Watoto 9 waliozaliwa na Halima Cissé na Kuvunja Rekodi ya Dunia jana wafikisha miaka 5
Watoto tisa hao wanatoka katika familia ya raia wa Mali, mama yao anaitwa Halima Cissé. Walizaliwa akiwa katika hospitali nchini Morocco mwaka 2021, baada ya ujauzito uliokuwa wa nadra sana duniani uliovuta hisia za kimataifa.
Watoto tisa waliozaliwa kwa mpigo na mama raia wa Mali, Halima Cissé, nchini Morocco, wamefikia hatua muhimu ya maisha yao baada ya kutimiza miaka mitano. Tukio lao la kuzaliwa lilikuwa la kihistoria na la kipekee duniani, likiwa miongoni mwa matukio adimu sana ya uzazi wa watoto wengi kwa wakati mmoja.
Watoto hao, ambao walizaliwa wakiwa na uzito mdogo na walihitaji uangalizi wa karibu wa kitabibu mara baada ya kuzaliwa, wameendelea kukua vizuri chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya pamoja na malezi ya familia yao. Safari yao ya maisha imekuwa ya matumaini na kuleta furaha sana hata kwa Watu wengine.
Kwa sasa, wanapoendelea kukua, familia yao imekuwa ikisherehekea maendeleo yao hatua kwa hatua, huku kila mmoja akionyesha ukuaji wa kawaida kama watoto wengine wa rika lao. Tukio hili limeendelea kuwa la ajabu katika historia ya uzazi duniani.

.jpeg)



Bonge la Historia
ReplyDeleteKabsaa
DeletePost a Comment
WEKA MAONI HAPA(Reply)