Ugonjwa wa Fangasi Sehemu za Siri kwa Mwanaume na Mwanamke

Ugonjwa wa Fangasi Sehemu za Siri kwa Mwanaume na Mwanamke

#1

Ugonjwa wa Fangasi Sehemu za Siri kwa Mwanaume na Mwanamke

Fangasi sehemu za siri ni tatizo la kiafya linalowakumba wanaume na wanawake. Mara nyingi huletwa na aina ya fangasi aitwaye Candida albicans, ingawa kuna fangasi wengine pia wanaohusika kama Trichophyton rubrum na Malassezia. Tatizo hili linaweza kusababisha usumbufu mkubwa, hasa kutokana na muwasho, harufu mbaya, na kutokwa na uchafu sehemu za siri.

Aina za Fangasi Sehemu za Siri

1. Candidiasis ya sehemu za siri (Genital Candidiasis),Hii ndyo chanzo kikubwa kabsa cha Fangasi Sehemu Za Siri na husababishwa na Fangasi anayejulikana kama Candida albicans

2. Tinea Cruris (Jock Itch)

Hii ni aina ya fangasi inayosababisha muwasho kwenye mapaja sehemu ya ndani, ngozi ya karibu na sehemu za siri (hususani kwa wanaume), na huonekana kama vipele vya mviringo.

3. Intertrigo

Ni maambukizi ya fangasi yanayotokea pale ngozi inapogusana na ngozi (kama sehemu za siri, chini ya matiti, kati ya mapaja) hususani sehemu zenye joto na unyevu mwingi.

Dalili za Fangasi Sehemu za Siri



Kwa Wanawake:

  • Muwasho mkali ndani au karibu na uke
  • Maumivu wakati wa kukojoa au kufanya tendo la ndoa
  • Uchafu mweupe mzito kama maziwa mtindi
  • Ngozi kuwa nyekundu, kuvimba au kuwa na vipele
  • Harufu isiyo ya kawaida (ingawa candidiasis mara nyingi haina harufu kali)


Kwa Wanaume:

  • Muwasho kwenye kichwa cha uume,Korodani na Sehemu zingine
  • Ngozi ya uume na korodani kuwa nyekundu na kuvimba
  • Kuwepo kwa mipasuko midogo au ngozi kukauka
  • Maumivu wakati wa kukojoa au tendo la ndoa
  • Mara nyingine kutokwa na uchafu au mabaka meupe kwenye ngozi

Vihatarishi Vikuu vya mashambulizi ya Fangasi Sehemu Za Siri

- Mabadiliko ya homoni (hasa kwa wanawake wajawazito)

- Kujamiiana na mtu mwenye fangasi

- Kuvaa Mavazi yasiyoruhusu hewa ikiwemo nguo za ndani ambazo hazipitishi hewa vizuri (tight underwear/synthetic fabric)

- Mazingira ya Unyevu mwingi sehemu za siri

- Kinga ya mwili kushuka kwa Sababu ya vitu mbali mbali (mfano: HIV, stress, chemotherapy), Kutumia antibiotics muda mrefu, magonjwa kama Kisukari kisichodhibitiwa n.k.

Vipimo na Uchunguzi

  • Daktari anaweza kuchukua sampuli ya uchafu au ngozi ili kuipima chini ya darubini au kupanda kwenye culture (maabara).
  • Kwa wanawake, pelvic exam hufanyika.
  • Kwa wanaume, uchunguzi wa ngozi ya uume au maeneo yaliyoathirika.

Matibabu ya Fangasi Sehemu za Siri

Zipo dawa mbali mbali za Kupaka na Dawa za Kumeza kwa ajili ya kutibu kabsa tatizo hili.

⚠️ Ni muhimu kutumia dawa kwa maelekezo ya Daktari na kwa muda uliopendekezwa hata kama dalili zimepungua mapema.

Njia za Kujikinga za Tatizo hili

  • Vaa nguo za ndani za pamba, zenye kupitisha hewa
  • Epuka kutumia sabuni zenye kemikali kali sehemu za siri
  • Kausha vizuri sehemu za siri baada ya kuoga
  • Usitumie antibiotics bila ushauri wa daktari
  • Fanya tendo la ndoa salama
  • Dumisha usafi wa mwili kila siku

Je Fangasi Hushambulia Mara kwa Mara?

Ndiyo. Baadhi ya watu hasa wanawake hupata maambukizi ya fangasi mara kwa mara (recurrent yeast infections). Hii husababishwa na kinga ya mwili kushuka, matumizi ya antibiotics mara kwa mara, au matatizo ya homoni. Katika hali hii, daktari anaweza kupendekeza matibabu ya muda mrefu au ya kinga (prophylactic treatment).

Madhara ya Kutotibu Fangasi

  • Maambukizi kuenea kwa ndani zaidi
  • Kuathiri mfumo wa uzazi
  • Maambukizi ya kudumu na ya mara kwa mara
  • Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa
  • Maambukizi kwa mwenza n.k.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Vyanzo Vilivyotumika pia (Health Sources):

  1. Centers for Disease Control and Prevention (CDC)
    https://www.cdc.gov/candidiasis/about/?CDC_AAref_Val=https://www.cdc.gov/fungal/diseases/candidiasis/index.html

  2. Mayo Clinic:

  3. Cleveland Clinic

  4. National Health Service (NHS UK)
    https://www.nhs.uk/conditions/thrush-in-men-and-women/

  5. Johns Hopkins Medicine

REPLY HAPA


image quote pre code