Maumivu ya tumbo upande wa kulia yanasababishwa na nini?

Maumivu ya tumbo upande wa kulia yanasababishwa na nini?

#1

Maumivu ya tumbo upande wa kulia yanasababishwa na nini?



Maumivu ya tumbo upande wa kulia yanaweza kusababishwa na sababu mbalimbali kutegemea eneo halisi (juu au chini) na aina ya maumivu. Hapa chini ni baadhi ya sababu kulingana na sehemu ya maumivu:

1. Upande wa Kulia Juu (Right Upper Quadrant):

Ini (Hepatitis, abscess, fatty liver)

(gallbladder) –  kama mawe kwenye vifuko vya nyongo-gallstones, n.k

Maambukizi ya njia ya juu ya mkojo (pyelonephritis)

vidonda cha tumbo (gastric ulcer)

2. Upande wa Kulia Chini (Right Lower Quadrant):

Appendicitis (kuvimba kwa kidole tumbo) – ni ya kawaida sana

Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)

Maambukizi ya via vya uzazi kwa wanawake (PID)

Mimba ya nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancy)

Ovarian cyst kwa wanawake

Hernia (matumbuko) n.k.

3. Sababu Nyingine za Jumla:

- Tatizo la Gesi tumboni

- Kuvimba kwa utumbo (inflammatory bowel disease)

- Maumivu ya misuli au neva  n.k.

Kumbuka: Maumivu ya ghafla, makali au yanayoambatana na homa, kutapika, damu kwenye kinyesi au kutoweza kupitisha hewa/choo yanahitaji matibabu ya haraka.

JE,UNATATIZO HILI NA UNAHITAJI TIBA?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Reply


image quote pre code