Mtazamo hasi dhidi ya Waaguzi kutoka kwa Jamii wawavunja Moyo

Mtazamo hasi dhidi ya Waaguzi kutoka kwa Jamii wawavunja Moyo

#1

Mtazamo hasi dhidi ya Waaguzi kutoka kwa Jamii wawavunja Moyo



Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania Tawi la Muhimbili , Ramadhan Mwita akizungumza na wauguzi

WAUGUZI wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wameeleza kusikitishwa na mtazamo hasi wa jamii dhidi yao, wakisema jamii inawadhalilisha na kushindwa kutambua mchango wao mkubwa katika utoaji wa huduma za afya.

Licha ya jukumu lao kubwa la kuokoa maisha ya wananchi, wamesema  jamii inapaswa kutambua kuwawana fanya kwa upendo, huruma na weledi, badala ya kuendelea kuwahukumu kwa mitazamo hasi. Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliyoadhimishwa Mei 30, 2025, Mwenyekiti wa Chama cha Wakunga (TANNA) Tawi la Muhimbili, Ramadhan Mwita, amesema wauguzi wamekuwa mstari wa mbele katika kumhudumia mgonjwa kuanzia anapowasili hospitalini hadi kuruhusiwa.

 “Jamii inapaswa kutambua kuwa sisi ni binadamu kama wao, tumeapa kuwatumikia kwa moyo, lakini bado tunadhalilishwa na kukatishwa tamaa,” amesema Mwita. Mwita amesisitiza kuwa licha ya changamoto hizo, uongozi wa hospitali yao inaendelea kuboresha mazingira yao ya kazi ikiwemo maslahi ambayo wanayapata kwa wakati.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Dk. Faraja Chiwanga ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, akimwakilisha Prof. Mohammed Janabi, amesema serikali itaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili wauguzi sambamba na kuboresha maslahi yao. Amesisitiza kuwa maadhimisho hayo ni fursa ya kuwakumbusha wauguzi wajibu wao kwa kuzingatia  viapo vya taaluma yao.

Kaulimbiu ya mwaka huu  ni “Wauguzi Nguvu ya Mabadiliko Duniani”, mnaweka  matumaini na uzima kwa wagonjwa, endeleeni  kuwa nguzo ya matumani na kujitolea kwa kuzingatia utu na ubinadamu,” alisema Dk Chiwanga.

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga hospitalini hapo,   Redemptha Matindi  amesisitiza umuhimu wa huduma za kuvutia zinazomjali mgonjwa kama njia moja wapo ya kuleta mageuzi  katika sekta ya afya.

Amesema wauguzi  wanayo nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko Chanya kwa kuonyesha upendo, huruma  na uadilifu katika kazi zao kila siku, maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Mei 12.

REPLY HAPA


image quote pre code