Dalili za chuchu kuuma,Chanzo na Tiba
Je,Unapata Dalili hii ya Chuchu au Matiti Kuuma?
Hakikisha unapata Msaada wa haraka kutoka kwa Wataalam wa afya ikiwa:
- Dalili ya Chuchu au Matiti kuuma Inaendelea kila siku kwa zaidi ya wiki kadhaa
- Hutokea katika eneo moja Zaidi la titi lako
- Hali Inaonekana kuwa mbaya zaidi kadri Siku zinavyozidi kwenda
- Hukufanya ushindwe kufanya shughuli zako za kila siku
- Hukufanya Ushindwe kulala Usiku n.k
Chanzo cha Chuchu Kuuma au Matiti kuuma
Kubadilika kwa viwango vya homoni kunaweza kusababisha mabadiliko katika mirija ya maziwa(ducts) au tezi za maziwa. Mabadiliko haya katika ducts na tezi yanaweza kusababisha uvimbe wa matiti, ambayo inaweza kuwa chanzo cha maumivu ya matiti.
Pia Maumivu ya matiti yasiyo ya kawaida yanaweza kusababishwa na Mtu kuumia, upasuaji wa awali wa matiti au mambo mengine.
Sababu hatarishi zinazoweza kuongeza uwezekano wa kupata dalili ya Chuchu au Matiti Kuuma(Risk factors)
Wakati mwingine, haiwezekani kutambua sababu halisi ya maumivu ya matiti, lakini baadhi ya mambo yanaweza kuongeza hatari ya kupata shida hii,
Kwa Wanawake, Mara nyingi Maumivu ya matiti ni ya kawaida zaidi kwa wale ambao hawajafikia Ukomo wa hedhi(menopause), ingawa inaweza kutokea pia baada ya kukoma kwa hedhi.
Baadhi ya Wanawake hupata maumivu ya Chuchu au matiti wanapokuwa karibu na kipindi cha hedhi, Katika kipindi hiki Chuchu huweza kuuma.
Maumivu ya matiti yanaweza pia kutokea kwa wanaume hasa walio na tatizo la gynecomastia, Tatizo ambalo huhusisha Mwanaume kuwa na Matiti kama ya mwanamke na hii ni kwa Sababu ya kuongezeka kwa kiwango cha Tishu kwenye tezi za matiti yaani breast gland tissue ambapo chanzo chake kikubwa ni tatizo la hormone Imbalance,
Hapa kunakuwa na Uwiano usio sawa kati ya vichocheo vya estrogen pamoja na testosterone.
Pia Mara chache Sana,Dalili ya Chuchu kuuma au matiti huweza kuwa kiashiria cha tatizo la Saratani ya Matiti(Breast Cancer).
Zipo pia Sababu Zingine ambazo huweza kuongeza hatari ya Chuchu Kuuma au Matiti,Sababu hizo ni Pamoja na;
1. Kuwa na Matiti makubwa.
Tafiti zinaonyesha Watu wenye matiti makubwa huweza kupata Dalili za kuuma kwa Matiti Zaidi kulingana na Ukubwa wa Matiti Yao,
Na mara nyingi dalili hii ya Kuuma kwa Matiti huambatana na dalili zingine kama vile; kupata maumivu ya Shingo,Mabega pamoja na Mgongo.
2. Upasuaji wa Matiti(Breast surgery).
Maumivu ya matiti yanayohusiana na upasuaji wa matiti na Utengenezaji wa kovu wakati mwingine yanaweza kudumu baada ya Sehemu ulipopasuliwa kupona.
3. Tatizo la Fatty acid imbalance.
Kukosekana kwa usawa wa asidi inayotokana na mafuta ndani ya seli kunaweza kuathiri unyeti wa tishu za matiti kwa homoni zinazozunguka, hali ambayo huweza kuleta Maumivu ya Matiti.
4. Matumizi ya baadhi ya Dawa.
Baadhi ya Dawa za hormones, ikiwa ni pamoja na baadhi ya dawa za tatizo la kutokubeba mimba na vidonge vya kuzuia Ujauzito maarufu kama Vidonge vya uzazi wa Mpango(oral birth control pills) vinaweza kuhusishwa na maumivu ya matiti.
Lakini pia Tafiti zinaonyesha hata baadhi ya Dawa zingine ikiwemo dawa za Presha pamoja na baadhi ya antibiotics huweza kusababisha dalili hii ya maumivu ya Matiti.
5. Matumizi ya kafeini kupita kiasi.
Ingawa utafiti zaidi unahitajika, baadhi ya watu wanaona Unafuu mkubwa kwenye maumivu ya matiti wanapopunguza au kuacha kabsa matumizi ya vitu vyenye kafeini.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
REPLY
image quote pre code