Haja Ndogo, ukeni,au sehemu nyingine yeyote mbali na Sehemu yake yakawaida

- kuwa na Harufu ya Mkojo mda wote (Urine Smell) hii ni kwa Sababu ya Ule mkojo unaotoka bila wewe kupenda.

- Wengine wakitembea huanza kubadilika tofauti na kawaida yao, Mfano unakuta Mgonjwa huanza kutembea kama Amepinda

- Mtu kuwa na Harufu ya Kinyesi

- Pamoja na dalili zingine kama vile; kupata homa,maumivu makali ya Ubavu na Tumbo chini ya kitovu n.k.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ugonjwa wa tb unasababishwa na nini Afyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa tb unasababishwa na nini 

Ugonjwa wa Tb au Kifua kikuu,ambapo kwa kitaalamu Zaidi hujulikana kama TUBERCULOSIS ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na maambukizi ya bacteria kwenye maeneo kama vile kwenye Mapafu.

Bakteria anayesababisha Ugonjwa huu wa kifua kikuu hujulikana kama mycobacterium tuberculosis. Kifua kikuu kinaweza kuambukiza wanyama pia kama vile ng'ombe n.k,

Ikiwa Mnyama kama Ng'ombe ana maambukizi haya, bacteria wa kifua kikuu wanaweza pia kutoka kwenye ng'ombe na kupitishwa kwenda kwa binadamu kwa njia mbali mbali ikiwemo kupitia maziwa yaliyoambukizwa. 

 ➖ Ugonjwa wa Kifua kikuu kwa kawaida huenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia nyingi ikiwemo wakati mtu mwenye Ugonjwa huu anapopiga chafya, kukohoa au kutema mate.  Kutoka kwenye mapafu, bakteria hawa wanaweza kuenea pia kwenye sehemu zingine za mwili na kusababisha kifua Kikuu,

Haya hapa ni baadhi ya Maeneo ambapo Bacteria wa Kifua kikuu huweza kuathiri mbali na Mapafu;

  • Figo
  • Ini.
  • Ubongo na Uti wa Mgongo, bacteria hawa huweza kushambulia Kwenye Majimaji yanayozunguka ubongo pamoja na uti wa mgongo.
  • Misuli ya moyo.
  • Sehemu za siri.
  • Kwenye lymph nodes.
  • Kwenye Mifupa
  • Joints
  • Kwenye Ngozi.
  • Kwenye damu, hapa nazungumzia kwenye Kuta za mishipa ya damu.
  • Kwenye koo,eneo la Kisanduku cha sauti(voicebox) pia huitwa larynx

➖ Kuenea kwa bakteria ni polepole, Na Wakati mwingine inaweza kuchukua muda hata wa miaka bila mtu kuonyesha dalili yoyote ya Kifua kikuu lakini ana vimelea Ndani.  Kudhoofika kwa kinga ya mwili kwa sababu mbali mbali ikiwemo ya magonjwa kama vile UKIMWI husababisha maambukizi ya haraka ya Vimelea hivi vya TB au huweza kusababisha Bacteria waliopo ndani ya mwili kupata nafasi ya kuanza mashambulizi,na hapa ndipo dalili huanza kujitokeza kwa Mgonjwa,

 Lakini pia Watu wanaoishi katika nyumba zilizojaa watu, au kukaa kwenye msongamano mkubwa wa watu kama vile masokoni,kwenye daladala,kukosa lishe bora n.k, vyote hivi huweza kuhusishwa na maambukizi ya ugonjwa huu wa TB.


Dalili za Ugonjwa wa TB,Kifua kikuu

Dalili za Ugonjwa wa TB ni pamoja na hizi;

(1) Kupumua kwa shida sana

(2) kuwa na kikohozi kinachoendelea, kinachoambatana na makohozi yenye damu 

(3) Pia homa za usiku huibuka.

(4)  Kuanza kupungua uzito kwa kasi sana

(5) kupoteza rangi halisi ya Ngozi,

(6) mwili kukosa nguvu au kuwa dhaifu.

(7) Mwili kukonda sana baaada ya Kupata Ugonjwa wa kifua kikuu au TB

(8) Mwili kutoa sana Jasho hasa wakati wa Usku n.k

🔺KAMA UNA TATIZO HILI LA UGONJWA WA KIFUA KIKUU AU TB/TUBERCULOSIS NI BORA KWENDA HOSPTAL NA KUKUTANA NA WATAALAM WA AFYA WA BOBEZI KATIKA ENEO HILI ILI KUPATA TIBA SAHIHI NA SALAMA KWAKO.

