Saratani ya matiti kwa wanaume imeendelea kuongezeka nchini,

Saratani ya matiti kwa wanaume imeendelea kuongezeka nchini,

#1

Tofauti na miaka ya nyuma, saratani ya matiti kwa wanaume imeendelea kuongezeka nchini, baada ya idadi ya wanaobainika miaka ya hivi karibuni kukua.

Taasisi ya Saratani Ocean Road, ORCI imesema kuna ongezeko la saratani ya matiti kwa wanaume kutoka mmoja kati ya wagonjwa wa aina hiyo ya saratani 100 mwaka 2020, kufikia watano kati ya 100 mwaka 2025.

Meneja Huduma za Uchunguzi wa Saratani na Elimu kwa Umma wa Taasisi hiyo, Dk Maghuwa Stephano amesema saratani ya matiti imeendelea kuwa changamoto kubwa duniani huku Tanzania ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa saratani hiyo.

Amesema saratani ya matiti kwa wanaume imeendelea kuongezeka nchini, tofauti na miaka ya nyuma ambapo idadi ya wanaume waliokuwa wakibainika kuwa na ugonjwa huo ilikuwa ndogo.

“Awali kati ya watu 100 wanaofanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti, ni mwanaume mmoja pekee aliyekuwa akikumbwa na ugonjwa huo, lakini sasa takwimu zinaonyesha kuwa kati ya watu 100, wanaume watano hubainika kuwa na saratani ya matiti,” amesema Dk Maghuwa.

Amesema saratani ya matiti inaweza ikampata mwanaume pia, hivyo kwa sasa kundi hilo nao wanahitajika wajikinge na wafanye uchunguzi wa mara kwa mara ili kujikinga mapema.

Via:mwananchi

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code