Mama baada ya kujifungua kushiriki tendo la ndoa ni baada ya Muda Gani?
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza hivi tunatakiwa kukaa muda gani ndipo tuanze kufanya mapenzi baada ya Kujifungua?.
Muda sahihi wa kufanya mapenzi baada ya mama Mjamzito kujifungua ni upi?
Je,mama ambaye kajifungua kwa Upasuaji asubiri Muda gani ndipo aanze kushiriki tendo?
Haya ni Maswali ambayo tumekuwa tukikutana nayo mara kwa mara, kwa kuliona hilo,leo tumeamua kukuelezea muda sahihi ambao unashauriwa kitaalam kushiriki tendo la ndoa toka Ujifungue.
Muda sahihi wa kuanza kushiriki tendo la ndoa baada ya kujifungua ni kuanzia Kipindi cha siku 42 au wiki 6 kwani hapa ndyo kipindi kila kitu ikiwemo via vya uzazi vimerudi katika hali ya kawaida. Kipindi hiki hujulikana kitaalam kama postpartum period.
Baada ya kujifungua, mama anaweza kushiriki tendo la ndoa wakati atakapojisikia vizuri na kuwa tayari, lakini kwa kawaida madaktari wanapendekeza kusubiri angalau wiki 4 hadi 6.
Lakini pia ikifika siku hizo 42 au wiki 6 sio lazima mwanamke kuanza kulazimishwa kufanya mapenzi kama bado anaona hajawa sawa. Hivo kuna Umuhimu pia wakujua hali ya mwenzako hata kama wiki 6 zimeisha.
Sababu za Kusubiri
Zipo Sababu za kusubiri mpaka kipindi hiki kifike,Sababu hizo ni pamoja na:
-
Kupona kwa mwili – Ikiwa mama alijifungua kwa njia ya kawaida, inahitaji muda kwa uke na perineum kupona, hasa ikiwa kulikuwa na michubuko au mshono kutokana na mama kuongezewa njia wakati wa kujifungua au kwa kitaalam(episiotomy). Na Ikiwa alifanyiwa upasuaji kwa ajili ya kujifungua yaani C-section kidonda kinahitaji muda wa kupona vizuri.
-
Kupungua hatari ya maambukizi – Katika wiki chache za kwanza baada ya kujifungua, mlango wa kizazi bado uko wazi, na mama anaweza kuwa na damu ya lochia, ambayo huongeza hatari ya kupata maambukizi. Hapa nazungumzia maambukizi kama vile PID n.k
-
Kurejea kwa homoni na hamu ya tendo la ndoa – Baadhi ya wanawake wanapitia mabadiliko ya homoni yanayoweza kupunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa, hasa kama wananyonyesha. Hivo kusubri kwa muda kidogo husaidia hamu ya tendo la ndoa kurudi kabla ya kuanza tena kushiriki.
-
Maumivu na ukavu wa uke – Baadhi ya wanawake katika kipindi hiki wanapata tatizo la ukavu wa uke kutokana na kupungua kwa kichocheo cha estrogeni, jambo linaloweza kusababisha maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Ili kuhakikisha kuwa mama yuko tayari kushiriki tendo la ndoa baada ya kujifungua, ni muhimu kuwasiliana na daktari wake kama huelewi chochote na pia kujadiliana na mwenza wako ili kuwe na uelewa wa pamoja. Ikiwa mama anahisi maumivu au kutokuwa tayari hata baada ya muda huo, ni vyema kusubiri hadi atakapojisikia vizuri.
HIVO basi, kipindi sahihi cha kuanza kufanya mapenzi baada ya mama Kujifungua ni angalau wiki 4 hadi 6 au Siku 42 toka ajifungue hapa tunazungumzia kipindi cha Postpartum period ambapo Via vya uzazi na vitu vingine hurudi kwenye hali yake ya kawaida baada ya kujifungua, Lakini pia na pale ambapo Mama atakapoona mwenyewe kakaa sawa hata kama amefikisha siku 42.
Hii Inatoa ANGALIZO kwamba; Hata kama mwanamke kamaliza siku 42, na bado hajawa sawa au hajajasikia kuanza kufanya Mapenzi,asilazimishwe,kwani yeye mwenyewe ndyo anajua mwili wake jinsi anavyojisikia.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Karibu Sana..!!!
REPLY
image quote pre code