ILA KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

0 Comment

Dalili za blood infection,Maambukizi kwenye DamuAfyaclass Bongo Social •

Dalili za blood infection,Maambukizi kwenye Damu

Blood Infection hapa tunazungumzia maambukizi ya vimelea mbali mbali vya Magonjwa kwenye damu, Vimelea hivo huweza kuwa Bacteria, Fangasi, Virusi n.k.

Maambukizi haya wakati mwingine huweza kufikia hatua ya kuitwa Sepsis.

Sepsis ni pale ambapo mwili wako unakuwa na mwitikio mkali dhidi ya maambukizi kwenye damu. Wakati huo mfumo wako wa kinga, ambao kwa kawaida unakukinga dhidi ya vijidudu, huanza kushambulia tishu za mwili wako.

Maambukizi ya damu, yanayojulikana kitaalamu kama sepsis, ni hali hatari inayotokea wakati mwili unajibu maambukizi kwa njia isiyo ya kawaida, kisha kusababisha kuvimba mwili mzima, kushindwa kwa viungo, au hata kifo. Sepsis inaweza kusababishwa na bakteria, virusi, fangasi, au vimelea vinavyosambaa kupitia damu na kuathiri viungo muhimu kama moyo, mapafu, figo, na ubongo.

Chanzo cha Maambukizi ya Damu

Maambukizi haya mara nyingi hutokana na:

Maambukizi ya bakteria – Kama vile Staphylococcus aureus, Escherichia coli (E. coli), na Streptococcus pneumoniae.n.k

Maambukizi ya virusi – Kama virusi vya dengue, HIV, na hepatitis.

Maambukizi ya fangasi – Kama Candida kwa watu wenye kinga dhaifu.

Maambukizi kutoka kwenye vidonda – Vidonda vikubwa au vidogo vinaweza kuwa mlango wa bakteria kuingia kwenye damu.

Maambukizi ya mfumo wa mkojo, mapafu, tumbo, au ngozi – Maambukizi kwenye damu mara nyingi huanza kutokana na maambukizi haya.

Matumizi ya vifaa vya matibabu – Katheta za mkojo, (IV lines), au mashine za kupumua zinaweza kusababisha maambukizi endapo hazitatunzwa vizuri kwenye hali ya Usafi wa hali ya juu.

Dalili za Maambukizi ya Damu

Dalili za maambukizi kwenye damu zinaweza kutofautiana, lakini kwa Ujumla huweza Kujumuisha:

1. Homa kali (joto la mwili kupanda au kushuka sana)

2. Mapigo ya moyo kuwa ya haraka (tachycardia)

3. Kupumua kwa shida au haraka

4. Mwili kutetemeka sana

5. Kuwa dalili kama za Kuchanganyikiwa au kupoteza fahamu

6. Kupata upele kwenye ngozi(Skin rashes)

7. Maumivu makali mwilini

8. Kukojoa kidogo sana kuliko kawaida au kutokukojoa kabsa.

9. Kuhisi kichefuchefu na kutapika

10. Kupata tatizo la Kuharisha

11. Mwili kuchoka sana, kuwa dhaifu au kukosa nguvu

12. Kutoa sana jasho

13. Kupata maumivu makali ikiwemo ya kichwa n.k

14. Kuhisi kizunguzungu

15. Kuhisi usingizi sana

16. Ngozi kuwasha sana n.k

Ukipata Dalili kama hizi,hakikisha Unapata Msaada mapema!

Tiba au Matibabu ya Maambukizi ya Damu

Matibabu ya maambukizi kwenye damu yanahitaji hatua za haraka ili kuokoa maisha hasa ikiwa ni Sepsis. Njia kuu za matibabu ni hutegemea na chanzo husika,Mfano; Matumizi ya Antibiotiki -kama chanzo ni maambukizi ya bakteria.n.k.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Dalili za chuchu kuuma,Chanzo na TibaAfyaclass Bongo Social •

Dalili za chuchu kuuma,Chanzo na Tiba

Dalili za Chuchu au Matiti kuuma huweza kutokea kwa Mwanamke na Mwanaume Pia,Katika Makala hii tutaangalia Sababu kubwa.

Je,Unapata Dalili hii ya Chuchu au Matiti Kuuma?

