#MICHEZO: UEFA imeidhinisha ombi lililotolewa na FA ya Ureno kuhusu kuwepo na dakika 1 ya ukimya kwenye mechi ya timu ya Taifa ya Ureno dhidi ya Uhispania katika mchezo wa Euro 2025 kwa Wanawake utakaopigwa hii leo Alhamis Saa 4.00 Usiku kufuatia kifo cha kushtua cha Diogo Jota.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool ameaga dunia alfajiri ya leo baada ya kupata ajali ya gari akiwa barabarani kaskazini-magharibi mwa Uhispania pamoja na mdogo wake Andre ambaye naye pia amepoteza maisha.
Wakati ulimwengu wa soka ukiendelea kuomboleza vifo vya nyota hao wote wawili, imeripotiwa kuwa sasa kutakuwa na salamu za heshima kwa dakika moja ya ukimya kabla ya mechi hiyo ya EURO 2025 usiku wa leo kama ishara ya kuwaenzi nyota hao wawili.
Mechi gani hutaisahau ambayo amewahi kucheza Diogo Jota?
#DiogoJota
REPLY HAPA
image quote pre code