WHO yatoa onyo kuhusu kuenea kwa Kipindupindu kutoka Sudan
Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, limeonya kwamba visa vya ugonjwa wa Kipindupindu nchini Sudan vinatarajiwa kuongezeka na vinaweza kuenea hadi nchi jirani .
Mwakilishi wa WHO nchini Sudan Dk Shible Sahbani, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwa njia ya video kutoka Port Sudan kwamba wasiwasi wao ni kuwa kipindupindu kinaenea.
Amesema ugonjwa wa kipindupindu umefikia majimbo 13 nchini Sudan, ikijumuisha Kaskazini na Kusini mwa Darfur ambayo inapakana na Chad, na kwamba watu 1,854 walikuwa tayari wamekufa katika wimbi la hivi karibuni la maambukizi ya ugonjwa huo wa Kipindupindu huku msimu wa mvua ukianza.
Sahbani pia amesema, wanafikira kuwa ikiwa hawatawekeza katika hatua za kuzuia na ufuatiliaji kwenye mfumo wa onyo la mapema, katika chanjo na kuelimisha watu, nchi za karibu pamoja na eneo hilo zinaweza kuathirika.
REPLY HAPA
image quote pre code