Pombe ya Ulanzi kuhifadhi viumbe vya maabara za kibaiolojia
Moja ya tafiti kuhusu kinywaji cha Ulanzi imefanywa katika Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (MUCE).
Katika tafiti yao waliyoifanya kwa zaidi ya mwaka mmoja, wamegundua kuwa kupitia ulanzi unaweza kutengenezwa nishati aina ya bioethanol kemikali muhimu kwa ajili ya kuhifadhia viumbe katika maabara za kibaiolojia.
Pia wamegundua ulanzi unaweza kuwa malighafi ya kutengenezea vitakasa mikono 'sanitizer', spiriti, mifuko ya plastiki ambayo ni rafiki kwa mazingira, mvinyo wa asili na bidhaa nyinginezo.
baada ya kufanya utafiti walibaini kuwa kupitia ulanzi unaweza kutengeneza nishati aina ya bioethanol.
Nishati aina ya bioethanol ni aina ya nishati mbadala (renewable energy) inayotokana na mchakato wa kuchakata sukari au wanga kutoka kwenye mimea.
"Nishati hiyo ni rafiki kwa mazingira na inaweza kutumika kupikia, koroboi zinazotumia nishati safi pamoja na mafuta kwa ajili ya magari yanayotumia nishati ya bioethanol,".
REPLY HAPA
image quote pre code