Hakikisha unapata Msaada wa haraka kutoka kwa Wataalam wa afya ikiwa:

  • Dalili ya Chuchu au Matiti kuuma Inaendelea kila siku kwa zaidi ya wiki kadhaa
  • Hutokea katika eneo moja Zaidi la titi lako 
  • Hali Inaonekana kuwa mbaya zaidi kadri Siku zinavyozidi kwenda 
  • Hukufanya ushindwe kufanya shughuli zako za kila siku
  • Hukufanya Ushindwe kulala Usiku n.k

Chanzo cha Chuchu Kuuma au Matiti kuuma

Kubadilika kwa viwango vya homoni kunaweza kusababisha mabadiliko katika mirija ya maziwa(ducts) au tezi za maziwa.  Mabadiliko haya katika ducts na tezi yanaweza kusababisha uvimbe wa matiti, ambayo inaweza kuwa chanzo cha maumivu ya matiti.

Pia Maumivu ya matiti yasiyo ya kawaida yanaweza kusababishwa na Mtu kuumia, upasuaji wa awali wa matiti au mambo mengine. 

Sababu hatarishi zinazoweza kuongeza uwezekano wa kupata dalili ya Chuchu au Matiti Kuuma(Risk factors)

Wakati mwingine, haiwezekani kutambua sababu halisi ya maumivu ya matiti, lakini baadhi ya mambo yanaweza kuongeza hatari ya kupata shida hii,

Kwa Wanawake, Mara nyingi Maumivu ya matiti ni ya kawaida zaidi kwa wale ambao hawajafikia Ukomo wa hedhi(menopause), ingawa inaweza kutokea pia baada ya kukoma kwa hedhi.  

Baadhi ya Wanawake hupata maumivu ya Chuchu au matiti wanapokuwa karibu na kipindi cha hedhi, Katika kipindi hiki Chuchu huweza kuuma.

Maumivu ya matiti yanaweza pia kutokea kwa wanaume hasa walio na tatizo la gynecomastia, Tatizo ambalo huhusisha Mwanaume kuwa na Matiti kama ya mwanamke na hii ni kwa Sababu ya kuongezeka kwa kiwango cha Tishu kwenye tezi za matiti yaani breast gland tissue ambapo chanzo chake kikubwa ni tatizo la hormone Imbalance,

Hapa kunakuwa na Uwiano usio sawa kati ya vichocheo vya estrogen pamoja na testosterone.

Pia Mara chache Sana,Dalili ya Chuchu kuuma au matiti huweza kuwa kiashiria cha tatizo la Saratani ya Matiti(Breast Cancer).

Zipo pia Sababu Zingine ambazo huweza kuongeza hatari ya Chuchu Kuuma au Matiti,Sababu hizo ni Pamoja na;

1. Kuwa na Matiti makubwa.

Tafiti zinaonyesha Watu wenye matiti makubwa huweza kupata Dalili za kuuma kwa Matiti Zaidi kulingana na Ukubwa wa Matiti Yao,

Na mara nyingi dalili hii ya Kuuma kwa Matiti huambatana na dalili zingine kama vile; kupata maumivu ya Shingo,Mabega pamoja na Mgongo.

2. Upasuaji wa Matiti(Breast surgery). 

Maumivu ya matiti yanayohusiana na upasuaji wa matiti na Utengenezaji wa kovu wakati mwingine yanaweza kudumu baada ya Sehemu ulipopasuliwa kupona.

3. Tatizo la Fatty acid imbalance. 

Kukosekana kwa usawa wa asidi inayotokana na mafuta ndani ya seli kunaweza kuathiri unyeti wa tishu za matiti kwa homoni zinazozunguka, hali ambayo huweza kuleta Maumivu ya Matiti.

4. Matumizi ya baadhi ya Dawa.

Baadhi ya Dawa za hormones, ikiwa ni pamoja na baadhi ya dawa za tatizo la kutokubeba mimba na vidonge vya kuzuia Ujauzito maarufu kama Vidonge vya uzazi wa Mpango(oral birth control pills) vinaweza kuhusishwa na maumivu ya matiti.

Lakini pia Tafiti zinaonyesha hata baadhi ya Dawa zingine ikiwemo dawa za Presha pamoja na baadhi ya antibiotics huweza kusababisha dalili hii ya maumivu ya Matiti.

5. Matumizi ya kafeini kupita kiasi. 

Ingawa utafiti zaidi unahitajika, baadhi ya watu wanaona Unafuu mkubwa kwenye maumivu ya matiti wanapopunguza au kuacha kabsa matumizi ya vitu vyenye kafeini.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD