Italia haiwezi kuchukua Nafasi ya Iran kwenye kombe la Dunia
Vuta nikuvute katika kutafuta Nafasi kwenye Kombe la Dunia,Pendekezo la Italia kuchukua nafasi ya Iran kwenye Kombe la Dunia la mwaka 2026 lakataliwa,
Mjumbe mmoja wa Marekani anayefahamika kwa jina la Paolo Zampolli alitoa pendekezo kwamba Italia ipewe nafasi ya Iran kutokana na mzozo unaoendelea kati ya Iran, Marekani na Israel,
Hata hivo Shirikisho la Soka Duniani, FIFA limekataa Pendezo hilo,Waziri wa michezo wa Italia, Andrea Abodi na Waziri wa Uchumi, Giancarlo Giorgetti pia wamekataa pendekezo hilo wakisisitiza kwamba kama ni Italia kushiriki Kombe la Dunia lazima ishinde uwanjani na sio kwa njia za aina nyingine kama hii.
You, Mehreen and others
Comment



