Ugonjwa wa Fistula,Chanzo,Dalili Zake na Tiba

Ugonjwa wa Fistula,Chanzo,Dalili Zake na Tiba

#1

Ugonjwa wa Fistula,Chanzo,Dalili Zake na Tiba

Fistula ni nini?

Fistula ni uwazi,tundu au njia isiyotakiwa kati ya sehemu mbili za mwili, kama vile kwenye viungo vya mwili, mishipa ya damu au utumbo.  

Hali hii ya kuwepo kwa uwazi au tundu lisilotakiwa ndyo husababisha vitu kama Mkojo,Haja kubwa au Usaha kutoka Sehemu ambapo havitakiwi kupita.

Mfano; Kutoa Haja kubwa(kinyesi) kwenye Sehemu ya haja ndogo n.k.

Fistula inaweza kusababishwa na Sababu mbali mbali ikiwemo; Kupata majeraha,maambukizi,upasuaji n.k. tutaangalia vizuri kwenye Makala hii ya Leo chanzo chake.

Kitu ambacho watu Wengi hawajui ni kwamba,Wengi wanafikiri Ugonjwa wa Fistula ni kwa Wanawake Tu, Hapana! Ugonjwa wa Fistula huweza kutokea kwa Mwanamke na Mwanaume pia.

Tutazame Aina za Fistula,

Aina za Fistula

Zipo aina nyingi za Fistula,ila baadhi ya aina hizo ni pamoja na hizi;

1. Anal fistula

2. Arteriovenous (AV) fistula

3. Vaginal fistula,Pamoja na aina nyingine nyingi,

Hii Vaginal Fistula, Ndyo aina ya Fistula ambayo huwapata Wanawake Pekee, 

Na aina hii imegawanywa kwenye makundi mbali mbali ikiwemo;

  • RectoVaginal Fistula(RVF)- Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya Njia ya Haja Kubwa na Uke
  • ColoVaginal Fistula(CVF)-Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya utumbo mkubwa na Uke
  • VesicoVaginal Fistula (VVF)- Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya kibofu cha Mkojo na Uke au Njia ya Mkojo ya mwanamke

Chanzo cha Ugonjwa wa fistula

Sababu za kuwa na Fistula hutofautiana kulingana na aina ya fistula uliyo nayo.  Ila Kwa ujumla, sababu zinazowezekana kuwa chanzo cha Fistula ni pamoja na:

1. Kupata maambukizi

Maambukizi ya Magonjwa mbali mbali kama HIV na magonjwa mengine ya Zinaa,uwepo wa Ugonjwa wa Saratani,Ugonjwa wa TB, na Magonjwa katika Utumbo ambapo kitaalam tunasema Intestinal diseases huweza kupelekea Mtu kuwa na tatizo la Fistula.

Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) yanaweza kuongeza hatari ya kupata fistula, hasa fistula ya njia ya haja kubwa(Anal Fistula), Hii ni kutokana na athari zake kwenye mfumo wa kinga, hivyo kufanya watu kushambuliwa zaidi na maambukizo ambayo yanaweza kusababisha fistula katika eneo la anorectal; Hali  hii inachukuliwa kuwa wasiwasi mkubwa kwa watu wanaoishi na VVU. 

2. Kuumia au kupata Majeraha kwenye baadhi ya Sehemu za Mwili(Trauma/injury)

3. Madhara baada ya Upasuaji(Complication of surgery).

Mfano; Majeraha au Tundu ambalo hutokea wakati Mwanamke anajifungua,ambapo linaweza kusabibishwa wakati wa upasuaji,au mgandamizo wa mtoto wakati anatoka,au wakati mama anasaidiwa kutolewa mtoto wakati anajifungua kwa Njia ya kawaida,ambapo hii huhusisha matumizi ya vifaa vyenye ncha kali, Mfano wakati wa procedure inaitwa Episiotomy au Forceps Delivery.

4. Madhara baada ya Matibabu yanayohusisha Mionzi ambapo kitaalam Hujulikana kama RADIATION THERAPY n.k.

Dalili za Ugonjwa wa Fistula,

Dalili za Fistula huweza kutofautiana kulingana na aina ya Fistula,ila kwa Ujumla,Dalili kama hizi huweza kutokea kwa Mgonjwa;

- Kupata Maumivu ndani au kuzunguka eneo la haja kubwa kwenye anus au Rectum, Eneo hili kuvimba,kuwa jekundu zaidi,pamoja na kutoa usaha au haja kubwa pembeni au karibu na tundu la haja kubwa,

Hizi ni dalili za Fistula ya njia ya haja kubwa au Anal fistula.

- Dalili zingine ni kutokwa na Mkojo pasipo Kujizuia (Dalili kubwa na kiashiria kikubwa cha Ugonjwa wa Fistula hasa kwa Wanawake)

- Uchafu wa Haja Kubwa(Kinyesi) kutoka katika Njia ya Haja Ndogo, ukeni,au sehemu nyingine yeyote mbali na Sehemu yake yakawaida

- kuwa na Harufu ya Mkojo mda wote (Urine Smell) hii ni kwa Sababu ya Ule mkojo unaotoka bila wewe kupenda.

- Wengine wakitembea huanza kubadilika tofauti na kawaida yao, Mfano unakuta Mgonjwa huanza kutembea kama Amepinda

- Mtu kuwa na Harufu ya Kinyesi

- Pamoja na dalili zingine kama vile; kupata homa,maumivu makali ya Ubavu na Tumbo chini ya kitovu n.k.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

REPLY


image quote pre code