Marufuku yatolewa kwa bidhaa za tumbaku na nikotiki zilizotiwa Ladha:WHO

Marufuku yatolewa kwa bidhaa za tumbaku na nikotiki zilizotiwa Ladha:WHO

#1

Marufuku yatolewa kwa bidhaa za tumbaku na nikotiki zilizotiwa Ladha:WHO



Nchi nyingi zimeona viwango vya kutisha vya matumizi ya sigara za kielektroniki miongoni mwa vijana.

Leo ni siku ya kimataifa ya kupiga marufuku matumizi ya tumbaku na bidhaa zake ambapo shirika la Afya duniani(WHO) limetoa wito kwa serikali zote duniani kupiga marufuku ladha zote katika bidhaa za tumbaku na nikotini ikiwemo sigara, shisha, na sigara za kielektroniki ili kuwalinda vijana dhidi ya uraibu na magonjwa hatari.

Kupitia chapisho jipya lililotolewa leo Geneva, Uswisi, WHO inasema ladha kama vile mentha, ubani na sukari pamba, huficha ukali wa bidhaa za tumbaku na kuzifanya zivutie vijana.” Ladha hizi si tu kwamba hufanya kuwa vigumu kuacha matumizi, bali pia zimehusishwa na magonjwa makubwa ya mapafu,” imesema WHO.

Nafasi ya ladha katika kuongeza mvutowa tumbaku na bidhaa zinazohusiana nazo.

Ladha katika tumbaku, nikotini na bidhaa zinazohusiana nazo huongeza mvuto hasa kwa watoto na vijana, na kuchangia kujaribu matumizi, kuanza kutumia na kuendelea kutumia kwa muda mrefu. Ladha zinageuzwa kuwa  mitego inayowavutia vijana.

Sigara, ambazo bado huwaua hadi nusu ya watumiaji wake, pia huuzwa zikiwa na ladha au huongezewa ladha

Ladha hizi zipo katika aina zote za bidhaa hizo na hutangazwa kwa nguvu, hasa kwa vijana. Pia, ladha hufanya kuwa vigumu kwa watumiaji kuacha.

Zaidi ya hayo, hakuna ushahidi kuwa ladha hizi ni salama kuvutwa, na zinaweza kusababisha madhara ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja kiafya.

“Ladha hizi zinaendeleza wimbi jipya la uraibu na zinapaswa kupigwa marufuku,”amesema Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO.

Kuelewa vipengele vya muundo wa bidhaa za tumbaku pamoja na athari zake zinazowezekana

Bidhaa za tumbaku, nikotini na zinazohusiana nazo hutengenezwa kwa makusudi ili kuwavutia watumiaji wapya hasa watoto na vijana na kuwafanya watumiaji waliopo waendelee kuzitumia.

Bidhaa hizi huundwa kuwa na mvuto wa macho, rahisi kutumia na kuvutia kihisia, huku zikificha madhara yake halisi. Viwanda vya tumbaku na nikotini hutumia vipengele kama vichujio, miundo midogo, rangi angavu na miundo ya kuvutia ili kupotosha mtazamo wa hatari na kuongeza uraibu.

Halikadhalika, baadhi ya bidhaa pia hutengenezwa ili zitumike kwa kificho, hali inayohujumu sera za maeneo yasiyo na moshi.

Zaidi ya nchi 50 zimepiga marufuku tumbaku zenye ladha.

Nchi kama Ubelgiji, Denmark na Lithuania zimeanza kuchukua hatua, na WHO inazitaka nchi nyingine kuiga mfano huo.Ladha ni mojawapo ya sababu kuu zinazowafanya vijana kujaribu kutumia bidhaa za tumbaku na nikotini.

Zikiwa zimeambatana na vifungashio vya kuvutia na matangazo kupitia mitandao ya kijamii, ladha zimeongeza mvuto bidhaa za tumbaku na nikotini.

“Tunaona kizazi kizima kikitekwa na uraibu wa nikotini kupitia bidhaa zenye ladha ya pipi na zile zisizotoa moshi zenye rangi kama upinde wa mvua,” amesema Dkt. Rüdiger Krech, Mkurugenzi wa Uhamasishaji Afya katika WHO.  “Hii si ubunifu ni udanganyifu. Na lazima tukomeshe.”

Kamoeni ya Siku ya kutotumia Tumbaku mwaka 2025  inataka serikali, wanaharakati vijana na mashirika ya kiraia kuzuia harakati za kuimarisha matumizi ya tumbaku ambapo Dkt. Krech anasema “Hatua zenu zinabadilisha sera na kuokoa maisha.”

WHO inasema kwa kuwa vifo vya watu milioni 8 kila mwaka vinahusiana na matumizi ya tumbaku, wakati wa kuchukua hatua ni sasa. Ladha, na viwanda vinavyozitumia,havina nafasi katika mustakabali wenye afya. 

REPLY HAPA


image quote pre code