Iran:Madaktari na waaguzi waagizwa kurudi kazini mara moja,Likizo zote zimefutwa
Tehran, Iran. Wakati mapigano kati ya Iran na Israel yakizidi kushika kasi, taarifa kutoka Iran na Gaza zimezua hofu mpya kuhusu hali ya kibinadamu na usalama wa kikanda.
Iran imeamua kuwaita kazini madaktari na wauguzi wote waliokuwa likizo, huku mashambulizi yakiendelea kati yake na Israel.
Naibu Waziri wa Afya anayeshughulikia Huduma za Tiba, Dk Seyed Sajjad Razavi, ametangaza kufutwa kwa likizo zote za madaktari na wauguzi nchini Iran.
Amesema hatua hiyo imelenga kuhakikisha huduma za afya zinaendelea kutolewa kwa ufanisi huku timu za matibabu zikipatiwa msaada wa kisaikolojia na kiakili ili kuhimili hali ya sasa ya dharura.
“Wahudumu wa afya wote wametakiwa kuwa kazini muda wote katika vituo vya afya, si tu kwa ajili ya kutoa huduma, bali pia kusaidia katika kuimarisha ari na utulivu wa kitabibu kwa wenzao walioko mstari wa mbele,” alisema Dk Razavi kupitia shirika la habari la Tasnim.
REPLY HAPA
image quote pre code