Dalili za blood infection,Maambukizi kwenye Damu

Dalili za blood infection,Maambukizi kwenye Damu

#1

Dalili za blood infection,Maambukizi kwenye Damu

Blood Infection hapa tunazungumzia maambukizi ya vimelea mbali mbali vya Magonjwa kwenye damu, Vimelea hivo huweza kuwa Bacteria, Fangasi, Virusi n.k.

Maambukizi haya wakati mwingine huweza kufikia hatua ya kuitwa Sepsis.

Sepsis ni pale ambapo mwili wako unakuwa na mwitikio mkali dhidi ya maambukizi kwenye damu. Wakati huo mfumo wako wa kinga, ambao kwa kawaida unakukinga dhidi ya vijidudu, huanza kushambulia tishu za mwili wako.

Maambukizi ya damu, yanayojulikana kitaalamu kama sepsis, ni hali hatari inayotokea wakati mwili unajibu maambukizi kwa njia isiyo ya kawaida, kisha kusababisha kuvimba mwili mzima, kushindwa kwa viungo, au hata kifo. Sepsis inaweza kusababishwa na bakteria, virusi, fangasi, au vimelea vinavyosambaa kupitia damu na kuathiri viungo muhimu kama moyo, mapafu, figo, na ubongo.

Chanzo cha Maambukizi ya Damu

Maambukizi haya mara nyingi hutokana na:

Maambukizi ya bakteria – Kama vile Staphylococcus aureus, Escherichia coli (E. coli), na Streptococcus pneumoniae.n.k

Maambukizi ya virusi – Kama virusi vya dengue, HIV, na hepatitis.

Maambukizi ya fangasi – Kama Candida kwa watu wenye kinga dhaifu.

Maambukizi kutoka kwenye vidonda – Vidonda vikubwa au vidogo vinaweza kuwa mlango wa bakteria kuingia kwenye damu.

Maambukizi ya mfumo wa mkojo, mapafu, tumbo, au ngozi – Maambukizi kwenye damu mara nyingi huanza kutokana na maambukizi haya.

Matumizi ya vifaa vya matibabu – Katheta za mkojo, (IV lines), au mashine za kupumua zinaweza kusababisha maambukizi endapo hazitatunzwa vizuri kwenye hali ya Usafi wa hali ya juu.

Dalili za Maambukizi ya Damu

Dalili za maambukizi kwenye damu zinaweza kutofautiana, lakini kwa Ujumla huweza Kujumuisha:

1. Homa kali (joto la mwili kupanda au kushuka sana)

2. Mapigo ya moyo kuwa ya haraka (tachycardia)

3. Kupumua kwa shida au haraka

4. Mwili kutetemeka sana

5. Kuwa dalili kama za Kuchanganyikiwa au kupoteza fahamu

6. Kupata upele kwenye ngozi(Skin rashes)

7. Maumivu makali mwilini

8. Kukojoa kidogo sana kuliko kawaida au kutokukojoa kabsa.

9. Kuhisi kichefuchefu na kutapika

10. Kupata tatizo la Kuharisha

11. Mwili kuchoka sana, kuwa dhaifu au kukosa nguvu

12. Kutoa sana jasho

13. Kupata maumivu makali ikiwemo ya kichwa n.k

14. Kuhisi kizunguzungu

15. Kuhisi usingizi sana

16. Ngozi kuwasha sana n.k

Ukipata Dalili kama hizi,hakikisha Unapata Msaada mapema!

Tiba au Matibabu ya Maambukizi ya Damu

Matibabu ya maambukizi kwenye damu yanahitaji hatua za haraka ili kuokoa maisha hasa ikiwa ni Sepsis. Njia kuu za matibabu ni hutegemea na chanzo husika,Mfano; Matumizi ya Antibiotiki -kama chanzo ni maambukizi ya bakteria.n.k.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

REPLY


image quote pre code